Msaada tafadhali, napitia wakati mgumu sana

Msaada tafadhali, napitia wakati mgumu sana

Wazee nakuja kwenu nikiomba ushauri,

Kama kichwa cha habari kinavyosema japo mimi sio mtaalamu sana wa kuandika nitajitahidi kuandika machache na ya muhimu, mwaka 2018 nikiwa kwenye safari zangu za kibiashara nilikutana na mwanamke mmoja tukiwa tumekaa siti moja kwenye bus tulilokua tunasafiria pamoja!!

Tulipofika kwenye kizuizi sehemu flan gari ikasimamishwa kwa ukaguzi, kumbe yule mwanamke alikua na mzigo wa magamu(magendo) na akatelemshwa hapo beria.

By then tulikua tushapeana namba za simu na nikataka kujua kulikoni ndipo aliponisimulia mkasa wake na akaniomba nifikishe taarifa kwa ndugu ambaye alinipa namba yake na maelekezo yote!!!

Hata nilipomtafuta yule bwana hakua tayari kuonyesha ushirikiano na yule mdada akawa Hana namna ila kuomba msaada wangu Kama naweza kumsaidia, baada ya michakato yote kufanyika ikawa inahitajika laki 5 ambayo alikua amepungukiwa ili amalize tatizo lake.

Mimi nkaamua kumsaidia kiroho Safi na akatoka ndani , mwanzonii mwa 2020 nkapata kesi ya uhujumu uchumi iliyoniweka gerezani mwaka mmoja na miezi Saba, yule dada nlimpa taarifa siku nakamatwa(alishakua rafiki yangu lakini sio kimapenzi) katika mwanzo wa kesi yangu Hadi natoka gerezani nlikua nae bega kwa bega na hakuna siku hata moja alikosa Kuja kunisalimia nkiwa gerezani (NB gerezani wanasalimiwa siku za wikend tu)

Mungu akasaidia kesi ikaisha na nkatoka, yule dada akanikaribisha nyumbani kwake na katika muda huo wote nlikua sijawahi kufika nyumbani kwake!! Nkakuta anaishi mwenyewe na akaniambia Ana miaka 2 hayuko kwenye mahusiano na pale anapoishi Ni nyumbani
kwake hajapanga

Basi nkatumia nafasi Ile kumuomba awe mwenzangu na akakubali !! Tumekaa kwa upendo na furaha nkiwa naenda kwake kila napohitaji hata Kama Ni usiku wa manane namkuta Yuko peke yake!!

Lakini alishaniambia huko nyuma alikua kwenye mahusiano na mtu japo waliachana sababu ya changamoto za maisha ya hapa na pale Basi kidume nkashika usukani

Yule X wake anasema waliishi pamoja miaka 10 lakini hawakua kwenye ndoa , waliishikimada tu, na walikua wameachana miaka imepita 2 Sasa Hadi mm nakutana nae kimapenzi

Siku moja yule X akapiga simu , akamwambia nasikia una mwanaume hapo nyumbani, Sasa Leo nakunywa KVANT nakuja kukufanyia fujo hapo kwako!! Nkamwambia yule mwanamke huyu X wako Kuna kitu anakudai hapa au alikusaidia kujenga hii nyumba?? akaniambia hajawahi hata kuninunulia glass hapa ndani, vitu vyote Ni jasho langu, Basi nkamwambia Kama Ni hivyo hawezi Kuja Ni mikwara tu!!

Ilipofika saa 5 usiku yule bwana akaja, kumbe alimaanisha, akafanya fujo anapiga madirisha na milango ikawa fujo kubwa wakati huo sisi tuko ndani tumefunga mlango

Asubuhi nkamtaka akaripot police akasema hawezi kumuweka ndani maana Kuna mazuri alimfamyia wakiwa pamoja Ila atamuonya asirudie! Jioni yake akanipigia simu akaniambia nimepata ushauri kwa watu wazima wamesema hapa kwangu nisilete mwanaume, kwa hiyo kuanzia leo usije hapa labda Kama Ni kukutana tukutane juu kwa juu!!

Nkasema sawa sitakuja Wala usiwe na Shaka kuhusu Hilo!!! Nkamuuliza au ndo unamrudisha x wako akasema yule siwezi kurudiana nae maana aliyonifanyia Ni makubwa!! Ntakua na wewe tu Ila nyumbani ndio usije maana namuogopa akisikia Tena uko hapa atakuja kunifamyia kitendo kibaya maana namfahamu Ni mkorofi.

Basi mm nkaamua kukaa kimya Ila Mara kwa mara akawa ananichokonoa kwa msg na simu akitaka tuonane, na mm nkajaa maana niwe mkweli nlijikuta nampenda Sana huyu mwanamke!! Juzi nkampigia simu hakupokea na sio kawaida yake , meseji hajibu nkasema huyu labda atakua na mwanaume ndani !

Nkaenda kwake kufika dirishani nkakuta anaongea na Yule x wake kwa simu ananisengenya na kuniongelea vibaya!! Nkamwambia fungua mlango na kweli akafungua tukiwa ndani nkamuhoji Kama anataka kuendelea na mm au anarudi kwa x wake akasema ananitaka Mimi!!

Basi ukatokea ugomvi Kati yangu na yeye na asubuhi akaita watu wazima tukasuluhisha , jioni hii Nimempigia simu kapokea yule x wake Ila kaongea kistaraabu tukamaliza , baadae nlipopiga Tena akapokea mwanamke akasema bwana yangu ameenda kazini ,namsubiria aje tulale Mimi nlikua na wewe sababu ya shida tu!

