Msaada: Nyoka Mkali anazunguka Mazingira ya Nyumbani

Fanya mazingira ya nyasi au vichaka vilivyozunguka nyumba yako kuwa wazi kabisa yaani kuwe peupe kusiwe na kitu kinachofunika kuta za nyumba nitahidi kila siku kuchoma choma taka na kuwe na kitanuru fulani kinachofoka moshi kila saa atahama
 
Kama alijeruhiwa na paka huyo nyoka anaenda kufa hutomuona tena maana nyoka huwa haponi jeraha bali linaoza
 
Nyoka gani mwingine anafanya multiple bites? Afrika, Kenya?
Multiple bites sio kigezo pekee cha kutambua aina ya nyoka. Hao ni wanyama wanaweza kuwa na tabia tofauti. Lakini kwa koboko hayo ni maumbile yake hawezi kupiga dry bite, akikugonga sumu lazima itoke. Lakini kama nilivyosema hawa ni wanyama: na kama ni koboko kweli basi alijeruhiwa akawa hawezi leta madhara.
Kuna msemo usemao kwamba ni wachache sana wanaogongwa na nyoka ambao huwaona nyoka waliowagonga unless huyo mtu alikuwa anacheza na nyoka anayemfahamu ni aina gani. Lakini mtu atagongwa halafu atasikia majani tu ya nyoka anayekimbia. Hii haimuhusu puff adder (kifutu) ambaye huwa haondoki eneo la tukio.
 
Pia ushauri mwengine, mkipenda na mkiweza tafuteni watu wa fumigation, labda mnawezapata ufumbuzi.
 
Dah una roho mbaya sana kwa mfano ukasikia kati ya wale vijana mmoja amefariki kwa kugongwa na nyoka utajisikiaje?
 
Mkuu poleni sana,lakini nyoka hua anapigwa na paka! Sasa sijui inakuaje,Nyoka amuue paka! Anyway dawa ya nyoka ni kumwaga mafuta ya taa au diesel au chomeni mataili!
inategemea na nyoka mkuu, mimi paka wangu aliwahi kuua nyoka nikashangaa anakuja nae anataka kumuingiza kwenye mabanda ya kuku kwa kipindi hicho yalikuwa wazi. nilichofanya ni kumnyang'anya yule nyoka na kwenda kumfukia ila kadri siku silivyokuwa zinasogea paka alizidi kudhoofika nilijaribu kumtibia lkn haikuwezekana akafa ndani ya mwezi mmoja.

kilichoniuma zaidi siku aliyokufa alipata nguvu akaja miguuni kwangu akalala na ndio akaishia hapo.
 
Ndiyo maana nimeuliza hivyo kama kuna nyoka mwengine anafanya hivyo.

Anyway, considering kuna mtu alimuua nyoka mmoja kwa panga hiyo inamaanisha waliweza kumuona au?

 
Sidhani kama ni kweli, mimi nilichoma juzi baada ya kuona nyoka chooni kwangu ila hakutoka hadi leo vinginevyo iwe alifia humo baada ya kuchoma maana hakuonekana kabisa.
kwa hiyo mzee tangu juzi hujapupu au unapupu kwa jiranj!?
 
Nyoka anapenda utulivyo kitengo cha kuhama umekosea Sana anaenda kutaduta ndg zake wanahamia hapo
 
Ukubwa wa umbo la mnyama hutathmini uwezo wa sumu kusambaa mwilini.

Mnyama mwenye umbo dogo maana yake moyo utasukuma damu haraka haraka hivyo kurahisisha usambazaji.

Paka atawahi kufa kuliko binadamu.

Lakini binadamu atawahi kufa kuliko tembo.
Mkuu, ebu ingia hata kwenye YouTube uone vile battle la nyoka na paka vile inakua..πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Umeambiwa mwanafunzi aligongwa na huyo nyoka kwenye kiatu.
 
Hujamuelewa mtoa mada, mwanafunzi aling'atwa kwenye kiatu
 
Mkuu, ebu ingia hata kwenye YouTube uone vile battle la nyoka na paka vile inakua..πŸ˜‚πŸ˜‚
Chief paka atamuua kwa urahisi nyoka ambaye hazidi futi 5 ambaye atazidi kila kitu kinakua 50/ 50

Pia nyoka walio chini ya futi 5 wengi ni wasio na sumu so probably hilo battle la nyoka na paka unalolisema ni battle la rat snake au common egg eater ambao wamekutana na balaa la paka.

Lakini venomous snakes wengi huzidi futi 5, koboko hufika mpaka futi 8. Ndiyo maana ni rahisi kwao kusimamia mkia na kuangaliana na binadamu uso kwa uso kabla hajastrike.

Sasa nyoka wa futi 7 na hawa paka wa nyumbani bado unataka utumie reference ya video ya youtube?
 
Dah una roho mbaya sana kwa mfano ukasikia kati ya wale vijana mmoja amefariki kwa kugongwa na nyoka utajisikiaje?
Sasa nilivyokuwa nawaita tena dirisha la nyavu wananisikia lkn wakauchuna Kama vile chizi nisiye na maana wananiona ,je na mm ningegongwa na huyo nyoka na wao wakistarehe ndani wakibishana upuuzi tu ingeleta faida gani kwangu na eneo sio langu


Shauri yao anaye kudharau na ww achana nae nadhani maana ya roho mbaya huijui ..unataka kumpa mtu msaada lkn anakupotezea msaada upi umpe kujisumbua na mdudu hatari wkt sioni faida yake
 
pakaa wanauwa nyoka Sana sio panya tu!
nina paka 3 nina waheshimu kwa zoezi hilo!
 
Amwage mafuta ya taa tu sehemu anazo hisi yupo atakufa yakimpata ama kuondoka atakaposikia harufu tu na hatoseogea tena. Nyoka ukimwagia mafuta ta taa anakufa dakika tano nyingi pia akisikia harufu ya mafuta ya taa anakimbia mno.
 
Aende idara ya wanyama pori atapata msaada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…