Msaada: Nimepewa siku 30 niondoke nyumbani kwa Baba mkubwa

Usinung'unike,usikasilike wala usione Baba mkubwa kama ni mbaya kuna muda mwingne changamoto unayokutana nao ndio mpenyo wako wa kutoka mahala na kufika mahala so kaza moyo wako ndio ukubwa huo
 
Hii ya kulia chumbani dah..nlikaa kwa watu mnapika ugali kidogo na mlenda mchana usiku hampiki ndo hadi kesho halafu anamuagiza mumewe nyama choma wanalia chumbani nyumba haina ceiling board basi harufu inakuumiza sa nne hiyo..unahesabu kenchi tu huku unameza mate..nikikumbuka nacheka sana.
 
Yaan unawaza unanyimwa msos ili iweje..hahaha
 
Chanzo ni huyo mke wa baba yako mkubwa. Asilimia kubwa ya ndugu wa mama ndio ndugu zako hao ndugu wa baba ni wa kubahatisha sana.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Hatari sanaaa..

Sent from my SM-G611K using JamiiForums mobile app
 
Mkuu umekumbusha kipindi kimoja nilikaa kwa father wangu mkubwa ki ukwel nilibweteka sana alivyonichoka akapiga sim kijijjn akanichafua kwamba natembea na mke wake habar ikanifikia nililia sana ikabid nijiongeze nikapata kaz ya promotion kutembeza bidhaa mtaan aisee hiyo kaz ni ngumu lakn nilikomaa kwa hasira kutokana na manyanyaso ya bamkubwa nilisema kwake sirud na takomaa mjin hapa hapa mpaka sasa akiwa kakwama pesa au watoto wake wamekwama ada ananiomba namsaidia bila kinyongo RIP mama yangu mdogo ungekua hai ungeona ushauri wako uliponifikisha hakika ww Takukumbuka daima
 
Huyo Dada yako alikua anajidharaulisha kwa mumewe bila kujijua,kitendo cha yeye kukwepa kukupa chakula wewe ndugu yake wa damu ni roho mbaya sana ambayo itafanya hata huyo mumewe asimuamini tena.

mbaya zaidi sisi wanaume huwa hatunaga mambo hayo,ukiona mwanaume ana tabia za kijinga za kusurpot upuuzi wa mkewe ujue kashikwa.

mimi nimeishi na dada pia,ila aliyekuwa anakaa upande wa mzazi ni shemeji yangu,mara nyingi dada ndiye alikuwa ananitolea boko.
 
Niliwahi ishi kwa ndugu nyakati Fulani aisee madhira niliyokutana nayo acha tu .

Siku hizi hata sitii mguu kwao labda tukutane kwenye matukio tu .
 
Jinsia yako tafadhali
 
Baba mkubwa wako yuko vizuri na anakusaidi mshukuru sana.

Soma hii ni story ya kweli
Mwandiko wangu siyo mzuri sana lakini angalau unaeleweka.

Mwaka 2016
18/3/2016 asubuhi mjomba angu mmoja mme wa Shangazi yangu aliamka asubuhi sana, akamwamsha mwanae wa kwanza(First Born) ambaye siku hiyo ilikuwa ni kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa(birthday). Kijana likuwa ana timiza miaka 25.

Mjomba akamwambia toka nje na kila kitu kilicho chako weka kwenye gari fanya haraka una nusu saa za kukusanya kila unachoona ni cha kwako kwenye nyumba yangu.

Kijana alifikiri labda baba yake siku hiyo alikuwa amerukwa na akili lakini siyo hivyo baba alikuwa na akili zake timamu kabisa. Kijana akakusanya nguo, Computer ya mkononi na baadhi ya vitu ambavyo aliona kwake ni vya kwake.

Baada ya kukusanya akaweka ndani ya gari, mzee akawasha gari na kumwambia kijana wake aingie ndani ya gari. Mzee akapiga horn kadhaa getini mlinzi akafungua geti, mzee akaendesha gari umbali mrefu akikatiza mitaa kadhaa ya jiji la Dar es salaam, kisha akafika eneo alilokusudia na kusima kisha akamwamru mtoto wake ashuke, ashushe na vitu vyake aingize kwenye nyumba mbele ya gari yao ilipo park.

