Afisa kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama ameeleza kuwa iwapo vyama vinataka kuunda ushirikiano vinapaswa kufanya hivyo kwa kufuata utaratibu wa vikao rasmi na sio utashi wa viongozi.
Ameainisha kuwa muda wa kufanya coallition ni miezi mitatu kabla ya kuanza kwa mchakato wa uchaguzi.
Tuwe tunasoma kanuni !
---
Vyama vya Siasa ambavyo vinatarajia kushirikiana wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu bila kufuata Sheria ya Vyama vya Siasa kama ilivyoainishwa kwenye Kifungu Na.11 (a) cha Sheria hiyo vitakuwa vimevunja sheria.
Onyo hilo limetolewa leo jijini Dodoma na Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, wakati alipofanya mahojiano kuhusu msimamo wa ofisi yake kwenye suala la ushirikiano wa vyama vya siasa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Nyahoza amesema kuwa ushirikiano wa vyama hivyo umeratibiwa vizuri kisheria ambapo vyama vinapohitaji kushirikiana vinapaswa kutumia vikao halali vya chama badala ya utashi wa mtu binafsi. Msajili Msaidizi Nyahoza ameongeza kuwa baada ya vikao halali kupitisha azimio la kufanya ushirikiano vyama husika vinapaswa kuwasilisha mkataba wa ushirikiano Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa miezi mitatu kabla ya mchakato wa uchaguzi kuanza.
“Vyama havijakatazwa kushirikiana bali vimewekewa utaratibu ili Tume ya Uchaguzi pamoja na taasisi zote zinazohusika na uchaguzi ziweze kujiandaa vizuri na kuimarisha ulinzi hasa wakati wa kampeni pamoja na kuvisaidia vyama vingine kuelewa wanashindana na vyama vya aina gani” alisema Nyahoza.
Kuhusu ushirikiano wa vyama vya siasa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2020 Msajili Msaidizi Nyahoza ameelezea kuwa mpaka sasa ofisi yake haijapokea mkataba wa makubaliano ya ushirikiano kutoka kwa chama chochote cha siasa hivyo kwa mujibu wa sheria vyama ambavyo vina nia ya kushirikiana vimeshachelewa.
Aidha, Msajili Msaidizi Nyahoza amesema hadi sasa vyama vyenye usajili wa kudumu ni 19 na chama kimoja kina usajili wa muda na maombi ya vyama 16 bado yanafanyiwa upembuzi.
Msajili anaacha kazi zake anashughulika na siasa za kuisemea CCM,
Huku Zanzibar Mwinyi ameshaanza kampeni,Mabango kila kona na kwenye vioo vya matangazo barabarani.
Ingelikuwa kuna Bango moja tuu la Mali seif Msajili angeliibuka na kusema chamakitafutwa kwa kukiuka taratibu.
Kuhusu Kushirikiana kwetu kuna muhusu nini? Pili pili aso ila inamuwashia nini?
Au Yeye yuko pale kuisaidia CCM isipate upinzani wa nguvu.?
Huku Znzibar ZEC wanapiga kura siku 2 ,mbona yeye hajatowa kauli?
Au huko Bara nako wanapiga siku Mbili?
Ajabu hii, eti Zanzibar kuna watendaji wengi zaidi wa tume ambao inabidi wapige kura siku moja kabla kuliko Bara!
Vyama vina lalamika Msajili kimyaa .
CCM wanakauli mbiu USHINDI LAZIMA
2015 Tume ya Uchaguzi ZEC iliuta matokeo baada ya kuona CUF imeshinda uraisi, NEC wakasema wao hawahusiki na utumbo huo.
ZEC wakasema ni kwa uchaguzi wa Raisi wa Zanzibar na wawakilishi tuu na madiwani si kwa wabunge .
Msajili kimyaaaa ,anaona taratibu zinakiukwa mchana kweupe anaufyata kwa kuwa anayevunja ni CCM.
Bilshit. Siasa za Taka Taka na Msajili wa Vyama asiyejitambua.
SISA BADO AFRIKA HUKU NI MBAVU TUUU.