Chrysanthemum
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 1,531
- 5,787
Ni jambo la kawaida pia mchunguze kwa umakini huenda pia ana changamoto ya Learning Disability ( natamani kuelezea hapa ila sio mwandishi mzuri ) hivyo anapofundishwa anahitaji kutiwa moyo ! na kuelekezwa mara nyingi kadri iwezekanavyo na akichoka asilazimishwe mpe muda kumaliza task yake
Kuna malengo hatayafikia vizuri kama unavyotaka mzazi ila usikate tamaa mwangalie vizuri kuna mambo anayoyaweza mpaka unafurahi hivyo muelekeze zaidi kwenye hayo anayoyawaweza maisha sio kusoma tu,
Nina mtoto wa dada yangu ana Learning Disability upande wa Dyslexia walikua wanamchapa sana basi wakati fulani nikamuomba niishi nae nikamnunulia supplements za omega 3 na chakula chake tukawa tunamwekea mafuta ya samaki, kwa kweli ilimsaidia sana na shule nikaongea na walimu nikawaeleza hali halisi ya mtoto !
Kwa hiyo task ambazo watoto wenzie watamaliza baada ya nusu sasa yeye ingemchukua hata masaa matatu ! Muda wenzie wakienda nyumbani anabaki mdogo mdogo na mwalimu mpaka kazi anamaliza ndo anakuja nyumbani !!
Watoto wa hivi wanakua vizuri sana kwenye sphere nyingine , ila upande wa cognitive anakua na changamoto , huyu mwanangu kwa sasa anaendelea vizuri siwezi kumlinganisha na watoto wengine kwa mambo ya darasani ila naona naweza kumuendeleza katika vitu vingine vingi tu.
Zingatia chakula , weka mahusiano mazuri na mtoto , usione aibu kueleza changamoto yake ili iwe rahisi kusaidiwa waeleze walimu , hata watu wako wa karibu ili kuondoa kumfedhehesha bila kujua katika utani na maneno.
Pia usimuendekeze , mpelekeni taratibu kwenye mambo mnayoona kweli anapata ugumu , ila mengine nendeni mchaka mchaka kama watoto wengine hasa upande wa tabia na kujituma na nidhamu!!