Msaada: Nimekuwa mkimya na mgumu sana kuzoeana na watu

Msaada: Nimekuwa mkimya na mgumu sana kuzoeana na watu

mimiamadiwenani

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
5,718
Reaction score
7,784
Hali zenu, SakoKwaBako!

Kile nilichokuwa nahisi kuwa ni kweli, hatimaye kimejidhihirisha kuwa ni kweli, na hii imedhihirisha kuwa nilikuwa sahihi kuwaza hivyo.

Tatizo langu ni la saikolojia, ndivyo watu wa karibu wanavyosema. Nina matatizo yafuatayo:

1. Ni mkimya sana mpaka nakera. JF ni sehemu ninayojiachia sana. Napenda kutoongea na kuwa kimya muda mwingi. Nimezubaa mno hali inayopelekea kukosa marafiki wengi. Sina marafiki kabisa.

2. Ni mgumu mno wa kuzoeana na watu, mara nyingi napenda kukaa ndani. Naweza nikaamka asubuhi nikakaa ndani mpaka saa 1 jioni, nikala kisha nikarudi ndani.

3. Wengi wananiambia nitaishi maisha magumu mno, hasa ikitokea ninataka kuomba kazi ya kuajiriwa. Hii ni kutokana na kuwa mabosi wengi wanataka watu wachangamfu na waongeaji. Mimi sipo hivyo.

4. Ninapenda muziki, napenda new trends in technology, napenda siasa.

5. Kimsingi inafika wakati najiogopa kwa kweli. Maneno ya watu yananitisha sana. Najiuliza nikaombewe? Au nimerogwa?

NB: Toka utoto nipo hivi. Pia, nikiwa serious kidogo tu unaweza kusema nimechukia, kumbe hata sijachukia. Sura yangu ni tough kiasi. Hali hii inapelekea niwe natabasamu kila nikiongea na mtu, ili nisiwatoe on mood kwa kudhani nimekasirika.

Mimi kwa unyenyekevu mkubwa, naomba msaada. Mficha uchi hazai.

Nimejaribu kila njia nimeshindwa. Kuwapapatikia watu napo nimeshindwa kabisa. Siwezi kufosi uchangamfu kabisa. Help please!
 
3. Wengi wananiambia nitaishi maisha magumu mno, hasa ikitokea ninataka kuomba kazi ya kuajiriwa. Hii ni kutokana na kuwa mabosi wengi wanataka watu wachangamfu na waongeaji. Mimi sipo hivyo.
Always swali langu hua ni hapa kwa nyie so called introvert, once umeweka mwenyewe let's go.

Hapa inamaanisha huna kazi elezea unaishije bila kazi au unategemea wazazi??
 
ephen wanna see that grumpy face...🤣
3aaed9a10719cd2e1f19ff866dbd534b.png
 
Kwa taarifa tu wengi tuliopo social media tuko hivyo binafsi Niko hivyo na hadi Sasa naona ndio maisha yangu Sina namna ila natambua mchango wa majirani nikitoka nje nasalimia vizuri kabisa wengine wanaitikia wengine wanapiga kimya ni life hela ya taka natoa hela ya ulinzi natoa lift nikitaka kuondoka natoa ila ndani kwangu nje ya girl friend hakuna ambae amewahi kuingia labda mama shadya nikiwa naumwa alinisaidia sana
 
Back
Top Bottom