Tetesi: Msanii Alikiba ampa talaka tatu mkewe chanzo kikiwa ni ndugu na kurogana

Tetesi: Msanii Alikiba ampa talaka tatu mkewe chanzo kikiwa ni ndugu na kurogana

Kuna shost ile tumemaliza form four tu alimpata kaka mmoja yuko serious kwa ndoa. Kaka alishajenga ghorofa, harusi kubwa na mama mkwe alikuja kutoka Malampanda.

Baada ya harusi mama mkwe aligoma kurudi kwake. Maisha ndipo yaliponona hapo.
Dah huyo maza ni mjinga
 
Ila Kiba naye anakosea! Huwezi kuishi na familia kubwa hivyo wakati umeoa. Choko choko zitakuwa nyingi tu. Kingine ndugu wasichojua huwa wanataka wawejuu ya mke. Wakati mke ni kwake yeye ndiye mama mwenye nyumba watazinguana tu.

Kama anampunga angefanya kama mkewe alivyomshauri angewapa mitaji wakachakarike na maisha huko.

Kukaa na ndugu sawa ila siyo kukaa na kikosi.
Nime prove u zero brain wa kiba
 
Hivi Amina alienjoy mdinyo kweli? Maana raha ya mdinyo any time anywhere mnabanjuana sasa hiyo nyumba jamani mara zabibu, mara mama mkwe mara abdu mara kings artist mara watoto maskini bint wa watu hata hajafaidi, bora alivyojiondokea atapata mume atakayefaidi.

Mimi nilikaa ukweni mwezi tu kila siku nlitafuta sababu turudi kwetu maana ukianza kupika ndo mkwe weee kama mbuzi mbuzi mzima unahangaika nae, mpaka mda wa kuhudumia mume usiku kiuno kimeganda.
Na kudinyana kwenyewe inabidi mwanaume akuzibe mdomo kelele za mautamu wasisikie wakwe, ikitokea mume katoka mihangaiko labda kajibandikia chai unaona kabisa hao ndugu wanamind na kuweka kikao cha dharura.
Kuolewa familia ya kimaskini na waswahili waliojazana ndani ni UTUMWA.
Hahahaha nimecheka sana
 
Ndio tatizo la ndoa za kishwahili mnapishana na ndugu kwenye korido Kama nzi. Afrika kuchomoka bado Sana unaweza kuishi na ndugu zaidi ya watano nyumba moja,Dada wa kazi anafanya kazi ya kupika kuanzia asubuhi Hadi usiku utadhan ni mpisha wa hotel.mnapika chakula kingi Hadi kinakosa ladha .
Hili linasumbua familia nyingi sana, ndugu wanataka kuishi wanataka kwako yaan hata ile amani mkeo anakosa
Watu wakiwa wengi tatizo lazima liwepo
 
Wasalaam wajamvi!

Msanii Alikiba a.k.a King Kiba amempa talaka tatu mkewe Amina raia wa kenya baada ya kushindwa kupata muafaka juu ya ugomvi wao na ndugu wa Alikiba na Mama wa Alikiba.

Ndoa ya King Kiba ilianza kuingia dosari baada ya Amina kutaka ndugu wa Alikiba wakajitafutie maisha yao na wajitegemee jambo ambalo lilizua taharuki na ugomvi mkubwa baini ya ndugu wa Alikiba na Amina..

Amina alidai ni vigumu kuishi na watu wengi vile ndani ya nyumba moja hata kama ni ghorofa na bado kuwe na amani...hivyo alimshauri alikiba awape mitaji wakajitegemee au awapangie nyumba nyingine.....

Hili jambo liliendeleza mgogoro mkubwa hadi Mama Alikiba kiingilia kati na kutaka Alikiba amuache Amina na akadai apendi hata watoto wa Alikiba kuwa pale....

Wakati hayo yakiendelea kutafutiwa uvumbuzi mtoto wa Alikiba aliugua na kupatwa ugonjwa ulio sababisha awe ana anguka kila muda.....hili lilichochea moto kwani ndugu na Mama Alikiba waliamua kufunga safari hadi kwa fundi ndipo alipotoa tv [emoji342] na kuwaonesha chanzo cha ugonjwa wa mtoto ikidawa amelogwa na Amina mke wa King [emoji146] kiba.

Hivyo basi Mama na ndugu baada ya kutoka kwa fundi walirudi na kumchana live Amina kuwa anataka kumuua mtoto wa King Kiba hivyo lazima aondoke jambo ambalo lilizua ugomvi mkubwa huku Amina akilia kama mtoto na kuwambie hawezi na hana tabia hizo labda kama wanataka aachane na ndugu yao lakini wasimsingizie....

Ugomvi ulikuwa mkubwa sana kupelekea Amina kubeba mwanae na kurudi kwao mombasa huku akitaka kupewa talaka maana ndoa imemshinda!

Mnamo mwezi wa nane mwisho King Kiba alimpa talaka Amina ili aendelee na maisha yake uku wakishirikiana kulea mtoto.

