Msamaha: Mzee Kinana amuangukia Rais Magufuli kufuatia mazungumzo yake na makada wenzake wa CCM yaliyovuja

Msamaha: Mzee Kinana amuangukia Rais Magufuli kufuatia mazungumzo yake na makada wenzake wa CCM yaliyovuja

Sauti ya Kanali mstaafu Mzee Abdulrahman Kinana haikubaliani na mwili/ mdomo wake ni kama analazimishwa vile atamke maneno au kawekewa aina ya shindikizo?
 
Yapo mengi ila wewe ndo unayaona kwa kuwa umepofuka, pia ni mawazo ya moyo wako tu kwa kuwa uliishi kwa mazoea.
Mambo yanabadilika bwashee.
Mbona umejibu tofauti na quote yenyewe? Au ukiwa CCM ndiyo excuse ya kunifanya Bia yetu
 
kodi za watanzania matumizi yake huwa yanakaguliwa na kutolewa report na C.A.G na ni C.A.G huyohuyo ambae amepewa dhamana ya kukagua kodi zetu alisema hizo 1.5 hazijulikani zilipo kuna wajanja washafanya yao...sasa wewe ni nani tukuamini mkuu,wewe ndo mkaguzi mkuu wa mapato na matumizi ya serikali? Mimi na wewe ili tujue mapato na matumizi ya serikali inatakiwa tusome report ya c.a.g ndo ina hayo majibu...sasa niwekee hapa huo ukurasa wa report ya c.a.g inayosema iyo 1.5 ilitumika kununua ndege??
Mkuu unahangaika na matanga??
 
Sina dhana mbaya kwa kila jambo la serikali acha kunichafua, bali ninakataa kwa nguvu zangu zote uovu wowote. Ni wapi umeona napinga serikali kujenga barabara? Ni wapi umeona napinga ujenzi wa hospitali? Je hayo sio mambo ya serikali? Acha kuchanganya mambo ya serikali na matumizi mabaya ya madaraka tafadhali.
Nakumbuka we jamaa niliwahi kukuletea clip juu ya kufufua reli ya Moshi toka Dar mwaka 2017 nadhani ukanambia hzo ndoto tu huyo Rais wenu hana uo ubavu! Nikakuambia muda utaongea ila nimeona mwaka jana December wachaga wakila nyama choma kwa mabehewa!
 
Mnaomsifiaga member ni jasusi mbobezi kumbe hana lolote aliongeaje na mapapai ya chato bila kujua
Huyu kinana na nape ni sawa na mapapai yaliyoenda mpaka chato na yakaomba yapimwe corona kwa jiwe
 
Umemsikiliza vizuri Kinana? Umemuelewa? Unajua ethics za uongozi wewe? Unajua umuhimu wa kipindi hiki kwa chama kuelekea uchaguzi mkuu?

Sasa elewa kuwa mzee Kinana ameombwa radhi ili kunusuru chama na kimaadili kaombwa aseme yale hadharani kurudisha imani ya wanachama.

Ndio maana hata lugha yake (tone) ilikuwa na dharau ndani yake. Mavuvuzela hamuwezi kuelewa hapo hata mpigwe nyundo kichwani
 
Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Abdulrahman Kinana amejitokeza na kumuomba radhi Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Dkt. John Magufuli kufuatia matukio yaliyojitokeza siku za nyuma ikiwemo mazungumzo ya simu baina yake na baadhi ya viongozi wakongwe wa CCM yakimlenga moja kwa moja Rais Magufuli.

Kauli hiyo ya Kinana ameitoa akiwa jijini Arusha, ambapo pia alipata nafasi ya kukutana na viongozi wa CCM mkoa wa Arusha akiwemo Mwenyekiti wa chama Mhe. Zelote Steven na Katibu wake Mussa Matoroka ambao wamemshukuru kwa hatua hiyo.

Kinana ambaye ni miongoni mwa wanasiasa wakongwe wa CCM, baada ya kustaafu alijiikuta katika malumbano na wanasiasa wenzake na pia viongozi wake ambazo hata hivyo hakuwahi kuzizungumzia.
====

My take: Waliokuwa wanadhani JPM ni moto wa mabua sasa wametambuwa kuwa walivyodhani haikua sahihi

Nimeusikiliza msamaha huu na jana nimeona kwenye TV news Kinana akiomba msamaha, hivyo sasa nakiri kwenye bandiko hili
Psychoanalysis ya Waomba Msamaha Kwa Rais, Makamba Snr is the Next, Membe Will Never for Pride, Kiburi na Jeuri, Kinana Will Never for Integrity
I was wrong kumhusu Kinana, sasa kwenye list ya kuomba msamaha bado Makamba na Membe.

