- Thread starter
- #21
Hata hivyo mna moyo sana. Usawa huu wa magu mnatoa 9m kirahisi rahisi kwa jina la uwekezaji? Mlishafika kufhakiki mashamba kabla hamjawekeza? Naiona QNET nyingine hapa, kupitia ninyi
Wengi wetu tulikuwa tayari na mashamba na mitaji lakini hatukuwa na utaalamu pamoja na masoko. Tulipoenda kuomba huduma ya consultancy ndio tukapewa huo mradi tukaona labda utafaa na masharti yao lazima walime wao ili kudhibiti ubora.
Tulienda hadi shambani Mkuranga kijiji cha Kimazichana na tulikuta matrekta na excavators ziko site zinangóa visiki pamoja na vibarua wengi tu.
Mara ya mwisho kwenye kikao na Mkurugenzi Grace Mzoo tuliambia kuwa anasafiri ili kwenda kutafuta pesa ya kuturudishia lakini tulivyofuatilia huyu mama yupo Dar na anaonekana Kanisani Anglican Church Ukonga. Ndio tukaona hapa tunaibiwa. Tukipiga simu hazipokelewi, Ofisini wameweka namba za simu zilezile
Asante