Msaada wa AirBags wakati wa Ajali

Sio salama kivile
kabisa sio salama kivile. Sema mimi naona.ni ile kutengeneza bond kati ya boss na suka ili kumsaidia kwenye mambo madogo madogo mfano kumtuma dukani , kumtafutia boss mchuchu (bebez), n.K . Labda ndio inafanya boss kukaa mbele ili dereva amrahisishie mambo yake personal. maana akikaa nyuma anaona mambo yake personal yatakuwa hayaendi kwa haraka kama anavyotaka. Mwisho wa siku lilitokea la kutokea ndio kama hivyo R.I.P.
 
Sensa ya airbag ipo kwenye seatbelt. Ikiwa
sensa imeharibika,
haujafunga mkanda,
sensa haijapata msukumo wa kutosha wa kuhisi hatari
haiwezi kufumua airbag.

Jambo la kwanza hakikisha umefunga mkanda
Au Mkuu alikuwa ana drive Toyota Corolla G touring 16 valve effi ya mwaka 1993 ?😂

(Natania)
 
Ndugu zetu wa European Cars wanasemaje?
hasa BMW little crush linafumua airbag
European cars (benz,bmw) haya madude yana side airbags. Ni wazi yapo salama zaidi. Kuna siku nilikitana na tangazo la gari fulani ya benz ya miaka ya 1970 na wamelisifu kwa usalama wanakwambia hata ligongwe na gari ndogo upande wa ubavuni bado abiria hatokufa kwa sababu mlango wao ni mzito sana
 
Kumbe yalikukuta? Pole mkuu.

Usiwaponde sana wajapani, Fuga inazo airbag kwenye viti.



Crown yako ni highest trim? Executive sedan crown ikose airbag kweny viti even at highest trim?
 
Maintenance haiendi monthly. Kwa gari zote japanese au mzungu

Kuna miezi unatumia 0 TZS na kuna siku isiyo na jina utaletewa invoice ya 2M TZS
 
Hapa sasa umenena ukweli, kwamba sisi watumiaji wa hizi Toyota lower class tutembee na magodoro tu ndani ya gari
 
Maintenance haiendi monthly. Kwa gari zote japanese au mzungu

Kuna miezi unatumia 0 TZS na kuna siku isiyo na jina utaletewa invoice ya 2M TZS
Namaanisha mie kwenye hesabu zangu ntaweka provision ya 300K monthly ili invoice ikija isinipe surprise au hata kama ni surprise isiwe surprise ya kunipa wenge
 
Sasa mtu una akili timamu unanunua gari la 4.5m halafu unataka ikigongana upone? Yaani zipo gari hapa bongo ikigongana na POPO au KUNGURU jike mwenye upwiru anaetafuta dume nakuhakikishia kupona kwako labda ajali itokee karibu na geti la Mloganzila.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…