P
 
Ukiwa mwanasiasa Ni Bora kusimamia kauli zako.
 
Umemsikiliza vizuri Kinana? Umemuelewa? Unajua ethics za uongozi wewe? Unajua umuhimu wa kipindi hiki kwa chama kuelekea uchaguzi mkuu?

Sasa elewa kuwa mzee Kinana ameombwa radhi ili kunusuru chama na kimaadili kaombwa aseme yale hadharani kurudisha imani ya wanachama.

Ndio maana hata lugha yake (tone) ilikuwa na dharau ndani yake. Mavuvuzela hamuwezi kuelewa hapo hata mpigwe nyundo kichwani
Mkuu acha kuzalisha Yale mwomba msamaha hakuyasema,wala hayamo moyoni mwake, tofauti na hapo ni ramli tu hii ufanyayo,

Kikubwa kinana kaomba msamaha kwa kinywa chake,hayo mengine ya kwambo sijui body language Mara tone tuuachie moyo wake maana ndo unajua dhamira yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliwahi kusema humu, hakuna aliyeshindana na mwenye mamlaka akashinda, mtu hata kama alikuwa Rais wa Nchii akishatoka madarakani hawezi kushindana na Rais aliyeko madarakani alashinda na ndio maana Mkapa, Kikwete na Mwinyi wote wanatulia kwakuwa wanajua Rais ana mamlka makubwa
 
Source wapi mkuu ila hii habari kama ni kweli kuna watu watanuna na kupasuka, Maana tayari walishaanza kusema twende na Kinana 2020 haha, Mimi nilisha sema hakuna kitu mtu ataweza kufanya akiwa nje ya mfumo.

Yaani nchi hii hakuna mtu aliepo nje ya mfumo anaweza kutingisha mfumo never ever hao kina Kinana kwa sasa ni kama mtu uwaoondoe meno afu uwape nyama ambayo haija iva fresh. Hata mkwere anajua ukishakuwa nje ya system huna impact tena.

Ukizingatia hao wastaafu wana makandokando kibao
Nimewahi kusema hii kitu humu, mfumo ndio kila kitu na wote hao wanajua ndio maana hawawezi kuleta fyoko fyoko wakafanikiwa
 
Nimeusikiliza msamaha huu na jana nimeona kwenye TV news Kinana akiomba msamaha, hivyo sasa nakiri kwenye bandiko hili
Psychoanalysis ya Waomba Msamaha Kwa Rais, Makamba Snr is the Next, Membe Will Never for Pride, Kiburi na Jeuri, Kinana Will Never for Integrity
I was wrong kumhusu Kinana, sasa kwenye list ya kuomba msamaha bado Makamba na Membe.

P
Due force of gravity, sometimes even rivers can start flowing upwards a mountain.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Abdulrahman Kinana amejitokeza na kumuomba radhi Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Dkt. John Magufuli kufuatia matukio yaliyojitokeza siku za nyuma ikiwemo mazungumzo ya simu baina yake na baadhi ya viongozi wakongwe wa CCM yakimlenga moja kwa moja Rais Magufuli.

Kauli hiyo ya Kinana ameitoa akiwa jijini Arusha, ambapo pia alipata nafasi ya kukutana na viongozi wa CCM mkoa wa Arusha akiwemo Mwenyekiti wa chama Mhe. Zelote Steven na Katibu wake Mussa Matoroka ambao wamemshukuru kwa hatua hiyo.

Kinana ambaye ni miongoni mwa wanasiasa wakongwe wa CCM, baada ya kustaafu alijiikuta katika malumbano na wanasiasa wenzake na pia viongozi wake ambazo hata hivyo hakuwahi kuzizungumzia.
====

My take: Waliokuwa wanadhani JPM ni moto wa mabua sasa wametambuwa kuwa walivyodhani haikua sahihi

Lumumba Bwana waliamua ''kumshit" huyu mzee na "madini" yake ..wakaja kustuka "kumekucha" baada ya Mchungaji Msigwa "kufanya yake" wiki tatu zilizopita...
 
Back
Top Bottom