Msaada wakuu ni app gani inatumika kuedit au kuweka maneno KWENYE picha kama haya

Unajua mi encoder nilishindwa kuelewa kabisa.. au mybe mashine yangu uwezo mdogo...

Encoder mara nyingi nilikua natumia kwa after effects tuu..
Ila kwa premier hapana na export moja kwa moja...

Na now mzigo wa after effect huwa na render kule kule so mzigo unatoka kwa AVI format hapo ndo naingiza kwa premier inakua ishaisha..

Encoder nilitumia baada ya kuona after effects kuna project zinachukua mda ila baada ya kujua hii ya ku render kule kule nikaachana nayo
 
Media encoder kwa mimi naona ni kama kitu cha kutumia kwa dharura, kama vile siku una kazi nyingi tofauti za kurender ndiyo inafaa.

Lakini, kama una kazi moja tu ama unao muda, ni bora ukarender tu kawaida. Maana kulikuwa na madai ya kushusha quality kwa encoder.

Ila sijathibitisha hayo madai, ila kama unazilist kazi nyingi za kurender, kuna nyingine unaweza kuona zinasoma errors, lakini ukitazama unakuta zimekamilika kurender.

Ova
 
Hivi ukiwa una Render na encoder huku una uwezo wa kuendelea na ishu zingine sio..?

Unaweza ku render kazi zaidi ya moja kwa encoder..?
 
Hivi ukiwa una Render na encoder huku una uwezo wa kuendelea na ishu zingine sio..?

Unaweza ku render kazi zaidi ya moja kwa encoder..?
Yeah! Unaweza kurender hata kazi kumi na bado ukaendelea kufanya kazi nyingine ila hakikisha project unayoirender usiiguse.

Yaani huweza kurender project huku project hiyohiyo ukawa unaifanyia kazi, kule kwenye encoder itazingua.

Encoder uzuri wake unaweza ukarender kazi zote, kisha ukalala na asubuhi ukakuta zote ziko tayari, kuliko kurender moja moja kwa premiere.

Kwa encoder hukeshi nayo wakati unarender.

Ova
 
Hapo nishaelewa sasa.... Nilifutiliaga mbali baada ya kuona nayo inazingua yaani kuweka audio spectrum tuu kwa audio caver ika render kwa masaa 2
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ
Nikaona hapa bora niwe na software special ya audio spectrum tuu
 
Ongeza uwezo wa mashine yako, ama tafuta mashine kubwa kidogo ili kupunguza huo muda wa kurender, ni mrefu sana.

Ova
 
Wakuu swali langu ni Hilo nataka nijue ni app gani inatumika KUANDIKA maneno juu ya picha hivyo
Mkuu wadau juu washa jibu mengi ila kuongezea unahitaji software inayoruhusu kucheza na layers, kwenye hio picha kuna layer nyingi zimeunganishwa.

Mfano kwa simu hiki Kipicha nimetumia program inaitwa pocket paint ipo store inaruhusu kucheza na layer

Sema kama upo serious photoshop inafanya hiyo kazi kwa ufanisi na haraka zaidi. Utahitaji pc.
 
Unaweza kunijibu kwanini IDM au Internet Download Manager inaweza kupakua file kwa kasi kuliko speed ya browser ya kawaida, je IDM inaongeza kasi ya internet au inatumia server za utofauti?

Adobe Media Encoder ina accelerate process ya rendering.. inafanya optimization flani wakati wa rendering..

Kuhusu specs za machine itategemea na version ya software unayotumia but given una render video moja kwenye machines tofauti moja inatumia media encoder nyingine haitumii, basi ujue yenye encoder itawahi.

Kingine media encoder inasaidia kutoa videos kwenye format nyingi kitu ambacho after effects peke yake haiwezi, inabidi ufanye exportation then uanze ku convert kitu ambacho kinachukua muda sana.
 
Encoder ni accelerator most of time kwenye hizi softwares, kama alivyokujibu mkuu Mdakuzi zinapunguza quality na kufanya kazi ya masaa kufanyika mda mchache. Hizi hazitumii cpu wala gpu bali ni accelerator ambazo zinajitegemea na zinaweza kuwekwa ndani ya cpu na gpu ili zikiwa zinatumika cpu yako ama gpu iendelee kufanya mambo mengine.

Mfano wake ni kama Intel Quicksync, Nvidia Nvenc, Amd VCE etc

Kama unatumia cpu/Gpu ya zamani unaweza usielewe ila ukiwa na hardware ya kisasa unaweza ku render in real time.
 
After effects in addons au extensions nyingi sana online ambazo zinaweza kufanya kitu kama hiko.

Kuhusu size ya file inategemea ume export kwa format ipi adobe media encoder inakupa options nyingi za format kuanzia 4K hadi formats za smartphones.

After effects na adobe photoshop zinafanya kitu kimoja, sema photoshop inaweka effects kwenye picha moja hali ya kuwa after effects inaweka visual effects kwenye frames au picha zinazokamilisha video, mfano picha unabadili background kwenye photoshop, after effects inabadili background ya video nzima lakini inavyofanya kazi inacheza na frame moja baada ya nyingine hadi imalize, video ni mkusanyiko wa picha nyingi zinazopita kwa haraka zikiunganishwa na sauti, after effect unaweza weka effect kwenye frame moja ya video baada ya nyingine watengenezaji wakafanya urahisishaji zaidi na automation za kutosha, ukiwa na after effects latest sasa hivi inatumia AI inapiga effects za kufa mtu kwa clicks chache tu tena walitoa beta version ambayo ipo free sijui kama bado ipo free.

Unity hapana sijatumia lakini concepts ni zile zile tu, kama unafanya animation na unatumia sana adobe unaweza kutumia adobe animator.. nilitumia sana blender kwa sababu ni open source...

Labda nikuambie kitu kimoja, ukitaka kuwa deep kwenye graphics ama issue yeyote jaribu kuwa wa tofauti, vitu vingi vyepesi anafanya kila mmoja, kitu chochote anaweza fanya kila mtu ni worthless, fanya vitu wanaweza kufanya wachache, kama unaiona after effects ni ngumu basi deal nayo hio hadi hollywood wanatumia sana after effects, lakini kama tu graphics ni kazi yako, na utatisha sana.

Hivi vi software kwenye android n.k ni vizuri kwa issues simple.

Filmora na adobe premiere zote ni softwares kwa ajili ya video editing ambazo zinakuja na basics za visual effects, color correction n.k, lakini after effects ina kila kitu kuanzia editing, rangi hadi sauti, lakini ukija kwenye rangi kuna softwares ambazo ni advanced zinatumiwa na studios za movies hadi hollywood mfano Da Vinci Resolve japo nayo hadi ina editing visual effects n.k ni bonge moja la software hata premiere inasubiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…