Msaada wa kisheria kuwapata watoto baada ya kuhitilafiana na baba yao

wanaume tuna taranta ya saikolojia...

mumeo ameshajua ukipata kazi na pesa utamsumbua...

baadhi ya wanawake mna ulimbukeni mkipata hivyo vitu viwili...

nakushauri achana na huyo mwanaume...

japo hakikisha mnakaa kikao ili upate haki ya access kwa watoto wenu...
 
 
Fata utaratibu Kafungue kesi ya talaka mahakama ya mwanzo au wilaya na ueleze sababu za msingi za kudai talaka ni zipi, labda ukatili, kutelekezwa, uzinzi, kutokuelewana kwa muda mrefu au sababu zingine.

Baada ya hapo mahakama itajaribu usuluhishi kupitia baraza la usuluhishi, ikiwa suluhu haitapatikana mahakama itasikiliza ushahidi wa ulichoshtaki na baadae itatoa hati ya talaka.

Masuala la mgawanyo wa mali au nani atabaki kulea watoto mahakama itaamua pia.

Ila hapa umeeleza malalamiko yako ya upande mmoja na siku zote anaesema peke yake ni mshindi, ikiwa na yeye anayo malalamiko yake ya msingi unaweza kunyimwa hao watoto na mahakama pia akaachiwa yeye kwa manufaa mapana ya mtoto.
 
Mimi kuacha kazi ni haiwezekani kutokana na mazingira niliyoishi na pia mimi binafsi ninayo malengo yangu isitoshe nina wazazi wanaonitegemea.
Pole dada yangu, ila tatizo lilianzia hapa, uliingia kwenye ndoa tayari ukiwa na msimamo wako kichwani na yeye akiwa na msimamo wake.
Inawezekana ulikubali kuwa utakuwa mama wa nyumbani ili kumridhisha jamaa na hatimaye mfunge ndoa, matokeo yake mmeingia kwenye ndoa na wewe ukaamua kuonyesha msimamo wako mpya.
Cha msingi mjulishe muajiri wako hayo unayopitia, then rudi dawati la jinsia na ikiwezekana fungua kesi.
NB: Msiingie kwenye ndoa kutokana na shinikizo la kijamii au rika, ukijua una misimamo yako iweke wazi mapema ili mkiamua kuingia huko kwenye ndoa msikumbane na mambo mapya sana. BTW kataa Ndoa.
 
Rudi nyumbani ulee familia!
 
Je naweza kumueleza mkuu wangu wa kazi juu ya changamoto ninayopitia ili pia niweze kupata ruhusa wakati nitakapohitaji kufuatilia watoto?
- Maisha yako binafsi na changomoto unazopitia hupaswi kuzipeleka sehemu yakazi.
Je nini cha kufanya:
  • Fuata miongozo na taratibu za kupata ruhusu, zipo.
  • Andika barua ya kuomba ruhus (itakapo fika wakati), Ainisha muda wa ruhusa, kwenye sababu waweza andika "Matatizo ya kifamilia".
  • Wakuu wako watapokea barua,wataipitisha na utapewa release.
anakujibu vibaya nanukuu “ watoto sio wangu watafutie baba yao”
  • Tuseme ukweli: Hii kauli haiji kwa bahati mbaya, Kuna kila dalili ameona wazi kuwa watoto huenda si wake, kilichobakia yeye ni kuthibitisha kupitia DNA
  • Nadhani hapa kuna red flag kadhaa aliona toka kwako. sio bure, Narudia tena hii kauli huwa haiji kwa bahati Mbaya.
 
Hivi mwanamke akiwa anajitafutia hata vi buku buku huwa ni jambo linalomkera sana mwanaume? Wanaume huwa wanainjoi kuona mtu unakua omba omba kwake mara akunyime....inaleta good feelings bila shaka 🤔

Pole kwa changamoto.
Shida nyie viumbe hamjawahi kujua kudhibiti kiburi mpatapo kauwezo kidogo, tumesikia story ya upande mmoja tu, tungepata na ya upande wa pili we could judge better
 
Hivi mwanamke akiwa anajitafutia hata vi buku buku huwa ni jambo linalomkera sana mwanaume? Wanaume huwa wanainjoi kuona mtu unakua omba omba kwake mara akunyime....inaleta good feelings bila shaka 🤔

Pole kwa changamoto.
Shida nyie viumbe hamjawahi kujua kudhibiti kiburi mpatapo kauwezo kidogo, tumesikia story ya upande mmoja tu, tungepata na ya upande wa pili we could judge better
Comment moja matata sana
 
Kwanza mshirikishe boss wako kisha nenda ustawi wa jamii.Otherwise mtafute advocate akusaidie.Usiache kazi
 
Yeye hajagusia mambo ya talqka.Kaongelea watoto ndo shida yake
 
Hivi mwanamke akiwa anajitafutia hata vi buku buku huwa ni jambo linalomkera sana mwanaume? Wanaume huwa wanainjoi kuona mtu unakua omba omba kwake mara akunyime....inaleta good feelings bila shaka 🤔

Pole kwa changamoto.
Halimkeri alichoniangusha mwanaume mwenzangu ni hataki mkewe afanye kazi huku kutoa matumizi na kumpendezesha mkewe hataki.

Kama hutaki mkeo aajiriwe na ana passion ya biashara mpe mtaji afanye biashara huyu jamaa ni mpumbavu sana
 

Kama inawezekana kama usiache Mwanaume akulelee watoto, wataenda kuteseka huko, hasa wa kike. Ni wanaume wachache wanaweza kusimamia maslahi ya watoto wao wakiwa na wanawake wengine au wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…