Okopa sana mtu anayepost mistari ya biblia kila mahali
Mhurumie sana mtu anayeogopa, anayepata wasiwasi au kupoteza amani na kuhuzunika anapoona mistari ya biblia ikipostiwa kila mahala sababu sio yeye anayeogopa bali ni ile roho iliyo ndani yake isiyotaka kusoma wala kuusikia utukufu wa Mungu aliye hai
Basi niseme tuu Mungu akakufungue ufahamu ukalione neno la Mungu kama taa inayofungua akili yako. Akupe hekima ya kumpa Mungu utukufu badala ya kumpa shetani utukufu kwa kumuona yeye "shetani na nguvu zake" pale unapkutana na neno lake limepostiwa
Kwa kuwa najua sio wewe usiyetaka kuona mistari ya biblia inapostiwa na kwa kuwa roho iliyo ndani yako inakufanya kuona na kuwaza kila anayepost mstari wa biblia ni kuogopwa wacha nikupe na bonus😂
Wakolosai 3:16-17
Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.
Zaburi 119:105 Msikilize pia Mfalme Daudi anamwambia Mungu
Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.
2 Timotheo 3:16-17
Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.
Usiwaogope tena wanaopost mistari ya biblia, usikasirike wala usiwe na shaka. Hakuna aliye safi sote tumepungukiwa ila tunakumbushana kukulia neno kwa sifa na utukufu wa Mungu.
Vinginevyo useme unatamani kuskia mistari gani🤣🤣🤣