Wakuu salamu natuamini mnaendelea na mapambano ya kila siku na mapambano ya Tozo. Samahani kwa uandishi wangu mimi sio expert sana wa kujielezea kwa maandishi.
Mwaka 2019..
Nilikuwa na mahusiano na binti mmoja, ambaye kwa muda huo ndo alikuwa main huyu tumuite R. Basi nilikuwa na mahusiano nayo kama miaka miwili hivi.. kufikia 2019 alihamishiwa mkoa fulan kwenye halmashauri fulan. Basi nikabaki kidume mwenyewe DSM ikaenda kama miezi sita.. basi kama ujuavyo upweke mbaya, nikaja kuwa na mazoea na binti fulani huyu tumuite S .. basi nkawa na mazoea mwisho wa siku yakawa mahusiano na huku R hajui hili wala lile.. kama Dec R akaomba likizo kuja DSM.
Sasa kwenye likizo yake 2020 akaja kujua nina mahusiano na S. Na ugomvi ukawa mkubwa wakaitakana huko na kutaka kuja kwangu kunifanyia fujo. Uzuri rafiki yangu alinitonya(huyu jamaa anaongea na R). Baada ya ugomvi si unajua tena wanaume kila sehem nkaenda kuomba msamaha na kumfanye amuone adui mwenzake (wazungu wansema divide and conqur) basi baada kuona hiyo inashindanyika nikamuacha R akarudi zake kazini. Mimi nkipambna na S..
Sasa kwa upande wa S nikaendela nae lakini huku nikimuwaza R.. sasa kuna kipindi mambo yakaja kuwa mabaya na nikatengana na S maana nae alisafiri.. nikaendelea na shughuli zangu..
2021
Nikakutana na R si unajua tena (kiporo hakihitaji moto mwingi) nkashangaa nimerudiana na R na mapenzI shamu shamu .. msamaha nkaomba na maisha yakaendelea..
2022 Feb
Mungu akatujalia R akashika ujauzito na nikawa najipanga kwaa ajili ya taratibu za kwenda kujitambulisha.. wakati nipo kwenye harakati za kuweka mambo sawa.. mara jion nashangaa txt iniangia kwenye simu yang, na alienitxt, S na tukaongea machache nkamsadia ya shida kuna sehem alikuwa amekwama kipesa.
2022 June
Sasa mama watoto wang future wife wakati yupo mkoani.. Bas mazoea na yule binti S yakawa kama yamerudi na kimasiraha, nikawa nimeshaweka na kipindi hicho amesema hakuwa na mtu, kiasi fulan hakuwa mtu wa mambo mengi na mimi ndo nilimzinguaga kipind kile..
Sasa juzi hapa kaja kwangu na kuniambia kuwa ana ujauzito wangu.. yaan kama nina watoto wawili wapo njiani.. na kwao pia nimeambiwa natakiwa niende nikajitambulishe..
Kiukwel wote nawapenda ila dini yangu hairuhusu kuwa na wake wawili.. Na hata kama zinaruhusu ila wao hawapatani.