Uchaguzi 2020 Msajili: Vyama vya siasa vyenye lengo la kushirikiana uchaguzi mkuu vimeshachelewa

jingalao

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
36,197
Reaction score
29,717
Afisa kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama ameeleza kuwa iwapo vyama vinataka kuunda ushirikiano vinapaswa kufanya hivyo kwa kufuata utaratibu wa vikao rasmi na sio utashi wa viongozi.
Ameainisha kuwa muda wa kufanya coallition ni miezi mitatu kabla ya kuanza kwa mchakato wa uchaguzi.

Tuwe tunasoma kanuni !

---

Vyama vya Siasa ambavyo vinatarajia kushirikiana wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu bila kufuata Sheria ya Vyama vya Siasa kama ilivyoainishwa kwenye Kifungu Na.11 (a) cha Sheria hiyo vitakuwa vimevunja sheria.

Onyo hilo limetolewa leo jijini Dodoma na Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, wakati alipofanya mahojiano kuhusu msimamo wa ofisi yake kwenye suala la ushirikiano wa vyama vya siasa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Nyahoza amesema kuwa ushirikiano wa vyama hivyo umeratibiwa vizuri kisheria ambapo vyama vinapohitaji kushirikiana vinapaswa kutumia vikao halali vya chama badala ya utashi wa mtu binafsi. Msajili Msaidizi Nyahoza ameongeza kuwa baada ya vikao halali kupitisha azimio la kufanya ushirikiano vyama husika vinapaswa kuwasilisha mkataba wa ushirikiano Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa miezi mitatu kabla ya mchakato wa uchaguzi kuanza.

“Vyama havijakatazwa kushirikiana bali vimewekewa utaratibu ili Tume ya Uchaguzi pamoja na taasisi zote zinazohusika na uchaguzi ziweze kujiandaa vizuri na kuimarisha ulinzi hasa wakati wa kampeni pamoja na kuvisaidia vyama vingine kuelewa wanashindana na vyama vya aina gani” alisema Nyahoza.

Kuhusu ushirikiano wa vyama vya siasa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2020 Msajili Msaidizi Nyahoza ameelezea kuwa mpaka sasa ofisi yake haijapokea mkataba wa makubaliano ya ushirikiano kutoka kwa chama chochote cha siasa hivyo kwa mujibu wa sheria vyama ambavyo vina nia ya kushirikiana vimeshachelewa.

Aidha, Msajili Msaidizi Nyahoza amesema hadi sasa vyama vyenye usajili wa kudumu ni 19 na chama kimoja kina usajili wa muda na maombi ya vyama 16 bado yanafanyiwa upembuzi.
 
Cc..Mbati
Mrema
lipumba
DP
 
CCM inajua Watz si wajinga. Wakiungana tu wanapindua meza.
 
Onyo hilo lilitolewa jana jijini Dodoma na Msaidizi wa Msajili wa vyama vya siasa, Sisty Nyahoza alipofanya mahojiano kuhusu ushirikiano wa vyama vya siasa wakati wa uchaguzi mkuu wa Oktoba.

Nyahoza alisema ushirikiano umeratibiwa vizuri na sheria kuwa vyama vinavyotaka kushirikiana lazima vitoe taarifa ofisi ya msajili kwa maandishi, lakini hadi sasa hakuna chama chochote kilicholeta taarifa, hivyo kwa uchaguzi huu vimeshachelewa.

Maoni yangu;
Wakati TLP kinampendekeza Magufuli (CCM) kuwa mgombea wake wa urais kilitoa taarifa?

====

Maono ya kuungana wapinzania wanayo kwenye vichwa vyao muda mrefu ila wanaogopana kwa sababu ya ubinafsi na umimi.
Ubinafsi wao ndo unawafanya wao kuwa wapinzani uchwara kwa kupinga kila jambo jema la serikali.
Hapo tunasema upinzani Tanzania hakuna bali kuna waganga njaa tu.
 
Onyo hilo lilitolewa jana jijini Dodoma na Msaidizi wa Msajili wa vyama vya siasa, Sisty Nyahoza alipofanya mahojiano kuhusu ushirikiano wa vyama vya siasa wakati wa uchaguzi mkuu wa Oktoba.

Nyahoza alisema ushirikiano umeratibiwa vizuri na sheria kuwa vyama vinavyotaka kushirikiana lazima vitoe taarifa ofisi ya msajili kwa maandishi, lakini hadi sasa hakuna chama chochote kilicholeta taarifa, hivyo kwa uchaguzi huu vimeshachelewa.

Maoni yangu;
Wakati TLP kinampendekeza Magufuli (CCM) kuwa mgombea wake wa urais kilitoa taarifa?
Vitaleta vikiafikiana kushirikiana. Mambo yote ya siasa yalisimamishwa hadi 2020. Yangeshika kasi Aprili lakini kakaingia kagonjwa kadogo kacorona. Mambo ndio yanaanza sasa. Hajaulizwa deadline ilikuwa au ni lini? Nchi ya vi-wonder!
 
Je Sheria IPO na inasemaje?
Inaukomo wa muda tajwa?

Mimi ni mshabiki mzuri wa JPM lakini naupenda upinzani Kwa sababu haya tunayodhani yamefanywa na serikali hii ni makubwa na mazuri, ni Kwa sababu huko nyuma, wapinzani waliwaonyesha Watanzania Kwa jinsi CCM isivyofaa na uozo uliokuwa ukifanywa, na sasa inawalazimisha wajikakamue kuonesha kwamba wakizubaa tu upinzani unachukua hatamu

Kwa nini unapigwa vita kiasi hichi upinzani Wakati ndio unaosababisha anayeongoza serikari afanye kweli?
 
Back
Top Bottom