Msaada: Nimekuta kibubu kina 30,000/- tu baada ya kuweka pesa karibu miezi 5, nifanyeje?

Vibubu almost vyote huwa vinaleta hizi shida, sjajua sababu ni nini lakini mashaka juu ya watengeneza vibubu siwaamini kabisa. Wanajua lazima utahifadhia pesa tu na wanaweza weka chochote ili kukupiga wewe . Kwahivo masuala ya vibubu siyo mazuri kabisa ni Bora ufungue account ya benki. Na simu pia muda Mwingine mtu unapigwa bila kutarajia na matapeli. #BANK MUHIMU SANA NA PIA POLE SANA
You added something in my mind.
Kumbe wezi wa pesa za kwenye kibubu ni mafundi vibubu
 
Habari, Jamani naomba msaada wa aina yeyote ile, nimechanganyikiwa sana sana. Niende kwenye mada;

Mimi ni dada ambaye najishughulisha na biashara ya kuuza matunda, sasa basi nimepanga mahala naishi mwenyewe, nina tabia ya kuhifadhi pesa ndani, yaani ule mfumo wa kuweka kwenye kibubu. Yaani hizi ambazo naweka kwenye kibubu ni kwa ajili ya kulipa Kodi, kwahiyo ndio maana nahifadhi ndani.

Nimeanza kuweka pesa toka mwezi wa 5 mwaka huu, nahifadhi kwa ajili ya kulipa Kodi kwa ajili ya muhula unaofata, Kodi yangu yaisha mwezi wa 10.

Jana wakati nimepumzika nikajikuta natamani kujua hadi sasa nimefikisha sh. ngap ili nione kama naweza kulipa kabisa au niongeze ili itimie nilipe Kodi yangu ya mwezi unaofata, chumba nalipa elf 50 ambayo huwa nalipa kwa miezi 6 ili niwe huru kufanya mambo mengine.

Cha ajabu nilichokuta sijui hata niseme nini, yaani niliishia kulia na kucheka kwa pamoja! Nimekuta elf 30 tu wakati nilikuwa lazima ingekuwa hata laki 2 au zaidi.

Jamani jamni hali ilivyo ngumu halafu unapata janga kama hili kiukweli niliishiwa nguvu, tangu jana hadi leo sijatoka kwenda kokote, nahisi kama naumwa.

Jamani kwa anayefahamu haya mambo ya Chuma Ulete naweza rudisha pesa yangu na kama inawezakana je nifanyeje au ndio nishikuru tuu niongee na mwenye nyumba mapema anipe muda wa kujitafuta?

Yaani sijui hata la kufanya, please please naomba mnisaidie cha kufanya sielewi nifanye nini!
Pole sana. Hapo nakushauri jitafute tena maana huko unakotaka kwenda sijui kwa mganga utapoteza muda wako tu maana utaombwa pesa na utajikuta umelipa pesa nyingine ambayo ingeweza kumlipa mwenyenyumba.
1. Hifadhi hela kwenye simu
2. Benki
3. Weka pesa zako kwenye kitabu au daftari. Uwe unaziweka katika hasa za noti.
4. Weka sehemu za droo kwenye kitanda au droo za tv case.
Hivi vibubu ni hatari sana. Chuma ulete ipo na inafanya kazi
 
Mimi ni mtalaam wa kutoa pesa kwenye kibubu chochote duniani naamini sipo peke yangu mwenye huu ujuzi

Ahsante
 
Mwanamke akichanganyikiwa huwa analose control, akishalose control hujikuta akifanya maamuzi ya hovyo.

TAKE CARE.
 
Nje ya mada. Nyota ya jaha maana yake ninini. Ucje kukuta jina lako linavutia wachumaji.
 
Kama umekuta buku buku zipo kibao basi jua niwewe uliweka ukidhani ni elfu kumi kumi,it happens,you know.Sasa mkuu kwa kuweka buku Kila siku unategemea laki 3 Kwa mwezi kweli?Hiyo laki 270 akuongezee nani?Anyway Kuna vibubu vya simu skuizi tuishi humo,ila usijesema nao chuma ulete
 
Hicho kibubu ulitenge eza mwenyewe?
Kama ulinunua pole.. Mchawi wako ni mtengenezaji.. Hao watu wakitengeneza huwa wananuwia.. So ukiweka hela ni kama umempa chuma ulete..

Inashauriwa utengemeze mwenyewe
 
Habari, Jamani naomba msaada wa aina yeyote ile, nimechanganyikiwa sana sana. Niende kwenye mada;

Mimi ni dada ambaye najishughulisha na biashara ya kuuza matunda, sasa basi nimepanga mahala naishi mwenyewe, nina tabia ya kuhifadhi pesa ndani, yaani ule mfumo wa kuweka kwenye kibubu. Yaani hizi ambazo naweka kwenye kibubu ni kwa ajili ya kulipa Kodi, kwahiyo ndio maana nahifadhi ndani.

Nimeanza kuweka pesa toka mwezi wa 5 mwaka huu, nahifadhi kwa ajili ya kulipa Kodi kwa ajili ya muhula unaofata, Kodi yangu yaisha mwezi wa 10.

Jana wakati nimepumzika nikajikuta natamani kujua hadi sasa nimefikisha sh. ngap ili nione kama naweza kulipa kabisa au niongeze ili itimie nilipe Kodi yangu ya mwezi unaofata, chumba nalipa elf 50 ambayo huwa nalipa kwa miezi 6 ili niwe huru kufanya mambo mengine.

Cha ajabu nilichokuta sijui hata niseme nini, yaani niliishia kulia na kucheka kwa pamoja! Nimekuta elf 30 tu wakati nilikuwa lazima ingekuwa hata laki 2 au zaidi.

Jamani jamni hali ilivyo ngumu halafu unapata janga kama hili kiukweli niliishiwa nguvu, tangu jana hadi leo sijatoka kwenda kokote, nahisi kama naumwa.

Jamani kwa anayefahamu haya mambo ya Chuma Ulete naweza rudisha pesa yangu na kama inawezakana je nifanyeje au ndio nishikuru tuu niongee na mwenye nyumba mapema anipe muda wa kujitafuta?

Yaani sijui hata la kufanya, please please naomba mnisaidie cha kufanya sielewi nifanye nini!
Miezi mingi haimaanishi pesa nyingi mkuu, ulikuwa unaweka bukubuku halafu unapitisha siku nyingi bila kuweka
 
Back
Top Bottom