Nikihesabu garama na muda ambao nimeuwekeza kwake afu Leo anakuja kunilipa jeuri nakosa Raha kabisa hapa najiuliza nimfamye Nini huyu mwanamke?? Na nitoke vipi kwenye hii Hali niliyonayo maana roho Inaumia Sana , nahisi nlikutana nae naweza kufanya tukio baya maana amenifanyia usaliti mkubwa Sana.

Nawasilisha wakuu naombeni ushauri wenu
Something is wrong here!
Yaani kabisa mwanaume unakuja kutulalamikia kwa issue ya wanawake?

Eti umelipa 500,000 yaani umeishi na amekufanyia yoote hayo ukiwa Gerezani halafu unaolala!

Fanya hivi sisi wanaume, hata tukioa wanawake wawili wawili hatuwezi kumaliza idadi ya yao.

Mbona wanawake wamejaa tele aisee, tafuta pesa kisha opoa mwanamke mwingine...

Kingine usithubutu kwenda kulala kwenye nyumba ya mwanamke hata siku moja, wana maneno matamu sana hao waone hivyo hivyo na ni wasiri mno na mikono yao ni mifupi
 
Wakati nimemtembelea kwake nkataka kujua why anaishi mwenyewe?!! Ndo akasema nlikua na mtu Ila tumeachana miaka 2 Sasa Niko peke yangu

Ulifata nini nyumbani kwa mwanamke?
 
Umepima magonjwa ya zinaa? Mshukuru Mungu wako kisha endelea na maisha yako
 
Sawa mkuu ntazingatia , eti kwa ubwege wmg toka Jana Niko nakunywa ! Sijala Wala Nini huu so ujuha huu!! Ila sababu nafahamu Hali ya kiuchumi ya yule mwanamke na huyo X wake , acha nipige kazi hela ikae vizuri kwenye account afu siku moja ntakuja kuleta mrejesho humu
wewe piga kazi siku akija kukuomba hela hakikisha una mla kwa hasira akiomba hela lazima akitoe halafu endelea na maisha mengine tena siku hiyo unapiga show ya uhakika
 
Usiwe na shida maana ulisema K ni yako na unaikosha na kuipaka mafuta wewe! Ila kumbuka mahondaw alipoanzana na Smart911 naye nilitoa angalizo lakini wakanitukana ingawa hawakuwa wanoko kama Nakadori alivyo ninyea! Ona sasa maskini jamaa hata comments zake ni ….. watakuja kukupa ushauri…. Wakati kabla hajaanzana na mahondaw alikuwa akitema Madini

Hahahah....dah!!!
 
Ila huyo Mwanamke naamini ipo siku atarudi tu, hawa Viumbe hawa mh!!!
Ni sahihi wengi wameniambia hivyo , nataka akirudi niwe nimeshamtoa moyoni!! Ibaki nimuumize na mm moyo au nimpige chini tu! Sitakia arudi nkiwa bado nampenda naomba Sana hilo
 
Ni sahihi wengi wameniambia hivyo , nataka akirudi niwe nimeshamtoa moyoni!! Ibaki nimuumize na mm moyo au nimpige chini tu! Sitakia arudi nkiwa bado nampenda naomba Sana hilo
Pole sana Mkuu kaza Moyo Mtoto wa kiume songa mbele
 
Ushauri kuntu tatizo Sasa hivi ananiogopa maana nlimtia kerubu mbili tatu usiku ule na nkampigia mkwara wa kufa mtu, taarifa nilizonazo ameripoti polisi si kwa nia ya kunikamata au kunishtaki hapana anataka niogope sababu Ana RB yangu!! Yaani haya mambo Ni shida kwangu Ila ushauri wako hata mm ndio hua zangu kwa muda huu acha nikifanye fala kwanza ili nimesahau na kumtoa moyoni
Achana nae kwa sasa mkuu, wanawake hawapendi kunyenyekewa na mwanaume hata kidogo(sio kubembeleza ila kunyeyekea!!)

Ko kausha kwa sasa.
 
Achana nae kwa sasa mkuu, wanawake hawapendi kunyenyekewa na mwanaume hata kidogo(sio kubembeleza ila kunyeyekea!!)

Ko kausha kwa sasa.
Ndicho nlichofanya Ila akijichanganya arejeshe uhusiano ntatumia mbinu z deppond ntalipa kisasi kibaya Sana Cha mapenzi
 
Mkuu ulipaswa kuota mbawa au kutafuta chimbo jipya pale ulipomkuta akikunkanyagia kwa X wake maana penzi lilisha rudi hukupaswa kuuliza eti unamtaka nan
 
Mkuu ulipaswa kuota mbawa au kutafuta chimbo jipya pale ulipomkuta akikunkanyagia kwa X wake maana penzi lilisha rudi hukupaswa kuuliza eti unamtaka nan
Hapo nlikua nshachelewa sikua na ujanja wa kuota mbaya si ndo maana nkakimbilia humu kwa waungwana kupata faraja!! Kipindi Cha nyuma ndo ningeota mbawa Ila nkafanya mistake nkarudi baada ya kua amesema tuachane
 
UPDATE!!!! kwa ushauri mlionipa humu wajuzi wa mambo , kinachoendelea saa hii Ni habari nyingine
 
Seems you are my bro ila ndugu afya yako, maisha yako ni muhimu sana , for the sake of your healthy please achana na huyo endelea na maisha yako japo ni ngumu si suala la mara moja , jichanganye mda mwingi na marafiki wazuri kama unao, chagua kitu unakipenda sana , kifanye hata mara mbili au zaidi kwa siku , change your mobile number, then pray for your God most of the time , hakika utanikumbuka .

Evening.
 
Back
Top Bottom