Msaada: Ni zaidi ya nusu mwaka sasa tunatafuta mtoto bila mafanikio, tatizo linaweza kuwa nini?

Msaada: Ni zaidi ya nusu mwaka sasa tunatafuta mtoto bila mafanikio, tatizo linaweza kuwa nini?

Jaribu badili jina na mitazamo nchi kavu haitoi mazao, Kama umechagua ndoa hiyo himaya yako uimbiaje nchi kavu?,
Uliyempata awali hayumo heman mwako kama mama yake hujamwoa na yupo hai hiyo ni nchi inalimwa na yoyote na mwanao anaweza "kula" kitokacho kwa mwanaume yoyote.
Badili mtizamo leo nchi izae
 
Itabd akatoe Handbrake
Duuuh yaani nusu mwaka tu unaanza kumtafuta mchawi .

Mm nilikaa 5years kwenye ndoa ndio nikapata mtoto wa kwanza na hatukua na shida yoyote,

Labda niongee jambo Moja japo sio wote wanaweza wakalielewa Kwa haraka

Kupata mtoto sio matokeo ya kufanya tu ngono/tendo la ndoa

Mtoto ni Mungu ndio anaruhusu azaliwe na ndio maan unaona una nusu mwaka mnasex na mko normal na hujapata

Iko hv japo na hii unaweza usiielewe

kila unayemwona kazaliwa duniani huja Kwa sababu maalumu na Kwa wakati maalumu japo sisi wanadamu Huwa tunataman pale tunapotaka mtoto basi tupate wakati huohuo

Ndio maana Kuna mtu unaweza mkuta anawatoto 5 wewe Hata mmoja huna lakin katika hao wa 5 hakuna Cha maana wanachosaidia au leta impacts katika ulimwengu

Halafu wewe wakwako anayechelewa kuja gafla akifika unashangaa anakuja na mambo ambayo Dunia ilikuwa inayasubiri Kwa miaka mingi

Fanya utafiti wako binafsi watoto wengi ambao kuzaliwa kwao kulipatikana kwa namna zisizo za kawaida na wenyewe huwa sio wakawaida

Mfano nimekwambia hapo juu mm nilikaa kwenye ndoa Kwa 5 years wapo wadogo zangu walikuwa na watoto wapo shemeji zangu walikuwa na watoto

Lakini ukweli siku alipozaliwa mwanangu kila mtu aliona sio mtoto wa kawaida yamkini ndio maana alikuwa anachelewa kuja.

Ngoja nitumie mfano huu pengine unaweza nielewa kidgo.

Note: Muda uliozaliwa na mahali ulipozaliwa pamebeba Kusudi lako.

Sijui kama umewahi kuwaza kama Yesu angezaliwa Tanzania je angefanikiwa kutimiza Kusudi?

-Haiko katika tamaduni zetu watanzania kumsulubisha mtu msalabani hata kama amefanya kosa Gani, lakini alizaliwa islael enzi za utawala wa kirumi ambapo hao walikuwa na utamaduni wa kusulubisha wakosaji msalabani.

Lakini pia hata kama angezaliwa hukohuko Islaeli alikozaliwa kma ingekuwa ni Karne hizi vilevile Kusudi lingekuwa gumu kulitimiza Kwa njia Ile

kipindi hiki ambacho Dunia ni kama Kijiji na kwa mtu maarufu kama Yesu asingeweza kuhukumiwa bila kosa , Kisha Dunia inyamaze
Watu wa haki za binadamu wangekuja n.k

Kwanini nimetoa mifano hiyo nataka niendelee kukutia moyo Mtoto sio tu dhana ya matokeo ya tendo la ndoa Bali ni Kusudi la Mungu juu ya kutimiza jambo Fulani duniani
Na ndio maana Kuna mtu anabakwa na kushika mimba papohapo na Kuna wewe unafanya Kwa style zote then hakuna mimba.

Kuna rafiki yangu sitomtaja jina ila yeye alikuwa na kasumba ya kila mkewake akishika mimba inatoka ,zilitoka mimba 5 wakawa wanamwomba tu Mungu

siku Moja akashika mimba nyngine Ile mimba ilikaa siku ya kuja kujifungua alijifungua mapacha watatu wawili ni boys na mmoja ni girls hii sio story ni real kwasasa anaishi Arusha, akajikuta kawapita Hadi wale waliomtangulia kuzaa yeye anawatatu ndani ya miaka 2 wenzake wana mmoja


Nimalize kwa kusema nenda hospital chukua ushauri wote wa daktari fuata taratibu zote ,yawezekana mwanao ndio mkombozi wa Tanzania ya kesho tunayoitaka hivyo anasubiri azaliwe kwa wakati sahihi [emoji120][emoji120]
Mpeleke kwa daktari atasema, kama aliwekewa kitanzi (Intrauterine contraceptive device ) kikitolewa atazaa tu, kama akili hiyo hana mtaendelea kumsaka mchawi .

Maana hii akiwekewa anasahau kabisa na inachukua miaka mingi sana ku conceive kama hakikutolewa.
 
miezi sita mbona michache, komaa usikute alikuwa anatumia njia za uzazi wa mpango tatizo likaanzia hapo
 
Acha kupanick na msikamie, kuleni mzigo freely ipo siku itaingia tu.Sipatii picha watu wanakuwa wanafanya kwa lengo kuu moja la kutafuta mimba..mnaenjoy kweli??
 
