Msafara wa Mwigulu Nchemba. Je, Kipindi Cha Magufuli ungeyafanya Haya?

Msafara wa Mwigulu Nchemba. Je, Kipindi Cha Magufuli ungeyafanya Haya?

Bado unaamini mwigu ataendelea kuwa WAZIRI??! Atatoswa pamoja na kupendwa kwake!!!
‘Extended Credit Facilities’ waliyopewa na IMF majuzi inaenda sambamba na ‘structure adjustment policies’ (SAP) mnazokubaliana ili upewe mkopo.

Serikali imetunga Tozo budget ya mwezi wa sita IMF wamekubali kuwapa mkopo awamu ya kwanza mwezi wa saba. Unaweza kuona ‘cause and effects’ za hiyo mikopo.

Kwa ivyo kumtoa Mwigulu hapo huyo atakae kuja lazima awe na majibu ya ku-meet IMF conditions za makusanyo hiyo equation ipo palepale with or without Mwigulu.

Alternative ya Tozo ni kuongeza makusanyo na kubana matumizi; njia ambazo kazivuruga raisi mwenyewe.

Sasa unadhani given the scenario ata mtoa kweli huyo Mwigulu hapo bila ya kujua anawezaje ku meet policy adjustment walizo kubaliana na IMF.

Never say never ila sioni akimtoa Mwigulu hapo ambae kwa sasa anachukua matusi kwa niaba yake.
 
Hawa watu bodaboda huwa hawaendi kwenye misafara hii bila kuwalipa...

Huyu Mwigulu anatoa wapi pesa za kuwalipa hawa iwapo yupo kwenye safari za kawaida tu za kikazi za serikali huku tukijua hulipwa posho ya safari kama mtumishi wa umma..??

Ndo kusema pesa ya posho yake ya safari analipa bodaboda wa kumwimbia barabarani badala ya kuachia familia yake ili wanunue chakula na maji...?

Hawa viongozi wetu mbona hawana haya wala aibu kiasi hiki..? Anawezaje kuwatumilia vumbi wananchi masikini hawa anaowatoza tozo huku yeye akiwa kwenye V8 New Model la TZs 600,000,000 peke yake...? Ina make sense kweli hii...?

Yaani katikati ya hali ngumu kifedha kwa wananchi na kufunga mikanda (maana wanatuambia hivyo) lakini cha ajabu wao wanatumia mali ya umma hovyo hovyo kiasi hiki halafu wanataka tukubaliane na mambo yao ya kijinga...?

Mbona wanatufanya wananchi majuha na wajinga hivi...?

Nani atabisha kuwa hawa sio wezi wa mchana kweupe wa fedha zetu za tozo na kodi...???

Matendo yao yanathibitisha madai haya bila shaka yoyote...
Acha awanyoroshe. Mwigulu kanyagia hapo hapo.
 
Kifupi ni kwamba kijana hajielewi na hajui njia ya kupita kuelekea pale juu.

Njia anayojaribu kutumia ni ya kitoto saaana na wakimkatia tawi namuonea huruma sana atapiga mueleka mkuuubwa sana na ile timu inaweza kufa.

Kama hiki anachokifanya hakina baraka za jamaa fulani basi namuonea huruma sana huyu kijana maana wakikubaliana wamtulize itakuwa mwisho mbaya sana kwake.
Yule jamaa atakuwa ametoa idhini. Ukiona kifaranga kinaruka ruka ujue mama yake yupo karibu
 
Savings alizokuwa anatumia Magufuli
  • Jaffo kusimamia miradi ya TAMISEMI kuhakikisha inajengwa kwa value for money.
  • Kutazama kwa karibu mapato na matumizi ya mashirika ya umma kwa kutaka hela zao ziwekwe hazina.
  • Kudai gawio serikalini mara ya mwisho mapato yalikuwa karibu trillion moja zaidi ya hela wanazokusanya sasa kwenye tozo
  • Kusimamia bandari vizuri kama chanzo cha mapato
  • Vitambulisho vya machinga
  • Kukaba wa kwepa kodi
  • Kubana matumizi hasa kwenye purchases za serikali kupitia ‘middle man’ wakati hizo taasisi zinaweza fanya wenyewe.
  • Kubana matumizi ya mikopo ya maendeleo na ku-divert hizo funds kwenye miradi yake ya mikakati hasa ile inayosimamiwa na TAMISEMI.
  • Kusimamia matumizi ya hela za mapato kwenye halmshauri
The list is endless, yote hayo hayapo sasa.
Unaishi kwa hisia zaidi, tunaita hearsay. Kwahiyo sasa hivi hakuna Waziri wa TAMISEMI au? Weka takwimu kila kipengele hapo ili tuelewe vizuri.
 
Kwani kuna kosa gani waziri nchemba kufanya ziara ama hao watu kumpokea kwa maandamano???? Siasa za chuki acheni
 
Ningekuwa mimi ndio Rais, namchungiza sana kwa siri kijua pesa ameweka nchi gani!

Ila nahisi yuko nyuma yake kuna gwiji ambalo hata Magufuli alilishindwa.
Gwiji lililokuja kumtoa ndugu yake alipokamatwa na shehena ya bunduki
 
Anamchukulia mama Poa.....Hili kundi litampa mama tabu sana. Tena wanamuimbia, tuna imani na Mwigulu?

Namuona na chapombe kando yake
anachokifanya NchembaMWIGULU hakina tofauti na alichofanya NNDUgay..
muda ukifika tutapata majibu yaleyale
 
H
Yale majamaa yanamchora tu, yanaishia kusema amuulize mwenzie EL kilichomkuta.

Kijana anajisahau labda kama wakali wa hizi kazi ndio wamempa hizo baraka lakini tofauti na hapo anaweza kufilisika kabisa huyu kijana, EL mwenzie pamoja na mizizi mirefu wahuni walimtingisha.
Ayo majamaa nayo majizi siku hizi. Hayana time
 
Back
Top Bottom