Msaada wa chakula toka USA ni kuichafua Tanzania

Hatuna Ukame, hatuna Vita wala sisi sio Wakimbizi.

Watufungulie miradi ya Irrigation Schemes tulime sisi wenyewe Mahindi ni Miezi minne tu tunavuna.

Unahisi tunapungukiwa nini? Akili yetu inafikiria luxuries kwa watawala tu, magari ya 600m tutapataje tukinunulia maskini chakula? Ndege je? Tunataka ndege mpya za viongozi, wanaodumaa wanajitakia wasubiri tu Biden aguswe
 

Utapiamlo ni shida kubwa ya nchi wala sio Dom, tuna chronic malnutrition ndio maana tunafanana wote tu! Awe profesa au mtawala hana tofauti na mzee wangu kule mbwilike ambaye hajui hata kusoma hela. Hatuna kitu tunafanya vizuri iwe michezo across all fields hadi uchungaji na ulokole wetu ni tofauti sana na dunia
 
Ni kweli tuna njaa!
Ila walaumu hawa watu...
 
Kuukataa msaada toka Marekani ni kosa la Jinai. Adhabu yake ni kupandikiziwa matatizo mpaka muingie katika vita.
 
Hakuna heri chini ya uongozi wa mwanamke hata wangereta hela zingeishia ikulu kununua shanga za kiunoni za dhahabu na almas na kununua vyupi vya halili kutoka dubai
 
Upumbavu mtupu, yaani serikali imeshindwa kwenda mbeya hapo na kuwanunulia chakula hao watu wa Dodoma?.

Serikali imeshindwa kuwekeza kwenye kilimo maeneo yenye rutuba na kuwawekea stock hao wanaoishi kwenye ukame hapo katikati ya Tanzania?

Serikali imeshindwa kuwekeza kwenye mazao yanayohimili ukame pamoja na kuwafundisha hao watu wa Dodoma nk namna ya kulima kwenye ukame?

Serikali imeshindwa kujenga storage water facility kubwa hapo Dodoma na Singida na kuzijaza maji mwaka nzima na watu wakafanya irrigations.
Yaani hatuna watu wakufanya assessment na kujua litter ngapi za maji zitahitajika Kwa hao raia mwaka mzima Kwa ajili ya irrigation na kuchimba storage ya kuhifadhi hayo maji?
Unahitaji nini kuchimba hizo storage kama sio mabulldozer, excavators nk ambavyo vipo tu available humuhumu.
Yaani maji yote yanayomwagika milima ya uruguru tumeshindwa kuyachanell yaende Dodoma na Singida kwa ajili ya Kilimo?
Ulaya zimechimbwa water channels kibao na kupitisha meli miaka kadhaa huko nyuma Leo sisi 2023 hatuwezi kuwapelekea maji Dodoma na Singida kutokea morogoro na Mwanza.
 
Umesahau na Gereza kuu la kunyongea wafungwa lipo huko.
 
Ukitaka kujua kuna utapia mlo makubwa hapa bongo angalia timu yetu ya taifa ya mpira wa miguu.
Kwa mtoto atakayekula virutubisho vyote inavyopaswa, basi anakuja kuwa lijitu lenye nguvu lirefuu. Sasa cheki timu yetu vijitu vilivyodumaaa hii yote instokana na kutokupata mlo wenye virutubisho walipokuwa wadogo.

In short ni kwamba ugali ni moja ya chakulaa chenye virutubisho vichacheee sana, alafu ndo unaliwaa kwaa wingii sana bongo
 
SIsi pesa zetu ni za kununulia V8 na kulipana posho
 
Ingekuwa inawezekana, misaada yote na mikopo tungekuwa tunaletewa au kitengenezewa vitu, na siyo kupewa pesa. Kama tunakopa pesa kwaajili pesa kwaajili ya barabara, inatafutwa kampuni ya kimataifa inayoaminika, inasaini mkataba, halafu inalipwa moja kwa moja na taasisi iliyotoa mkopo, bila ya pesa kuingia mfuko mkuu wa Serikali. Ingekuwa inafanyika hivyo, barabara zetu zingekuwa na ubora wa hali ya juu, wala zisingekuwa hovyo kama hizi zinazojengwa na makampuni ya mchongo ya China, na wala tusingekuwa na njia za umeme ambazo nguzo zinadodondoshwa hata na upepo.
 
Hatuna Ukame, hatuna Vita wala sisi sio Wakimbizi.

Watufungulie miradi ya Irrigation Schemes tulime sisi wenyewe Mahindi ni Miezi minne tu tunavuna.
Hawa watawala walisha jua wanatawala watu wajinga na wanacho kifanya kwa ssa aanajilimbikizia pesa za wajukuu wao kuja kutumia.
 
maoni na mtazamo wako sio mabayaπŸ’

yalikuako, yalijadiwa, yakachakatwa, yakachambuliwa, yakatatmininiwa kitaalamu na kwa umakini mkubwa sana na wawakilishi katika jambo hili, na kujiridhisha kua mpango au mradi huu ni mzuri una manufaa, hauna madhara wala athari zozote kiafya, bali unafaida nyingi sana kwa mustakabali wa afya za watoto wetu waliokua wameathirika pakubwa na utapia mlo kutokana na lishe duni hususan katika eneo husika πŸ’

Bilasha maeneo mengine yatafikiwa hapo baadae...

mradi unakwenda vizuri tangu kuanza kwake, mafanikio na matokea chanya yameanza kuoneka kwa wahusika πŸ’

masuala ya lishe bora ni nin, sijua vyakula vya viwandani sijui vina nini, yalishajadiliwa mno πŸ’

by the way ukijitathimini wewe mwenyewe apo, tangu umeamka kupiga mswaki, kuoga na sabuni, kujipaka mafuta na pafyumu, kunywa chai ya rangi au maziwa na mkate mpaka hapo tu vitu vya viwandani vingapi umetumia πŸ’

Fear of unknown ni utumwa na ni adhabu nzito sana kisaikolijia πŸ’

Kwa Neema Na Baraka za Mungu Tutafika salama πŸ’
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…