Kushukuru ni kuomba tena.
Hebu jaribu hivi:
1. Akirudi kutoka shuleni uwe unakagua madaftari yake kuona ni katika masomo gani ndo kuna changamoto kubwa. e.g. Hesabu au Jiografia Haya ni kati ya masomo yanayowachanganya watoto.
2. Mwelekeze kwa kuzingatia alivyoelekezwa na Mwl. wake i.e. unakazia maarifa.
Halafu umtake afanye masahihisho then mpe kazi /homework ya aina hiyo hiyo na akimaliza sahihisha mkiwa pamoja.
3. Akifanya vizuri umpongeze au mpe zawadi yoyote. Akikosea usimgombeze hata kidogo bali mwelekeze tena kwa maneno ya kirafiki e.g. unaanza hv: Mmm; wee fulani mbona hapa umefanya vizuri halafu hichi kiswali kidogo namna hii kinakushinda? Hebu tufanye tena mm na ww.(
mnafanya).........Umeona? umeelewa? Hebu sasa nenda tena karudie kwa uangalifu kufanya haya yafuatayo e.g. 5qns. zinatosha.
4. Jitahidi sana sana
TV isiwe on; kusiwe na mazungumzo ya aina yoyote wakati akifanya H/W zake e.g. kuongea na simu au kuagiza kwa sauti kubwa jambo fulani lifanyike huko nje, kucheka-cheka hovyo n.k..Hayo yana
-disrupt sana
attention yake na kuhafifisha
concentration ya kile anachofanya
NB: Na mimi nimekuwa na changamoto hiyo hadi sasa,nilijitahidi hata kuweka mwl. wa kumfundisha hapa nyumbani, kumpeleka Tuition lakini wapi - Ngoma ikagoma. Lakini nilishangaa na kufurahi sana hapo juzi kati (Feb 2025) nilipozingatia na.2 na 4; sasa anaweza kufanya hesabu(Maths) kuzidisha na kugawanya kwa njia ndefu, anazijua kwa kichwa orodha(Tables) 2-13; anajua kutumia dira (Cardinal compass rose) kueleza uelekeo wa kitu fulani kilipo (Cardinal na Ordinal compass directions).
Huyu wa kwangu yupo darasa la Nne(4) na ni
Ke. Zawadi ninazompaga ni e.g. Namsifia-sifia na kumpongeza; namwahidi kesho tutaongozana kanisani au nampa pipi kijiti au namwacha akacheze na wenzake huko nje uani au namwuliza anapenda zawadi gani n.k. Tena huwa nafuatilia sana huko shuleni marafiki zake ni akina nani? Ninakuwa karibu sana na Waalimu wake esp. mwl. wa darasa.