Na hizo mali ulishamwonyesha zote?
Niliachana na mke wangu miradi yangu mingi nikaiweka chini ya kampuni "Sole" ambayo niliifungua kabla sijamuoa, tukaishi nae miaka sita vitu vingi naviweka chini ya kampuni alipokuja kudai talaka akaambulia nyumba moja na vitu vyote vilivyokuwa chini ya Kampuni vikapona imiwemo biashara ambazo alizikuta, nyumba na maghala na mtaji. Na mali kibao nilizificha kwa ndugu alikuwa hazijui ila nyumba niliyomjengea "ya kishikaji" niliona nimwachie akae na watoto wake yaani ni ya watoto. Vitu vya ndani vyote alichukua na gari moja ikauzwa na biashara moja niliyomfungulia ikapigwa panga mtaji tukagawana, shamba moja nilinunua alime na kufuga likauzwa, ila niliokoa zaidi ya 80% ya mali zangu na mtaji ambazo nilikuwa nimezificha kupitia kampuni na ndugu hasa mshua.
Ishi na mwanamke uliemuoa kwa ndoa kwa akili, usijisahau ukafikiri hakuna kesho. Wenzetu wakienda Mahakamani basi wanapewa uzito sana na sheria zetu, ningeshakuwa masikini maana ilikuwa pasu kwa pasu, 50:50 kila kitu.
Usiombe mke wa ndoa akupeleke mahakamani na talaka iamuliwe unafilisika dakika chache tuu na mali zako wanaenda kula watakao mgegeda baada ya yako.