Msamaha wa Spika Ndugai kwa Rais Samia ni kifo cha mende kwa lile kundi

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Walidhani wanaweza kutumia wingi wao kila idara na bungeni kutingisha gogo. Lkn wamekumbana na kisiki cha Zanzibar kikiwa kinalindwa na katiba ya nchi na chama. Wanaanzia wapi kuukata mpingo?

Aliyepewa jukumu la kukitikisa kisiki kapima kina cha maji halafu mwenyewe kaona isiwe taabu. Kwani kuomba msamaha shiling ngapi bwana??! Kajitokeza mwenyewe kuomba poo!

Huu wala siyo uchochezi. Lilikuwa battle la kweli kweli. Si mlimsikia yule mtendaji mkuu wa shughuli zote za serikali akiliongelea? Ilikuwa siyo mchezo.

Sasa mipango, ndoto na matumaini ya lile kundi kuirudia neema na kutamba kama mwanzo ndiyo yamekufa kabisa. Hakuna tena pa kuanzia.

Poleni sana wazee wa legacy.

Nyanengh'we!!
 
Watanyooka tuu nliwaambia mapema hawakunisikia
Sasa washasalimu amri Kama nivita wamenyoosha mikono juu

Lazima ufanye kile tutakachokuambia kwisha habari yenu
Mmetepeta mapema sasa tuone mtu ananyoosha mdomo wake tunaufekelea mbali
Wahuni nyie
 
Mna mihemko ya kitoto hata hamjui mnachoshangilia, hao wote bado ni CCM na siku zote wataendelea kulinda maslahi yao.

Wewe usije kurupuka kuikosoa serikali ukadhani ndio utasikilizwa, nawe utaonekana mpiga kelele tu, akili ndogo hata hujui madhara ya unachoshangilia.
 
Nimekosa mimi, nimekosa sana nimekosa mimi.
 
Nakumbuka ya Fred Mpendazoe

Kina Nape, Samwel Sitta na Mwakyembe wakamjaza akaanzisha Chama cha CCK wakamuahidi watajiunga nae…nae ghagla kwa mihemko ya Kanda ya Ziwa akatangaza kujiuzulu Ubunge wa Kishapu akajiunga chama kipya…

Jimboni aliekuwa anamshawishi ajiuzulu Ubunge kupinga 'ufisadi' wa Kikwete ndio akachukua form ya jimbo lile lile kupitia CCM na Team ya Kampeni kumtokomeza ikaundwa na Wale wale waliokuwa wanamshawishi akapotea na chama chake kikafa kabla hakijapata Uhai

Ndugai kastuka mapema

Ukitaka kuandika falsafa ya unafiki na usaliti ndani ya Chama basi Chapter ya kwanza mpe Lowassa kwa kuwa Jumbe na Seif tayari hawapo
 
Mna mihemko ya kitoto hata hamjui mnachoshangilia, hao wote bado ni CCM na siku zote wataendelea kulinda maslahi yao.
Kwa katiba hii, hakuna namna CCM itakaa iondoke madarakani bila ya yenyewe kusambaratika.

Ndiyo maana wenye akili wanashangilia mpasuko ndani ya ccm maana wanaona kama ukombozi unakaribia
 
Walidhani wanaweza kutumia wingi wao kila idara na bungeni kutingisha gogo. Lkn wamekumbana na kisiki cha Zanzibar kikiwa kinalindwa na katiba ya nchi na chama. Wanaanzia wapi kuukata mpingo?

Aliyepewa jukumu la kukitikisa kisiki kapima kina cha maji halafu mwenyewe kaona isiwe taabu. Kwani kuomba msamaha shiling ngapi bwana??! Kajitokeza mwenyewe kuomba poo!

Huu wala siyo uchochezi. Lilikuwa battle la kweli kweli. Si mlimsikia yule mtendaji mkuu wa shughuli zote za serikali akiliongelea? Ilikuwa siyo mchezo.

Sasa mipango, ndoto na matumaini ya lile kundi kuirudia neema na kutamba kama mwanzo ndiyo yamekufa kabisa. Hakuna tena pa kuanzia.

Poleni sana wazee wa legacy.
Wanalalamikia kodi wanayokusanya kwenda kuiendeleza Zanzibar kama vile sio sehemu ya Muungano. Wanadhani ipo salama kwa kuiendekeza hoja dhaifu ya Utanganyika!.
 
Kwa katiba hii, hakuna namna CCM itakaa iondoke madarakani bila ya yenyewe kusambaratika.

Ndiyo maana wenye akili wanashangilia mpasuko ndani ya ccm maana wanaona kama ukombozi unakaribia
CCM ni watu wanaounganishwa na chama chenye uzoefu mkubwa sana wa siasa. Wanajua namna ya kukaa pamoja baada ya kuwa na mpasuko.

Ni sawa na akili za fisi kutegemea siku moja utokee mpasuko mkubwa ndani ya chama. Sio kama TLP au NCCR, kile ni chama chenye misingi imara sana.
 
Ukishaona speaker wa Bunge ambae ni mhimili wa dola unaojitegemea ametoa msimamo wake juu ya jambo fulani halafu ghafla akamuomba msamaha Rais kwa msimamo aliotoa, jua hilo Taifa limefika mwisho na limekufa.

Kwenye hili mtu asipoona tena umuhimu wa katiba mpya basi huyo mtu ni maiti inayotembea.
 
CCM ni watu wanaounganishwa na chama chenye uzoefu mkubwa sana wa siasa. Wanajua namna ya kukaa pamoja baada ya kuwa na mpasuko.

Ni sawa na akili za fisi kutegemea siku moja utokee mpasuko mkubwa ndani ya chama. Sio kama TLP au NCCR, kile ni chama chenye misingi imara sana.
Njaaa tuu Kaka,, Mengine mbwembwe... tuu
 
Acha kujidanganya mwenyew,tegemeo kubwa lipo ktk ile katiba chakavu
CCM ni watu wanaounganishwa na chama chenye uzoefu mkubwa sana wa siasa. Wanajua namna ya kukaa pamoja baada ya kuwa na mpasuko.

Ni sawa na akili za fisi kutegemea siku moja utokee mpasuko mkubwa ndani ya chama. Sio kama TLP au NCCR, kile ni chama chenye misingi imara sana.
 
mkuu umewaza kitoto sana, wale ni watu wazima wameamua kucheza mind game kuwapoteza watu ili waendelee kusuka mipango yao kimya kimya, kwa sasa ccm haitakiwi kuwaamini hawa watu maana wana ajenda zao.
 
Back
Top Bottom