Habari wadau,

Suala hili linaumiza kichwa. Kwa mujibu wa shirika la afya wanasema mwanamke akitimiza mwaka bila kuzaa na anashiriki tendo, basi huyo ni tasa. Sasa ni zaidi ya nusu mwaka mtoto anatafutwa bila mafanikio. Najua humu kuna wataalamu na wajuzi wa hizi changamoto.

Kama mwanamke hana changamoto zozote na mfumo wake uko sawa, tatizo nini. Ni umri? maana ana miaka 37 sasa. Kwani kwa umri huo inashindikana nini kupata ovulation? Wajuzi tusaidiane hapa.
Mkuu wewe umepima????? Kama Huna tatizo?
 
Yah, ninae
Una uhakika ni wa kwako? 👇👇👇

Screenshot_20240621_120952.jpg

➡️➡️➡️ Badala ya kukimbilia kumbebesha lawama mkeo nyote nendeni mkafanyiwe uchunguzi wa kina kuhusu afya zenu za uzazi. Kwako wewe ni lazima kujua kama unazalisha mbegu zenye ubora unaotakiwa, kiasi gani, uogeleaji wake; na hasa kama zinaweza kusafiri kulifikia yai kabla hazijakata moto. Mkeo naye hali kadhalika - afya ya ovaries, mayai anayozalisha, mirija, homoni na mengineyo. Kuwa na hard talk naye na akwambie kama alishawahi kutoa mimba, kutumia dawa za uzazi wa mpango hapo kabla (kawaida ya wanachuo kwenye ndoa bubu zao), kufakamia P2, kama kwao wana tatizo la kupata watoto; na mmengineyo.

Pia tambua kwamba miaka 37 kama ndiye mtoto wake wa kwanza basi atakuwa amechelewa kidogo na kunaweza kuwa na changamoto kwenye kupata mimba hasa hii ya kwanza.

Kama nyote mtakuwa OK basi sioni ni kwa nini msipate mtoto hasa mkiwa chini ya uangalizi wa daktari. Mambo yakiendelea kuwa magumu mnaweza pia kuangalia ustaarabu wa dawa asilia maana inaweza kuwa ni ishu ndogo tu huko ndiyo inakwamisha. Masuala ya kiimani pia yanaweza kuhusika hapa.

Naamini mtoto mtapata ni suala la muda tu. Kwa sasa jitahidini msiwe na presha. Kulaneni tu kwa raha zenu bila kufikiria mimba na mtakuja kushtukia tu kitu tayari. Na utambue kuwa huyo mkeo anakuhitaji sana hasa kisaikolojia. Usijiunge na dada zako (mawifi zake) kumzodoa wala kumsema sema. Kuwa naye karibu. Mtie moyo. Mwaminishe kuwa Mungu Atawapa tu mtoto; na kwamba unampenda sana no matter what. Asipokuwa na msongo wa mawazo pia itamsaidia sana!

Kila la heri mkuu!
 
Kuuna wanaume wa ajabu kweri kweri,kuna binti kadumu kwenye ndoa miaka 8 bila mtoto hadi mwanamume akamfukuza kuwa ni tasa,aliporudi nyumbani nikaanza kumfuatilia akawa ameingia kwenye 18,mara moja baada ya mwezi ananiambia haoni siku zake,kwenda kupima akabainika kuwa na ujauzito,amejifungua sasa mapacha

Wanaume wamekalili utasa uko kwa mwanamke,ndo maana matatizo mengi ya kukosa watoto lawama huelekezwa kwa mwanamke
Mlipima ukimwi kwanza?
 
Habari wadau,

Suala hili linaumiza kichwa. Kwa mujibu wa shirika la afya wanasema mwanamke akitimiza mwaka bila kuzaa na anashiriki tendo, basi huyo ni tasa. Sasa ni zaidi ya nusu mwaka mtoto anatafutwa bila mafanikio. Najua humu kuna wataalamu na wajuzi wa hizi changamoto.

Kama mwanamke hana changamoto zozote na mfumo wake uko sawa, tatizo nini. Ni umri? maana ana miaka 37 sasa. Kwani kwa umri huo inashindikana nini kupata ovulation? Wajuzi tusaidiane hapa.
Pole kwa changamoto, nimewahi kupitia hii....kwetu ilibidi dokta ampe wife dawa za "kuvuruga" mzunguko na akapata mimba.....shida ilikuwa hormones
 
Kwanza nenda hospital kubwa kama Rabinisia, kairuki aghakan au muhimbili.

Kapime ubora wa mbegu zako na wingi, inashauriwa utoe bao lenye ujazo wa 64M sperms & 75% ya hizo sperms ziwe na uwezo wa kujongea na kufanya fertilization.
Kama mbegu zako ziko chini ya kiwango utapewa vidonge vya kuongeza ubora wa mbegu zako na kuongeza uzalishaji.

Mke wako atumie vidonge letrozole kama sikakosea Huwa ni 5 na anaanza kumeza baada tu ya kutoka period.

Kula vizuri, Fanya mazoezi na punguza msongo wa mawazo wa kutaka kupata mtoto Kila unapokutana na mke wako.

Hakikisha Kila siku we piga mbupu, hakuna cha kusubiri siku za hatari wala nn yaani we ni mwenda wa kusuuza lungu tu, utaona kama hajanasa na Kisha utakuja nishukuru.
 
Back
Top Bottom