Msaada tunaomba Mhe. Paul Makonda atusaidie, Kampuni ya Jog imechukua fedha za wawekezaji

Nilikwenda ofisini kwao wakaniambia wanaandaa semina nilipie 6000 nikapiga hesabu mara 500 nikakuta wanaingiza 3000000 nikajua hawa ni matapeli
 
share economy inatumika duniani kote na watu wanapata hela.

usihukumu mfumo mzima kwa incident chache km hii alioleta mleta mada
Vipi hii ya Mr. Kuku?
 
Mwaka jana wakati tumekuja tz, tulienda ziara mkoa fulani nilikuja na Waarabu kutoka UAE. Huo mkoa tuliofikia kwa mdogo wetu ambae ni mkulima, tukakutana na Company kama hiyo ambayo kama sikosei Inaitwa Macleans Benecibo. Hivi kuna mtu yeyote anaweza kunihabarisha kuhusu ile company??
 
Tumejaribu kufanya hivyo Pwani (Mkuranga) wakatuambia tuje Dar manake Kampuni ipo huku na wakurugenzi wanaishi huku. Dar nako wanasema ni kama hawaoni jinai.

Thanks
Hawaoni jinai?? Ni chombo kipi kinatafsiri sheria????
 
Mkuu umemaliza haha haa....
 
Uko sahihi kabisa kaka/dada... Natumaini mamlaka husika watafatilia hili, usichoke kupaza sauti kwa manufaa ya wengine. Be blessed!!
 
Yale yale ya Mr Kuku... yaani wewe ulipe hela watu wakulimie mapapai na wakuuzie kisha wakupe faida

Mkuu watu wanachekesha sana, sijui ni uvivu eti walipe pesa wao wafuge au walime kwa niaba yao na kampuni ya kilimo iko posta kweli maajabu hayaishi duniani
 
Mtapigwa sana na upumbavu wenu. Huwa tunawaambia hamsikii.

Kuna wengine wanalipa milioni tatu na laki mbili kwenye mradi wa sungura. Narudia 3.2M na unapewa sungura 20 ukafuge.

Hivi kweli mtu mzima na akili yako unauziwa sungura mmoja laki na nusu, amekuwa mbuzi huyo?
 
Asante mkuu
 
Asante mkuu
Wengi watakuvunja moyo...... Kudhulumiwa, kupata hasara kupo kwenye biashara.. Kikubwa ni kuminimize your loss...... Kuangalia investment ambayo ipo not too risk to put your money........ Yupo mtu atakutukana ila kila weekend bar anatumia laki 1 piga mara miaka 30 ya ulevi wake........ Jifunze kulingana na makosa.
Soma, tafiti fursa yeyote ile kabla ya kuingia, usifanye biashara ambayo huna uhakika nayo 100%.
Wekeza kiasi ambacho hata kikipotea hutafirisika.
Duniani tunazidi Kujifunza........ Wapo waliowekeza kihalali na miradi yao zaidi ya milioni 100 na zote zikapotea wakaanze tena upya.
Nakutakia uvumilivu na subira kwenye kipindi hiki kigumu

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Nashukuru mkuu
 
Daaah watu wanapigwa kizembe sana,mimi pesa zangu utazisubiria ahera
 
Huyo mama ningemchukua na kumalizana nae kimenomeno bila police na pesa angerudisha na riba,mnapigwa na wajinga kwa kuchotwa akili ya faida kubwa
 
Asante sana.

Kumkamata mtu pia inahitaji msaada ukiona mpaka tumekuja hapa jamvini mambo yamesuasua mahali fulani ndugu yangu.

Nashukuru kwa ushauri wako
Huyo mama ningempa kesi ya mbaya mpka astuke marinda yote yameisha
 
Hivi Bashite mnamuamini vipi nyie. Bashite hana uwezo wa kutafuta suluhu yenu. Nendeni mahakamani.
 
Wajinga ndio waliwao
Milioni 9 yako umeshinda kuingiza shambani kwako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…