Poleni sana wafiwa. Poleni majeruhi.
Kuna kitu hakipo sawa. Maafa yamekuwa mengi. Wenye imani wanahitaji kutafakari. Enzi zile, kukiwa hivi, watu waliwaendea manabii kuwauliza, kuna nini na wafanye nini?
Mimi siyo nabii na wala hata sikaribii kwa lolote. Mimi siyo mtaalam wa maandiko japo nayasoma maandiko kadiri ninavyojaliwa.
Viongozi wa Serikali, wenye imani wayatafakari tunayoyapitia, na waone ni kawaida au tunapita milima mikali yenye miba.
Kiimani, 'dhuluma huzaa laana'. Uongozi ni utumishi. Viongozi huchaguliwa na Mungu kwa kupitia watu wake. Na hao ndio wanaotengeneza mamlaka ya kutoka Mungu. Using'ang'anie madaraka wala kuyapora kwa nguvu au hila maana juu yupo aliyemkuu na mwenye uwezo wa kukatisha mbinu zote za mwanadamu.
Mungu atujalie hekima ya kujua kilicho muhimu katika maisha yetu ya sasa na ya baadaye.