Uchaguzi 2020 Msajili: Vyama vya siasa vyenye lengo la kushirikiana uchaguzi mkuu vimeshachelewa

Uchaguzi 2020 Msajili: Vyama vya siasa vyenye lengo la kushirikiana uchaguzi mkuu vimeshachelewa

Maono ya kuungana wapinzania wanayo kwenye vichwa vyao muda mrefu ila wanaogopana kwa sababu ya ubinafsi na umimi.
Ubinafsi wao ndo unawafanya wao kuwa wapinzani uchwara kwa kupinga kila jambo jema la serikali.
Hapo tunasema upinzani Tanzania hakuna bali kuna waganga njaa tu.
Hakuna wapinzani Tanzania, Bali Kuna wajasiriamali,
 
Hiyo sheria anayoisema huyu naibu msajili ya vyama vya siasa kuungana/kushirikiaña imetungwa lini?

Mimi nijuavyo utaratibu wa mashirikiano ya vyama vya siasa katika uchaguzi ni uleule uliotumika mwaka 2015...

Kwamba mnakaa na mnakubaliana kuwa tumuunge mkono mgombea wa chama hiki katika ngazi ya Urais ama Jimbo (ubunge) na kata (udiwani)...

Hili linahitaji sheria na ruhusa gani ya Msajili? Linahitaji msajili kupewa taarifa gani na ya nini?
Nafikiri kuna tofauti kati ya kuungana na kushirikiana labda tuangalie kamusi
 
Nafikiri kuna tofauti kati ya kuungana na kushirikiana labda tuangalie kamusi

Well, tuliache la KUUNGANA kwa sababu typically ni la kisheria na hakuna sheria hiyo na vyama vyote vya siasa najua vinajua hili....

Na hili la kushirikiana kwa mtindo uleule walioutumia mwaka 2015 linahitaji sheria gani? Na Msajili anataka ataarifiwe kwa msingi UPI na ili iweje?
 
Hii kauli ya huyu kada wa ccm anayetapeli watu kwa kujiita naibu Msajili inaonyesha ule muungano wa UKAWA ndio walioshinda uchaguzi 2015 hivyo anahofu wakiungana Mara hii hujuma zitashindikana.
 
Sidhani kama wanashirikiana kwa kuunga vyama,,hawa wanashirikiana virtually,,wanaongea wanakubaliana kuachiana majimbo,etc
Ni kama mrema tu anavyoshirikiana na ccm,,haiko kisheria,haitambuliki bali ni uamzi wa tlp wamefanya na hakuna sheria itawazuia
 
atwambie tangu lini tokea vilipoanzishwa vyama vingi kuna vyama vilishirikiana au kuungana hata leo iwe ya pili?
 
Ajabu wanaotaka kuleta mabadiliko hawafahamu taratibu za nchi wanayotaka kuiongoza.

Watakuja kuwadanganya wafuasi wao hapo baadae kuwa wamekataliwa maombi yao kuungana na msajili anapendelea chama tawala.

Hiyo sheria ilitungwa kwa nia ovu. Ni wendawimu kuheshimu sheria zilizotungwa kwa nia ya kukomoa vyama fulani.
 
PLP na CCM hawana ushirikiano! Kwa ushirikiano, pande zote zinakaa chini na kuwa na maazimio ya pamoja. Lakini katika hilo mliwasikia TLP peke yake!

TLP sio chama cha siasa, ni kikundi kinachoongozwa na mzee mmoja muhuni.
 
Je Sheria IPO na inasemaje?
Inaukomo wa muda tajwa?

Mimi ni mshabiki mzuri wa JPM lakini naupenda upinzani Kwa sababu haya tunayodhani yamefanywa na serikali hii ni makubwa na mazuri, ni Kwa sababu huko nyuma, wapinzani waliwaonyesha Watanzania Kwa jinsi CCM isivyofaa na uozo uliokuwa ukifanywa, na sasa inawalazimisha wajikakamue kuonesha kwamba wakizubaa tu upinzani unachukua hatamu

Kwa nini unapigwa vita kiasi hichi upinzani Wakati ndio unaosababisha anayeongoza serikari afanye kweli?
Sasa sio Paul Silly bali Paul Brave. Utakuwa umeelewa. Hii ndiyo tafakuri. Sio takataka za akina Kawe Alumni, Nazgur na yote magonjwa mtambuka. Tunataka nchi yenye vijana smart, vijana wa kujivunia na sio wale wa buku saba. Anakurupuka na kudai: hujui maana ya maandamano. Akidhani maandamano ni fujo na virungu vya polisi. Maandamano ni matembezi ya hiari yanayolindwa na polisi na si kusambaratishwa na polisi. Lini tutafika huko? Yes, we can(Obama's voice)!
 
Hiyo sheria anayoisema huyu naibu msajili ya vyama vya siasa kuungana/kushirikiaña imetungwa lini?

Mimi nijuavyo utaratibu wa mashirikiano ya vyama vya siasa katika uchaguzi ni uleule uliotumika mwaka 2015...

Kwamba mnakaa na mnakubaliana kuwa tumuunge mkono mgombea wa chama hiki katika ngazi ya Urais ama Jimbo (ubunge) na kata (udiwani)...

Hili linahitaji sheria na ruhusa gani ya Msajili? Linahitaji msajili kupewa taarifa gani na ya nini?
Anataka uteuzi tu. Amechoka kuwa naibu msajili. Anataka kuwa msajili fool! Atasikikaje? Ndio tena kujifanya hamnazo. Kwake hakuna tofauti kati ya kuungana na kushirikiana!
 
