Msaada: Nimekuwa mkimya na mgumu sana kuzoeana na watu

Msaada: Nimekuwa mkimya na mgumu sana kuzoeana na watu

Dah hata mm nipo hvo hasa wikend sidhan kama huwa wananiona hata nje pale kumbe nakuwa ndani nime myuti tu hasa nikiwa zang nachek movie kwenye cm inakuwa #kizazi_cha_nzi
 
Mkuu, upo kawaida endelea kujipenda na kujikubali. Wewe ni wewe usijifananishe na yeyote yule. Wewe ni mshindi tayari na umekamilika
 
Hakuna tatizo hapo! Labda kama wewe ndo unalitafuta
Mimi ni mkimya nina grumpy face kama wewe na maisha yanaenda.
Kwa mwanamke ukimya unafaa wala hauna shida maana utachangamshwa tu.
Na kama ni mzuri ndo kabisaa ukimya kwako ni siraha.

Ila kwa Me ni tofauti, ukimya kwa hapa kwetu sometimes unaumiza na kufanya ukose baadhi ya fursa.
 
Bahati mbaya mimi sio mchaga ila nawapenda wachaga kwanini umesema mimi niroboti mkuu?😁😁😁
Robotic behavior hasa kwenye uwezo kubonyeza kitufe cha Like kwenye threads nyingi ni sababu ya kukufikiria wewe ni robot .
 
Mimi pia nimeishi hivyo utoto wangu wote ila nilianza kuchange baada ya kuish uboyzini na nilipoanza kufanya biashara na kaz za hapa na pale basi ile Customer care ikanimix na jamii, kwa sasa atleast ninaconfidence kubwa sana ila nimemaintain kiburi tu kwa kuwapuuza baadhi ya watu.

Kama hatuna story common (ziwe za maana hata za hovyo) na hatuna biashara tunaeza tusiongee miaka buku ila salam uhakika.
Mkuu unafanya meditation?
 
Hali zenu, SakoKwaBako!

Kile nilichokuwa nahisi kuwa ni kweli, hatimaye kimejidhihirisha kuwa ni kweli, na hii imedhihirisha kuwa nilikuwa sahihi kuwaza hivyo.

Tatizo langu ni la saikolojia, ndivyo watu wa karibu wanavyosema. Nina matatizo yafuatayo:

1. Ni mkimya sana mpaka nakera. JF ni sehemu ninayojiachia sana. Napenda kutoongea na kuwa kimya muda mwingi. Nimezubaa mno hali inayopelekea kukosa marafiki wengi. Sina marafiki kabisa.

2. Ni mgumu mno wa kuzoeana na watu, mara nyingi napenda kukaa ndani. Naweza nikaamka asubuhi nikakaa ndani mpaka saa 1 jioni, nikala kisha nikarudi ndani.

3. Wengi wananiambia nitaishi maisha magumu mno, hasa ikitokea ninataka kuomba kazi ya kuajiriwa. Hii ni kutokana na kuwa mabosi wengi wanataka watu wachangamfu na waongeaji. Mimi sipo hivyo.

4. Ninapenda muziki, napenda new trends in technology, napenda siasa.

5. Kimsingi inafika wakati najiogopa kwa kweli. Maneno ya watu yananitisha sana. Najiuliza nikaombewe? Au nimerogwa?

NB: Toka utoto nipo hivi. Pia, nikiwa serious kidogo tu unaweza kusema nimechukia, kumbe hata sijachukia. Sura yangu ni tough kiasi. Hali hii inapelekea niwe natabasamu kila nikiongea na mtu, ili nisiwatoe on mood kwa kudhani nimekasirika.

Mimi kwa unyenyekevu mkubwa, naomba msaada. Mficha uchi hazai.

Nimejaribu kila njia nimeshindwa. Kuwapapatikia watu napo nimeshindwa kabisa. Siwezi kufosi uchangamfu kabisa. Help please!
Tatizo Hilo llkitaalamu linaitwa ubandidu jumuishi...halitibiki ila linataka ujikubali kwa kuwa huwezi kujibadilisha.
 
Back
Top Bottom