Wasalaaam
Huwezi kuishi nyumba moja na ndugu wote hayo ni mambo ya zamani. Ndugu wenyewe wana uwezo wa kujitegemea. Hili suala la kuamini ushirikina waislam hamjambo. Nilikuwa na demu wa kiislam anapenda sana kuongelea masuala ya kwenda Kwa wataalam. Mpaka nilikuwa naogopa jinsi anavyoamini masuala ya uchawi. Kiutaratibu alikiba hakutakiwa kuishi nyumba moja na ndugu zake. Inatakiwa ndugu wa mke na mume wajitegemee
 
Ndoa nzuri mkioana mkae hata mwaka wenyewe mfurahie ndoa mfinyane wenyewe lakini duu ndoa zetu unatoka kwenu unasema ngoja nikale tunda la ndoa uwiiii unatumbukia kwenye kundi la watu 12, wakati mwingine sio uchoyo Bali nikupeana nafasi tu
For sure, ndoa hata mwaka bado then ndugu wanataka kuja hapo hapo
 
Huwezi kuishi nyumba moja na ndugu wote hayo ni mambo ya zamani. Ndugu wenyewe wana uwezo wa kujitegemea. Hili suala la kuamini ushirikina waislam hamjambo. Nilikuwa na demu wa kiislam anapenda sana kuongelea masuala ya kwenda Kwa wataalam. Mpaka nilikuwa naogopa jinsi anavyoamini masuala ya uchawi. Kiutaratibu alikiba hakutakiwa kuishi nyumba moja na ndugu zake. Inatakiwa ndugu wa mke na mume wajitegemee
Nadhani Mkuu utakuwa umekengeuka kidogo comment kwenye uzi uliotolewa but sio kwa kutusi dini nyingine sidhani kama inaleta afya
 
This is sad,pole Amina..uwe haupendani na ndugu za mumeo na mumeo anawa support ndugu zake..hio atmosphere ni ngumu...bora ukapumue mwaya!!
Namsikitika! Kukaa nyumba iliyojaa ndugu, wote wakimtegemea mumewe ni shughuli!
 
Kama ni kweli,Salama yake! Ashukuru maana hao siwaamini sana
 
Hivi Amina alienjoy mdinyo kweli? Maana raha ya mdinyo any time anywhere mnabanjuana sasa hiyo nyumba jamani mara zabibu, mara mama mkwe mara abdu mara kings artist mara watoto maskini bint wa watu hata hajafaidi, bora alivyojiondokea atapata mume atakayefaidi.

Mimi nilikaa ukweni mwezi tu kila siku nlitafuta sababu turudi kwetu maana ukianza kupika ndo mkwe weee kama mbuzi mbuzi mzima unahangaika nae, mpaka mda wa kuhudumia mume usiku kiuno kimeganda.
Na kudinyana kwenyewe inabidi mwanaume akuzibe mdomo kelele za mautamu wasisikie wakwe, ikitokea mume katoka mihangaiko labda kajibandikia chai unaona kabisa hao ndugu wanamind na kuweka kikao cha dharura.
Kuolewa familia ya kimaskini na waswahili waliojazana ndani ni UTUMWA.
Inahitaji kipaji cha hali ya juu.
 
This is sad,pole Amina..uwe haupendani na ndugu za mumeo na mumeo anawa support ndugu zake..hio atmosphere ni ngumu...bora ukapumue mwaya!!
Sure this is sad.
Napenda ndugu zangu lakin napenda zaid kuishi peke yangu na wanangu pamoja na mama yao.Wengine waje waslimie na kuondoka nitawasaidia huko huko waliko.
Ni changamoto kuishi na kundi ndani hata privacy mnakosa
 
Nakumbuka, Mama Salma Kikwete, wakati wa sherehe za harusi ya Alilkiba na Amina aliwauliza Wanawake waliohudhuria sherehe hiyo :
Wenzangu wanawake mliohudhuria sherehe hii wangapi mnapenda kuolewa mitara? Naomba mnyoshe Vidole.
Hapakuwa na jibu.

Hata hivyo alitoa nasaha nzuri sana kwa kumtaka Amina kuwa mvumilivu ndani ya Ndoa na kutofuatilia mambo ya mmewe na hasa kupitia kwenye simu ya mkononi.
Kubwa ni kwamba Wasichana wa kileo, wasomi na wajuzi wa mambo, kuolewa mitara na kudumu kwenye ndoa ni jambo gumu sana.
Hii ni kwa sababu wanaiga maisha ya kizungu zaidi kuliko ya Kiafrika au Kiarabu
Desturi za kuoa mke zaidi ya moja si za Kidini zaidi ila ni za Kiafrika na Kiarabu.
Desturi hizi sina masharti yake magumu nayo ni.
1. Nila lazima mwanaume awe na uwezo wa kuwatunza wake zake.
2. Mke mkubwa ni lazima aridhie mme wake kuoa mke mwingine na ashirikishwe katika kuchagua mke wa kuoa.
Ndoa za namna hii zinadumu kwa wanawake ambao elimu yao ni ya chini sana, hawachanganyiki kabisa na watu wengine na kutoka nyumbani huwa ni mara chache na hawaruhusiwi kutembea peke yao.
Pengine Ndoa za namna hii zitakoma jinsi ustaarabu unavyozidi kukua kwa wanaume kushindwa kuoa zaidi ya mke moja kutokana na wanawake kutaka elimu nzuri na watoto wote kusomeshwa hadi vyoo hadi vikuu.
Yote ni kheri tu kwa kuoa mke moja au wake wengi au kutokuoa kabisa, kubwa kuliko yote ni kuishi kwa upendo na amani.
 
Tabata mitaa gani hiyo mana kuna kipindi nlikaa dar kama wiki 2 mitaa ya sanene,nlikua namuona hapo kwetu pazuri
Mama haishi Tabata ila ila Tabata iko mkononi mwake hata sindano ikidondoka kajua na kafika
 
Back
Top Bottom