Maono ya kuungana wapinzania wanayo kwenye vichwa vyao muda mrefu ila wanaogopana kwa sababu ya ubinafsi na umimi.
Ubinafsi wao ndo unawafanya wao kuwa wapinzani uchwara kwa kupinga kila jambo jema la serikali.
Hapo tunasema upinzani Tanzania hakuna bali kuna waganga njaa tu.

Hapo umeongea jambo la mbolea mkuu
 
Msajili msaidizi wa vyama vya siasa mh Nyahoza amesema vyama vyenye lengo la kushirikiana katika uchaguzi mkuu wa 2020 vimeshachelewa.

Msajili amesisitiza kuwa sheria inatamka babayana makubaliano ya kushirikiana yafanyike miezi mitatu kabla ya tarehe ya uchaguzi na si vinginevyo.

Source: Swahili Times
 
Anawashwa huyo.
CDM tukiona ACT ina nguvu kata flani/jimbo hatusimamishi mgombea tunawachia ACT kama ndiyo wenye nguvu hapo.

Mataga mnahaha kama kuku aliyekatwa kichwa.
 
hii sheria imefanyiwa marekebisho au ndio ile ile iliofanya kazi mwaka 2015?
1596521496615.png
 
Afisa kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama ameeleza kuwa iwapo vyama vinataka kuunda ushirikiano vinapaswa kufanya hivyo kwa kufuata utaratibu wa vikao rasmi na sio utashi wa viongozi.
Ameainisha kuwa muda wa kufanya coallition ni miezi mitatu kabla ya kuanza kwa mchakato wa uchaguzi.

Tuwe tunasoma kanuni !

---

Vyama vya Siasa ambavyo vinatarajia kushirikiana wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu bila kufuata Sheria ya Vyama vya Siasa kama ilivyoainishwa kwenye Kifungu Na.11 (a) cha Sheria hiyo vitakuwa vimevunja sheria.

Onyo hilo limetolewa leo jijini Dodoma na Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, wakati alipofanya mahojiano kuhusu msimamo wa ofisi yake kwenye suala la ushirikiano wa vyama vya siasa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Nyahoza amesema kuwa ushirikiano wa vyama hivyo umeratibiwa vizuri kisheria ambapo vyama vinapohitaji kushirikiana vinapaswa kutumia vikao halali vya chama badala ya utashi wa mtu binafsi. Msajili Msaidizi Nyahoza ameongeza kuwa baada ya vikao halali kupitisha azimio la kufanya ushirikiano vyama husika vinapaswa kuwasilisha mkataba wa ushirikiano Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa miezi mitatu kabla ya mchakato wa uchaguzi kuanza.

“Vyama havijakatazwa kushirikiana bali vimewekewa utaratibu ili Tume ya Uchaguzi pamoja na taasisi zote zinazohusika na uchaguzi ziweze kujiandaa vizuri na kuimarisha ulinzi hasa wakati wa kampeni pamoja na kuvisaidia vyama vingine kuelewa wanashindana na vyama vya aina gani” alisema Nyahoza.

Kuhusu ushirikiano wa vyama vya siasa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2020 Msajili Msaidizi Nyahoza ameelezea kuwa mpaka sasa ofisi yake haijapokea mkataba wa makubaliano ya ushirikiano kutoka kwa chama chochote cha siasa hivyo kwa mujibu wa sheria vyama ambavyo vina nia ya kushirikiana vimeshachelewa.

Aidha, Msajili Msaidizi Nyahoza amesema hadi sasa vyama vyenye usajili wa kudumu ni 19 na chama kimoja kina usajili wa muda na maombi ya vyama 16 bado yanafanyiwa upembuzi.
Msajili anaacha kazi zake anashughulika na siasa za kuisemea CCM,
Huku Zanzibar Mwinyi ameshaanza kampeni,Mabango kila kona na kwenye vioo vya matangazo barabarani.
Ingelikuwa kuna Bango moja tuu la Mali seif Msajili angeliibuka na kusema chamakitafutwa kwa kukiuka taratibu.

Kuhusu Kushirikiana kwetu kuna muhusu nini? Pili pili aso ila inamuwashia nini?
Au Yeye yuko pale kuisaidia CCM isipate upinzani wa nguvu.?
Huku Znzibar ZEC wanapiga kura siku 2 ,mbona yeye hajatowa kauli?
Au huko Bara nako wanapiga siku Mbili?
Ajabu hii, eti Zanzibar kuna watendaji wengi zaidi wa tume ambao inabidi wapige kura siku moja kabla kuliko Bara!

Vyama vina lalamika Msajili kimyaa .

CCM wanakauli mbiu USHINDI LAZIMA

2015 Tume ya Uchaguzi ZEC iliuta matokeo baada ya kuona CUF imeshinda uraisi, NEC wakasema wao hawahusiki na utumbo huo.
ZEC wakasema ni kwa uchaguzi wa Raisi wa Zanzibar na wawakilishi tuu na madiwani si kwa wabunge .
Msajili kimyaaaa ,anaona taratibu zinakiukwa mchana kweupe anaufyata kwa kuwa anayevunja ni CCM.

Bilshit. Siasa za Taka Taka na Msajili wa Vyama asiyejitambua.

SISA BADO AFRIKA HUKU NI MBAVU TUUU.
 
Back
Top Bottom