Msaada: Nimekuta kibubu kina 30,000/- tu baada ya kuweka pesa karibu miezi 5, nifanyeje?

Hata hapa utapata msaada, kuwa na imani...wanaotoa msaada watakuja in a way hutaelewa🤣

Yote kwa yote pole sana, tumia simu, bank, kufanya savings
 
Ongeza kiwango cha saving.....hakuna miracle hapooo...jibane zaidiii
 
Hapo ukute hakuna Cha chuma ulete Wala Nini Bali mwamba anayekwendaga kula mzigo ndio kakifyatua kiaina hicho kibubu na kukomba mkwanja
 
Dah..... omba msaada tukusaidie sasa acha kulia lia.
 
Yaani unahifadhi pesa nyumbani wakati benki zipo, na hujui zipo kiasi gani! Acheni ujinga mnaishi karne ya 18 huko nyie?
 
Pole sana dada yangu. Najua unapitia mazingira magumu sana maana hali kama yako imewahi kunikuta. Pole kwa mara ya pili.

1.....
Nakumbuka nilikua nimepata hela yangu ya boom nikaweka geto kwangu juu ya meza baada ya siku tatu sikuikuta na hapo hakuna mtu alieingia ndani kwangu nikawaza sana imekuaje ila sikupata jibu

2....
Kwa mara nyingine tena nikapata boom kama kawaida nikaweka ndani ya begi langu hapo ilikua ni ijumaa. Nakumbuka mpaka ijumaa tatu nilikua nimenunua vitu kama vya 30,000 ila cha ajabu kwenda kuangalia salio nikakuta zaidi ya laki moja hakuna hapo nikapagawa tena

3.....
Baada ya matukio yote hayo nikabadili njia ya kutunza pesa ikawa nikichukua hata 100 ya kununua kitunguu naandika ( pesa bila daftari huisha bira habari ) lakini haikusaidia kitu maana kwenye daftari langu nakuta balance ni tofauti na cash in hand ( nakuta labda daftari linasema salio ni 140,000 ila cash ni 120,000 ) hapo twenty wamebeba.

Finally nikapata conclusion or conclution ( sijui ni ipi kati ya hizo ) kuwa huo mchezo ni ule wa chuma ulete

Solution....
Muda huu naifadhi pesa zangu M-PESA japo makato ya kutoa kwa wakala ni tatizo sana kwangu

ANGALIZO

Kama swala kama hilo halijawahi kukutokea basi acha maneno ya kebehi na dharau. Hujui kiasi gani mtu anapitia maumivu makali ya moyo kwa pesa kupotelewa kimiujiza.... So painfull

DONT TAKE THINGS EASILY...DONT SIMPLFY.....Life is not piece of cake.. Pesa inauma sana
 
Mimi ni mdau wa vibubu.
Mara Moja tu niliona negative ya sh. 50k ila nahisi ni issue ya kihesabu tu
Mara nyingi nakuta pesa yangu taslimu maana nahesabu Kila nikiweka, muda mwingine nakuta kaongezeko kidogo.
Wewe ni mweupe ndio maana unachezewa
 
Mimi ni mdau wa vibubu.
Mara Moja tu niliona negative ya sh. 50k ila nahisi ni issue ya kihesabu tu
Mara nyingi nakuta pesa yangu taslimu maana nahesabu Kila nikiweka, muda mwingine nakuta kaongezeko kidogo.
Wewe ni mweupe ndio maana unachezewa
Anaweza asikuelewe, akadhani unazungumzia weupe wa rangi ya ngozi😊
 
Wenzako wanaweka kwenye kibubu cha tigopesa, hapo kuna panya anazila.
 
Uje nikupe 1000000
 
Anza kutumia M Koba ya Voda

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
Pole sana mamy! Badili njia ya uhifadhi pesa uone
 
Pole Sana nadhani maumivu ya PESA ndo maumivu yanayoumiza Sana hapa Duniani
 
Kuna fundi alikua ananionesha maujuzi ya kuiba hela kwenye vibubu hasa alivyotengeneza yeye na bila kuacha ushahidi.

Jinsi ya kufungua madirisha mbalimbali bila kuacha ushahidi.

Huenda sio chuma ulete ni mtu anakulia timing tu.

Nje ya mada, unakaa wapi mkuu wmbako room ni 50k??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…