Msaada: Nimekuta kibubu kina 30,000/- tu baada ya kuweka pesa karibu miezi 5, nifanyeje?

Msaada: Nimekuta kibubu kina 30,000/- tu baada ya kuweka pesa karibu miezi 5, nifanyeje?

Kibubu mtu anqweza kuiba kirahis tu kama akiamua mm nishawahi weka Hela nikabanwa😀 nikachukua kiwembe nikachonga kidogo kwenye tundu nikatoa Hela na kijiti na kibubu kikabaki kma kilivo na sio rahis mtu kujua 😀😀
NB.sikuiba zilikuwa zangu
Na kuhus chumaulete nasikia ipo sana hasa ukinunuaVibubu mitaani
Njia rahis tafuta kopo mfano la chupa ya lotion iloisha yenye tundu dogo weka hii unatunza hata kwenye begi la nguo unafunga sio rahis mtu kujua ndani kuna Hela
watengenezajiwwenyewe ndio wanaviwekea usinunue kibubu kiennyeji
 
Kububu sio njia salama sana ya kutunza fedha yako…bora kweny lain

Napo kibubu hakitakusaidia kukuza misuli yako ya utunzaji fedha

Ifike point mtu uweze kuweka fedha sehemu ya wazi ama kwenye simu na unakua na uwezo wa kutoitumia bila utaratibu.

Hii n point muhmu kwnye maisha,sio fedha n yako lkn Una struggle kuipata Una struggle na kuitunza…
 
Ukweli nami nina kibubu. Naweka hela nzuri tu. Nimeshaambiwa kuhusu haya mambo ya chuma ulete. Itabidi niamini tu, ila sina mpango wa kukivunja kwa sasa. Huwa nakitikisa kusikiliza, nasikia noti.za kutosha.

Namuuliza dada huyo, hakuwa akitikisa kupima kiasi? Binafsi nataka nikusanye kwa mwaka mzima na nikija kuvunja nikute mil 6 hivi
 
Kibubu noma sita sahau nlikuta elfu 70 pesa tulikua tuna save kila siku elf 20 kwa miezi 5
 
Hiyo pesa imechukuliwa na mtu wako wa karibu (mpenzi, rafiki au ndugu).. Kumbuka ndani ya kipindi chote ulichokuwa unaweka pesa kwenye kibox, kama kuna mmoja kati yao alikutembelea na kumwacha ndani walau dk kadhaa akiwa peke yake..

Mambo ya chuma ulete yapo lakini kwa suala lako sidhani kama ni chuma ulete..
 
Hiyo pesa imechukuliwa na mtu wako wa karibu (mpenzi, rafiki au ndugu).. Kumbuka ndani ya kipindi chote ulichokuwa unaweka pesa kwenye kibox, kama kuna mmoja kati yao alikutembelea na kumwacha ndani walau dk kadhaa akiwa peke yake..

Mambo ya chuma ulete yapo lakini kwa suala lako sidhani kama ni chuma ulete..
Haya mambo mpaka yakupate ndio uta pata experience vinginevyo unaweza hisi mzaha
 
Haya mambo mpaka yakupate ndio uta pata experience vinginevyo unaweza hisi mzaha
Sijakataa kuwa hayapo bali nilichomaanisha ni kuwa watu wa karibu yako ndio wanaokuibia.. Mtu anaiba kwenye kibenki kwa kuwa anajua wewe muhusika huwezi kujua kwa haraka na inaweza pita hata miezi kadhaa ndipo uje kugundua kuwa umeibiwa..

Mwizi wa kwenye kibenki anaiba kila anpopata nafasi na hata ukimwuliza mtoa mada hiyo 30k aliyoikuta ni pesa ambayo anaiweka ndani ya wiki mbili tu.
 
Nenda NMB fungua acc ya chapchap achana na vibubu ukute fundi ndo muhusika wa hiyo mbanga
 
Kwanza pole sana kwa mkasa uliokufika, kwa kweli janga siyo dogo lakini maisha yanaendelea.