Kijana akashusha na na kuingiza ndani, nilikuwa ni Nyumba kubwa vyumba viatu na sebule, choo cha ndani, jiko, na sehemu ya kuhifadhia vifaa (store), nyumba ile ilikuwa na kila kitu ndani tv, fridge, makochi, meza, vyombo, vitanda na samani mhimu za ndani.

Maneno ya mzee
Mwanangu(Jina) siku kama ya leo ulizaliwa huko kanda ya ziwa nakumbuka ilikuwa asubuhi majira ya saa kumi na mbili, hivyo leo unatimiza miaka 26. Nimefanya kila kitu ambacho nadhani ni mhimu kwangu mimi kukifanya na kama kuna kitu unadhani bado unanidai utaniambia nikutimizie kama kutakuwa na umhimu huo.

Umesoma kuanzia unamiaka 6 hadi ukiwa na miaka 22 tayari ulikuwa unaelimu ambayo mimi naona inakutosha kuanzia maisha. JaPo sijaona jitihada zako za kutafuta kazi/ajira kila siku nakuacha umekaa ndani unachat facebook na bbm, ukichoka unaangalia tv na kucheza magem, unakuvywa na kula unavyotaka, unalala muda unaoamua wewe.

Sasa kuanzia leo nimekufukuza rasmi nyumbani kwangu, na ninakukabidhi nyumba hii nimekupangishia utakaa kwa muda wa miezi 6 baada ya hapo utatakiwa kuliPa kodi kama utaamua kiendelea kukaa kwenye nyumba hii. Kumbuka mwanangu vitu vyote ulivyovikuta humu ndani siyo vya kwako ni vya mwenye nyumba.

Utatakiwa kulipa umeme na maji kuanzia mwezi ujao. Nakukabidhi na hiki kiasi cha Tsh laki 5 kitakusaidia kuanza maisha. Kumbuka hautakuwa na gari wala usije ukarudi nyumbani, ukija nyumbani njoo kutusalimia na siyo kuishi kwa heri mwanangu(jina).
••••

Mjomba akamwacha mwanae kwenye mazingira hayo kijana alijiuliza sana, akalia na kumuona baba yake hajamtendea haki kabisa.

Lakini ndo' hivyo mzee alikuwa ameamua, hakuweza kukataa. Alikaa akili ikaanza kumji na kuanza kuhangaika kutuma maombi ya kazi sehemu tofauti tofauti. Kwa muda wa miezi minne akiwa anahangaika akaanza kufanya kibarua kwenye moja ya duka la baba yake, akaajiliwa kama mfanyakazi wa kawaida kabisa.

Yule kijana kiburi na dharau viliisha akawa mtu wa malaengo. Baada ya kufanya kazi kwa miezi miwili dukani kwa baba yake akabahatika kuitwa kwenye usaili kwenye taasisi moja ya serikali akafanikiwa kuajiriwa serikalini.

CHA KUSHANGAZA
Akaendekea kulipa kodi ya nyumba aliyokuwa anaishi kwa zaidi ya miaka miwili. Siku moja aligundua kuwa hata ile nyumba aliyokuwa anaishi ni nyumba ya baba yake na kodi alikuwa analipa kwenye akaunti ya baba yake (akaunti ya bank ilikuwa imesajiliwa kwa jina la mradi NYUMBA INVESTIMENT.

sijui ilikuwaje hadi kijana akafahamu hilo.

Kwa sasa kijana huyo ni mtu mzima sana ana maisha mazuri na familia, amejenga, ana gari, ana biashara na ni mwajiriwa wa serikalini.

Kijana huyo huwa abamshukuru sana baba yake kuwa alimfanya ajitambue.

KUHUSU MJOMBA
ukitoka mkoani ukaamua uende kumtembelea anakuuliza utakaa siku ngapi na umekuja kufanya nini Daslam. Use na sababu za mhimu siyo eti Nimekupa kukaa ukimwambia umekuja ukapa anakutimua anakwambia sitaki niwe kikwazo cha wewe kushindwa kutimiza Ndiyo zako. Kitendo cha mimi kukuruhusu kukaa kwangu Bila kazi yoyote eti kwa sababu wewe ni ndugu yangu noooollo.


Kijana jifunze
Hivi ni story ya Kweli akaniambia kaka ambayo ndiyo mhusika kwenye hii story. Na Mzee wake yaani mjomba langu huwa anaigusia hisia.

Langu jina inaitwa
Machepele Tanzania
 
Una umri gan? Na jinsia yako
Hata mm ningekuwa baba yako mkubwa ningekufukuza tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…