Hance Mtanashati
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 20,137
- 26,189
Usikute hata huyo pia sio wako.Duuuh yaani nusu mwaka tu unaanza kumtafuta mchawi .
Mm nilikaa 5years kwenye ndoa ndio nikapata mtoto wa kwanza na hatukua na shida yoyote,
Labda niongee jambo Moja japo sio wote wanaweza wakalielewa Kwa haraka
Kupata mtoto sio matokeo ya kufanya tu ngono/tendo la ndoa
Mtoto ni Mungu ndio anaruhusu azaliwe na ndio maan unaona una nusu mwaka mnasex na mko normal na hujapata
Iko hv japo na hii unaweza usiielewe
kila unayemwona kazaliwa duniani huja Kwa sababu maalumu na Kwa wakati maalumu japo sisi wanadamu Huwa tunataman pale tunapotaka mtoto basi tupate wakati huohuo
Ndio maana Kuna mtu unaweza mkuta anawatoto 5 wewe Hata mmoja huna lakin katika hao wa 5 hakuna Cha maana wanachosaidia au leta impacts katika ulimwengu
Halafu wewe wakwako anayechelewa kuja gafla akifika unashangaa anakuja na mambo ambayo Dunia ilikuwa inayasubiri Kwa miaka mingi
Fanya utafiti wako binafsi watoto wengi ambao kuzaliwa kwao kulipatikana kwa namna zisizo za kawaida na wenyewe huwa sio wakawaida
Mfano nimekwambia hapo juu mm nilikaa kwenye ndoa Kwa 5 years wapo wadogo zangu walikuwa na watoto wapo shemeji zangu walikuwa na watoto
Lakini ukweli siku alipozaliwa mwanangu kila mtu aliona sio mtoto wa kawaida yamkini ndio maana alikuwa anachelewa kuja.
Ngoja nitumie mfano huu pengine unaweza nielewa kidgo.
Note: Muda uliozaliwa na mahali ulipozaliwa pamebeba Kusudi lako.
Sijui kama umewahi kuwaza kama Yesu angezaliwa Tanzania je angefanikiwa kutimiza Kusudi?
-Haiko katika tamaduni zetu watanzania kumsulubisha mtu msalabani hata kama amefanya kosa Gani, lakini alizaliwa islael enzi za utawala wa kirumi ambapo hao walikuwa na utamaduni wa kusulubisha wakosaji msalabani.
Lakini pia hata kama angezaliwa hukohuko Islaeli alikozaliwa kma ingekuwa ni Karne hizi vilevile Kusudi lingekuwa gumu kulitimiza Kwa njia Ile
kipindi hiki ambacho Dunia ni kama Kijiji na kwa mtu maarufu kama Yesu asingeweza kuhukumiwa bila kosa , Kisha Dunia inyamaze
Watu wa haki za binadamu wangekuja n.k
Kwanini nimetoa mifano hiyo nataka niendelee kukutia moyo Mtoto sio tu dhana ya matokeo ya tendo la ndoa Bali ni Kusudi la Mungu juu ya kutimiza jambo Fulani duniani
Na ndio maana Kuna mtu anabakwa na kushika mimba papohapo na Kuna wewe unafanya Kwa style zote then hakuna mimba.
Kuna rafiki yangu sitomtaja jina ila yeye alikuwa na kasumba ya kila mkewake akishika mimba inatoka ,zilitoka mimba 5 wakawa wanamwomba tu Mungu
siku Moja akashika mimba nyngine Ile mimba ilikaa siku ya kuja kujifungua alijifungua mapacha watatu wawili ni boys na mmoja ni girls hii sio story ni real kwasasa anaishi Arusha, akajikuta kawapita Hadi wale waliomtangulia kuzaa yeye anawatatu ndani ya miaka 2 wenzake wana mmoja
Nimalize kwa kusema nenda hospital chukua ushauri wote wa daktari fuata taratibu zote ,yawezekana mwanao ndio mkombozi wa Tanzania ya kesho tunayoitaka hivyo anasubiri azaliwe kwa wakati sahihi 🙏🙏