Tuliza mawazo kwanza ili pressure iweze kushuka halafu ndiyo unaweza kuona nini la kufanya. Kwa kweli la kufanya ni kuanza kusevu tena, lakini hivi hakuna njia nyingine zaidi ya kibubu? Huna akaunti benki angalau kila mwisho wa wiki hata ukahamisha kwa simu?

Usiogope nenda benki ukafungue akaunti, kila ukipata fedha ziweke kwenye simu halafu mwisho wa wiki unazihamishia kwenye akaunti yako. Hapo chuma ulete hatokupata.
Nadhani kwanza tujiulize hela yake imepoteaje? Sidhani kama ni chuma ulete.

Mimi nahisi alimpa mtu siri hasa likijana fulani jobless limpenzi lake, lilipofika likamvizia kaenda bafuni au dukani likafungua kibubu chake.

Kama ni kibubu vha mbao kufungua ni dakika sifuri tu.

Sasa bi dada hebu tuambie hakuna mtu unamsuspect??
 
Habari, Jamani naomba msaada wa aina yeyote ile, nimechanganyikiwa sana sana. Niende kwenye mada;

Mimi ni dada ambaye najishughulisha na biashara ya kuuza matunda, sasa basi nimepanga mahala naishi mwenyewe, nina tabia ya kuhifadhi pesa ndani, yaani ule mfumo wa kuweka kwenye kibubu. Yaani hizi ambazo naweka kwenye kibubu ni kwa ajili ya kulipa Kodi, kwahiyo ndio maana nahifadhi ndani.

Nimeanza kuweka pesa toka mwezi wa 5 mwaka huu, nahifadhi kwa ajili ya kulipa Kodi kwa ajili ya muhula unaofata, Kodi yangu yaisha mwezi wa 10.

Jana wakati nimepumzika nikajikuta natamani kujua hadi sasa nimefikisha sh. ngap ili nione kama naweza kulipa kabisa au niongeze ili itimie nilipe Kodi yangu ya mwezi unaofata, chumba nalipa elf 50 ambayo huwa nalipa kwa miezi 6 ili niwe huru kufanya mambo mengine.

Cha ajabu nilichokuta sijui hata niseme nini, yaani niliishia kulia na kucheka kwa pamoja! Nimekuta elf 30 tu wakati nilikuwa lazima ingekuwa hata laki 2 au zaidi.

Jamani jamni hali ilivyo ngumu halafu unapata janga kama hili kiukweli niliishiwa nguvu, tangu jana hadi leo sijatoka kwenda kokote, nahisi kama naumwa.

Jamani kwa anayefahamu haya mambo ya Chuma Ulete naweza rudisha pesa yangu na kama inawezakana je nifanyeje au ndio nishikuru tuu niongee na mwenye nyumba mapema anipe muda wa kujitafuta?

Yaani sijui hata la kufanya, please please naomba mnisaidie cha kufanya sielewi nifanye nini!
Umeibiwa tu kawaida dada. Hakunaga Cha chuma ulete Wala Nini.
Ni ujinga na upuuzi tu kuamini ushirikina kiasi hicho. Weka mtego Kuna mtu kakuzunguka
 
Natamani kukuuliza unaishi na nani, unatembelewa na nani, nani unamwamini anabaki ndani kwako wakati mwingine.... Si kila pesa inayopotea inachukuliwa na chuma ulete
 
Vibubu almost vyote huwa vinaleta hizi shida, sjajua sababu ni nini lakini mashaka juu ya watengeneza vibubu siwaamini kabisa. Wanajua lazima utahifadhia pesa tu na wanaweza weka chochote ili kukupiga wewe . Kwahivo masuala ya vibubu siyo mazuri kabisa ni Bora ufungue account ya benki. Na simu pia muda Mwingine mtu unapigwa bila kutarajia na matapeli. #BANK MUHIMU SANA NA PIA POLE SANA
 
Natamani kukuuliza unaishi na nani, unatembelewa na nani, nani unamwamini anabaki ndani kwako wakati mwingine.... Si kila pesa inayopotea inachukuliwa na chuma ulete
Vibubu MzeeWakazi sio Poa Kabisa, Siyo huyo tu wengine wanaviwekea na kufuri kabisa lakini akija kuhesabu ni empty mzee
 
Back
Top Bottom