Msafara wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wapata ajali. Mmoja wa Watumishi wake afariki

Msafara wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wapata ajali. Mmoja wa Watumishi wake afariki

Hii ni kwa mujibu wa ITV .

Taarifa zaidi zitawajia ....

UPDATE
Mhudumu wa ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hamis Machenga amefariki dunia baada ya msafara wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kupata ajali nje kidogo ya mji wa Zanzibar na watu kadhaa wamejeruhiwa.
Sa kamji kenyewe kama Dar hadi Mlandizi mbio za nini
 
Poleni sana wafiwa. Poleni majeruhi.

Kuna kitu hakipo sawa. Maafa yamekuwa mengi. Wenye imani wanahitaji kutafakari. Enzi zile, kukiwa hivi, watu waliwaendea manabii kuwauliza, kuna nini na wafanye nini?

Mimi siyo nabii na wala hata sikaribii kwa lolote. Mimi siyo mtaalam wa maandiko japo nayasoma maandiko kadiri ninavyojaliwa.

Viongozi wa Serikali, wenye imani wayatafakari tunayoyapitia, na waone ni kawaida au tunapita milima mikali yenye miba.

Kiimani, 'dhuluma huzaa laana'. Uongozi ni utumishi. Viongozi huchaguliwa na Mungu kwa kupitia watu wake. Na hao ndio wanaotengeneza mamlaka ya kutoka Mungu. Using'ang'anie madaraka wala kuyapora kwa nguvu au hila maana juu yupo aliyemkuu na mwenye uwezo wa kukatisha mbinu zote za mwanadamu.

Mungu atujalie hekima ya kujua kilicho muhimu katika maisha yetu ya sasa na ya baadaye.
 
Mhudumu wa ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hamis Machenga amefariki dunia baada ya msafara wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kupata ajali nje kidogo ya mji wa Zanzibar na watu kadhaa wamejeruhiwa.
Kiswahili hakipo sawa hapa. Bora ingesomeka " Gari moja au magari mawili yaliyokuwa ktk msafara yamepata ajali" sio Msafara wote as if magari yote yamepata ajali. RIP marehemu na majeruhi mungu awape nafuu haraka.
 
Back
Top Bottom