Msamaha: Mzee Kinana amuangukia Rais Magufuli kufuatia mazungumzo yake na makada wenzake wa CCM yaliyovuja

Msamaha: Mzee Kinana amuangukia Rais Magufuli kufuatia mazungumzo yake na makada wenzake wa CCM yaliyovuja

Huyu mzee yuko Smart sana. Hana mishe mishe za ajabu kama makada wengine wa Chama Cha Mapinduzi
 
Chuki yanini mkuu,huwa nasikitika sana kuona mtu humu jukwaani anakuwa siriazi na mambo ya mitandao,pole mkuu,relax maisha ni mafupi sana jipe raha,sina chuki na wewe hata kidogo mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata hapa jukwaani ni mtandaoni pia na wewe hukauki humu. Kuwa mpole tu wala hakuna chuki, wenye chuki ni wale wanaoteka, kutesa na kupiga risasi wale wasiokubaliana nao kimtazamo. Mungu ibariki Tanzania.
 
Kodi za watanzania zilizonunua ndege ndo hizo trilion 1.5.Usiwe king'ang'anizi bwashee
kodi za watanzania matumizi yake huwa yanakaguliwa na kutolewa report na C.A.G na ni C.A.G huyohuyo ambae amepewa dhamana ya kukagua kodi zetu alisema hizo 1.5 hazijulikani zilipo kuna wajanja washafanya yao...sasa wewe ni nani tukuamini mkuu,wewe ndo mkaguzi mkuu wa mapato na matumizi ya serikali?

Mimi na wewe ili tujue mapato na matumizi ya serikali inatakiwa tusome report ya c.a.g ndo ina hayo majibu...sasa niwekee hapa huo ukurasa wa report ya c.a.g inayosema iyo 1.5 ilitumika kununua ndege??
 
digba sowey,
Hiyo "Mytake yako" kama ungechukua muda wa kuangalia body language ya Kinana nina hakika ungeifuta
 
Moto wa Magufuli unakula kila ajaye mbele yake.

Tundu lissu shujaa wa utabiri, kwani alisema. Mtu huyu akishatughurikia Wapinzani akitumaliza atawageukia ninyi.

Hivi maneno haya hawa viongozi wastaafu wanayasoma au kuyasikia?

Wamekubali kushughulikiwa ivi alafu kuonekana wapumbavu mbele ya jamii ya CCM na Watanzania!!!

Mungu tuokoe
 
Baada ya kimya cha muda mrefu hatimaye katibu mkuu mstaafu wa chama cha mapinduzi Comrade Abdulrahaman Kinana amejitokeza hadharani na kumuomba radhi mwenyekiti wa chama cha mapinduzi taifa dakta John Pombe Magufuli kwa matukio mbalimbali yaliyojitokeza baada ya kung’atuka katika uongozi chama hicho. Kinana pia amewaomba radhi watanzania na wanachama wa CCM aliowakwaza kwa kitendo kilichotokea.

Kinana akiwa na baadhi ya viongozi wakongwe wa chama hicho walipewa adhabu hiyo baada ya mazungumzo yao ya simu kunaswa wakimteta rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania dakta John Pombe Magufuli na kusambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii hali iliyosababisha uongozi wa CCM kuwaita na kuwahoji, viongozi hao wakiwemo wastaafu na waliopo madarakani.

Awali akizungumzia adhabu aliyopewa na chama Kinana amekiri kutokea kwa jambo hilo na kudai kuwa kama binadamu alighafilika na kudai kuwa akiwa ni mkongwe katika chama hicho adhabu ni utaratibu uliopo katika chama chochote kwa kiongozi au mwanachama anapokosea.

Wakati huo huo Komrade Kinana ametembea ofisi za CCM mkoa wa Arusha na kuzungumza na mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Arusha Zelothe stephen zelothe.

Tangu sakata hilo litokee Katibu mkuu huyo mstaafu wa CCM Abdulrahamani Kinana hakuwahi kusikika katika vyombo vya habari wala mitandao ya kijamii kuzungumzia sakata hilo.
magu.jpeg
 
CCM imekuwa ya hovyo haijawahi tokea, yaani mtu kaomba msamaha mnavujisha mtandaoni ili iweje? au mlikuwa mnauwinda msamaha wake? kumbe ukitaka kuwateka ccm kirahisi waombe msamaha.
 
Inaonekana wazi mzee kinana kafanya hivyo kwa basi tu alimradi. Kazi kubwa imefanyika kumshawishi. Wenzake wameomba radhi ili kulinda maisha yao ya kisiasa, au ya watoto wao, kama mzee Makamba.

Kinana ana msimamo. Anaonekana haelewi inakuwaje barua yao ya malalamiko iwekwe kando, badala yake wavuliwe nguo wao? Ama kweli CCM imepatikana. Hakuna haki, hakuna demokrasia, ni kumlamba Magu miguu tu. Poleni wanaccm
 
Source wapi mkuu ila hii habari kama ni kweli kuna watu watanuna na kupasuka, Maana tayari walishaanza kusema twende na Kinana 2020 haha, Mimi nilisha sema hakuna kitu mtu ataweza kufanya akiwa nje ya mfumo, yaani nchi hii hakuna mtu aliepo nje ya mfumo anaweza kutingisha mfumo never ever hao kina Kinana kwa sasa ni kama mtu uwaoondoe meno afu uwape nyama ambayo haija iva fresh. Hata mkwere anajua ukishakuwa nje ya system huna impact tena
Ukizingatia hao wastaafu wana makandokando kibao
Wachache wanajua kua kwasasa tuna mungu ikulyu
 
Back
Top Bottom