Msaada: Nyoka Mkali anazunguka Mazingira ya Nyumbani

Nimejitahidi kusoma uzii huu mpka hapa ninaogopa, yani siku ya leo kwangu haitokua nzuri.
Naomba kuuliza hivi unaondoaje hofu ya nyoka maana inanitesa kupitiliza. Nikiona picha yake usiku lazima nimuote, mara amepanda ukutani mara anatamba yan mradi niteseke usiku.
Naoondoaje hii hofu maana ni zaidi ya 10 yrs nahishi na fear ya nyoka, sikuwahi kugongwa na nyoka ila nikiwa nasoma shule enzi hizo, nilifua begi la shule kumbe lilidondoka sasa nyoka aliingia ndani ya begi, jioni baada ya prepo kufungua begi nieke madaftari nyoka akatoka ndani ya begi, kwanza sikuwahi kujua kua nna uwezo wa kuruka kiasi kile maana niliruka dekani nikarukia kitanda cha tatu bila kujua nliruka vipi
 
Yule nyoka mwenye jicho moja mbona humuogopi? 😂 😂 😂
 
Amesema mwanafunzi kwenye kiatu wewe bwiga
 
Mmoja huyo alipitiliza kwenye homeground na pana kuku, sivyo aliishia kwenda ahera. 😂 😂 😂
Hiyo ndiyo size ya kuku, nyoka wengine size kubwa, kuku hatoboi! 🤣
 
Andika getini "Nyumba hii inalindwa na nyoka mkali"

Sent from my SM-G9250 using JamiiForums mobile app
 
Fuga kuku. Kuku wangu juzi nilimuona anakula nyoka aliyejileta kiwanjani kwangu. Nafikiri watakusaidia sana.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]mkuu hebu tufatie mrejesho kwenye hiyo nyumba!
 
Tufahamishe hii vzr ndugu.
 
Wazee kuna Nyoka wengine ninwakubwa mno..awali dikujua wapo nyoka ninwakubwa kiasi ukimuona kama uko pekeyako unaweza kimbia nyumba. Home miaka ya 2012 alitokea nyoka mmoja alikuwa anakula bata, bata walikuwa 200 waliliwa mpaka wakabaki 30, mwanzo tulihisi ninwatu wanawaiba ila kuna siku sasa akaonekana live yule mjuba. Kwanza alikuwa anaishi katika choo, yaani kile choo kiliterekezwa kilikuwa hakitumiki sana sababu kilijengwa kwa ajili ya mgahawa ( mgahawa ukafunhwa hivyo kile choo kikawa hakitumiwi ) sasa yule kiumbe ndimo alifanya makazi yake humo..

Yule nyoka hakuwa chatu, sababu chatu nawafahamu vizuri sana, na kwa ukubwa pengine hao chatu waunganishwe watatu kwa pamoja kwa upana na urefu. Nasema hivi sababu hiyo siku halikuja usiku mnene lilikuja mapema tu saa mbili usiku likaingia jikoni, kule jikoni kulikuwa na mamayangu mdogo anapika bahat nzuri ule muda anaenda kuangalia chakula ndio akawa anasikia mchakacho sasa, dah limejaa jiko zima! Lina macho makali kinyama, sasa ikabidi tuanze kuita watu maana nyumba ipo pembezoni mwa barabara na kuna stendi muda huo watu walikuwa wengi bado, wakaja na fimbo wengine nondo, wengine mawe, hahahaaa cha ajabu mawe yalikuwa yanadunda lijamaa likacharuka sasa linavimba mle ndani pa kutokea hamna , nje watu kama kijiji, yule m$&!ge unajua alibomoa lile jiko aliamsha timbwili mle ndani si la kitoto, watu wanapiga makelele ndo wanazidi mvuruga.. wenye mishale wakarusha, wa mikuki wakarusha, wa upinde wakafanya hivyo na mwisho kuna mdau akaja na Gobole lakini bado shughuri ilikuwa pevu. Sasa ikawa si jiko tena kuanguka na ukuta ukaangushwa upande mzima yule nyoka hafi anataka kue scape arudi kule chooni, sasa home pakageuka kama vita, ila hakuna anayejaribu kulisogelea, saa mbili mpaka inatimu saa nne usiku yule mwamba bado hajafa, wakaja watu wa mali asili toka Moro town nao wakashiriki sasa limeingia kwenye shimo nusu mwili umebaki nje, choo kikashuka kwa kupigwa mawe, boonge la msala kwa mwenye nyumba.. huku na huku mpaka saa tano ndio lile timbwili linaisha baada ya nusu ya nyumba ya marehemi babu kubomolewa kisa lijoka. Likavutwa mle shimoni mali asili wakalipakia kwenye canter wakaondoka nalo wakalichunguze mbelembele huko...hakika sijawahi ona nyoka kama yule iwe katika documentary ama mtaani. Wengi walihusisha na mambo ya tamaduni. ( Mambo meusi ) na mimi pia niliamini hivyo na tangu iyo diku mpaka leo hii siwezi lala nyumba ile aisee...yawezekana hakuwa nyoka wa kawaida.
 
Nenda maliasili ulizia kuna vijana wanakamata nyoka aina yeyote ile, watu wa maliasili wanawajua.
Mwanzo walikua wanakamata kwa ajili ya wafanyabiashara waliokua wanasafirisha nje, tangu biashara ilipopigwa marufuku hawa vijana wapo tu mitaani sema ujuzi hauzeeki. Unakumbuka yule chatu aliyetoroka kwenye box lake pale mpingo house keko? Vijana wa namna hii ndio waliitwa kumtafuta. Haikuchukua muda wakamleta mzima kabisa
 
Huyo nyoka atakuwa alikuwa na kiu ya maji. Mimi mmoja nilikuwa napishana naye chooni usiku kwa takribani siku mbili bila kujua nikidhani ni mjusi kwa sababu akili yangu haikutegemea kuwa kuna weza kuwa na nyoka ndani. Sema Mungu saidia alikuwa ni mdogo halafu ni hawa jamii ya weusi wanafuata panya ndani. Mara zote nilikuwa nashtukia tu mkia unapoteelea chini ya vitu nikawa najua mjusi lakini akili inakuja inakataa mjusi gani mweusi hivi sasa ukichanganya wenge la usingizi nikawa najipa moyo kuwa atakuwa mjusi tu. Na mara zote nilikuwa napishana naye wakati naingia chooni kujisaidia usiku kabla sijawasha taa yeye anakuwa ameshasikia mapema kuna mtu anakuja kwa hiyo tulikuwa tunapishana kabla sijawasha taa. Siku ya siku nimetoka zangu kwenye mishe mishe usiku nikiwa na chupa ya maji nimenunua mtaani sikuimaliza nikawa nimeiweka pembeni ya kitandani kwangu chini. Sasa kabla sijasinzia vizuri nikawa nasikia sauti isiyo ya kawaida pale chini nilipoweka chupa ya maji kumbe nilikuwa sijaifunga vizuri matone ya maji kidogo yalikuwa yamedondoka pembeni kidogo. Nikiwa na wenge la usingizi nikachungulia kupitia kwenye chandarua nilichokiona ni nyoka anakunywa yale matone ya maji sikushtuka sana kwa sababu nilishaua nje ya nyumba nyoka wakubwa zaidi yake. Nilichofanya nikuchukua ndala ninazotumia ndani wakati wa baridi maana ndio silaha iliyokuwa karibu nikambamiza kweli kweli akafa pale pale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…