Msaada: Ni zaidi ya nusu mwaka sasa tunatafuta mtoto bila mafanikio, tatizo linaweza kuwa nini?

Jaribu badili jina na mitazamo nchi kavu haitoi mazao, Kama umechagua ndoa hiyo himaya yako uimbiaje nchi kavu?,
Uliyempata awali hayumo heman mwako kama mama yake hujamwoa na yupo hai hiyo ni nchi inalimwa na yoyote na mwanao anaweza "kula" kitokacho kwa mwanaume yoyote.
Badili mtizamo leo nchi izae
 
Itabd akatoe Handbrake
 
miezi sita mbona michache, komaa usikute alikuwa anatumia njia za uzazi wa mpango tatizo likaanzia hapo
 
Acha kupanick na msikamie, kuleni mzigo freely ipo siku itaingia tu.Sipatii picha watu wanakuwa wanafanya kwa lengo kuu moja la kutafuta mimba..mnaenjoy kweli??
 
Mkuu wewe umepima????? Kama Huna tatizo?
 
Yah, ninae
Una uhakika ni wa kwako? 👇👇👇


➡️➡️➡️ Badala ya kukimbilia kumbebesha lawama mkeo nyote nendeni mkafanyiwe uchunguzi wa kina kuhusu afya zenu za uzazi. Kwako wewe ni lazima kujua kama unazalisha mbegu zenye ubora unaotakiwa, kiasi gani, uogeleaji wake; na hasa kama zinaweza kusafiri kulifikia yai kabla hazijakata moto. Mkeo naye hali kadhalika - afya ya ovaries, mayai anayozalisha, mirija, homoni na mengineyo. Kuwa na hard talk naye na akwambie kama alishawahi kutoa mimba, kutumia dawa za uzazi wa mpango hapo kabla (kawaida ya wanachuo kwenye ndoa bubu zao), kufakamia P2, kama kwao wana tatizo la kupata watoto; na mmengineyo.

Pia tambua kwamba miaka 37 kama ndiye mtoto wake wa kwanza basi atakuwa amechelewa kidogo na kunaweza kuwa na changamoto kwenye kupata mimba hasa hii ya kwanza.

Kama nyote mtakuwa OK basi sioni ni kwa nini msipate mtoto hasa mkiwa chini ya uangalizi wa daktari. Mambo yakiendelea kuwa magumu mnaweza pia kuangalia ustaarabu wa dawa asilia maana inaweza kuwa ni ishu ndogo tu huko ndiyo inakwamisha. Masuala ya kiimani pia yanaweza kuhusika hapa.

Naamini mtoto mtapata ni suala la muda tu. Kwa sasa jitahidini msiwe na presha. Kulaneni tu kwa raha zenu bila kufikiria mimba na mtakuja kushtukia tu kitu tayari. Na utambue kuwa huyo mkeo anakuhitaji sana hasa kisaikolojia. Usijiunge na dada zako (mawifi zake) kumzodoa wala kumsema sema. Kuwa naye karibu. Mtie moyo. Mwaminishe kuwa Mungu Atawapa tu mtoto; na kwamba unampenda sana no matter what. Asipokuwa na msongo wa mawazo pia itamsaidia sana!

Kila la heri mkuu!
 
Mlipima ukimwi kwanza?
 
Pole kwa changamoto, nimewahi kupitia hii....kwetu ilibidi dokta ampe wife dawa za "kuvuruga" mzunguko na akapata mimba.....shida ilikuwa hormones
 
Kwanza nenda hospital kubwa kama Rabinisia, kairuki aghakan au muhimbili.

Kapime ubora wa mbegu zako na wingi, inashauriwa utoe bao lenye ujazo wa 64M sperms & 75% ya hizo sperms ziwe na uwezo wa kujongea na kufanya fertilization.
Kama mbegu zako ziko chini ya kiwango utapewa vidonge vya kuongeza ubora wa mbegu zako na kuongeza uzalishaji.

Mke wako atumie vidonge letrozole kama sikakosea Huwa ni 5 na anaanza kumeza baada tu ya kutoka period.

Kula vizuri, Fanya mazoezi na punguza msongo wa mawazo wa kutaka kupata mtoto Kila unapokutana na mke wako.

Hakikisha Kila siku we piga mbupu, hakuna cha kusubiri siku za hatari wala nn yaani we ni mwenda wa kusuuza lungu tu, utaona kama hajanasa na Kisha utakuja nishukuru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…