Msaidizi wangu wa ndani anagawa vitu vyangu kwa wanandoa

Msaidizi wangu wa ndani anagawa vitu vyangu kwa wanandoa

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2015
Posts
28,122
Reaction score
52,886
Jamani nina huzuni mwenzenu acheni tu na mvua hizi. Kama nilishawahi kukukosea humu kwanza nisamehe
kuwa single parent jamani kila kitu kinakuzoom wewe sio mchezo.

Unajitahidi wanao basi wasipate shida. Unajitesa kuweka mambo sawa ila kuna mtu anakuja kumlaghai dada wa kazi ampe vitu na huku yeye ana mume.

Kusema kweli moyo wangu unavuja damu maana kwanza nimechoka balaa yaaani

Naombeni tu mnifariji wenzenu maana huyu dada ni mlezi mzuri wa watoto halafu niko nae kitambo sana hata kabla sijazaa drama za wasichana mnazijua

Nifanyeje jamani

Me kununua vitu kidogo kidogo siwezi kuna sikunitakuwa sina.hela iwe shida .
 
Wangu alikuwa anagawa unga, sukari, anapika chakula cha ziada anagawa, n.k.

Epuka kumfokea ama kukasirika, muelimishe kwanza kwasababu wengi huwa wametoka vijijini wanataka kuishi maisha ya kijamaa ya kijijini na pia upweke wa nyumbani unawachosha wanatafuta kampani za nje bila kujua mjini kupo tofauti

Kuna vitu sina budi inanilazimu kumvumilia tu maana analea watoto fresh, anapika vizuri, n.k. shida yake nyingine anaacha TV ipo on muda wote. bora hizi kero kuliko aanze visasi vya kimya kimya mnadhani mnakula chakula kumbe nnya, vipigo kwa watoto ukiwa haupo, n.k.
 
Back
Top Bottom