karibu kilindoni, ni kweli wapo vijana wanapenda starehe lakini hawana shughuli za kuwaingizia hela za kuja kutumia kwenye lounge yako. Shughuli zao ni bodaboda na uvuvi wa samaki kwa zana duni sana.
Hela iko kwa wazee kwa sababu wanamiliki mashamba ya nazi.
Garama utakazotumia kwenye lounge yako obvious bidhaa zako utauza bei juu tofauti na bar za kawaida. Watakaomudu labda wazungu na watumishi wachache wa halmashauri. Garama za usafirishaji kutoka dar kuja mafia zinasababisha kila kitu kuwa bei juu. Mafano azam cola dar wanauziwa 500 huku ni 800, Maji kubwa yote 1000, soda zote 1000
Mara nyingine wazee wakicharuka bar zinafungwa saa sita usiku, huruhusiwi kukesha. Wazee wana fitna sana hawa ni balaa. Mafia iko uchi kifursa yaani ni rahisi kuziona fursa za kupiga hela lakini ukiingia. Changamoto za kiroho, mzunguko mdogo wa hela, usafiri wa wananchi mmoja mv kilindoni, kufitiniwa.
Car wash ya kibabe, utapata magari labda ya halmashauri na madereva mara nyingine huosha wenyewe ili wabakie na vijihela. Watu binafsi wana magari japo ni ya kuhesabu sana
Uje umejipanga bwashee