Msanii gani maarufu umewahi kuonana naye live mkaongea mawili matatu

Msanii gani maarufu umewahi kuonana naye live mkaongea mawili matatu

Nawakumbuka waha Mzee Majuto. Muhidine ngurumo. Bibi kidude. Yusuf chchu sound. Mungu awapumzishe na awasameh madhambi yao walioyatenda hapa duniani.
Wasanie wa kisasa hawakushangamkie kama huna pexa...
 
Hahahaaaa mi sikua teller nilikua customer service desk japo teller lazma atajua salio especially unapotaka kutoa hela
Ndio maana huwa sipendi kwenda kwa ma tellers aisee

Maana huku niliko Kuna mwanangu mmoja nimesomA nae olevel nae Ni teller sitaki hata ajue salio langu huko[emoji1787][emoji1787]

Uzuri Ni akaunti mbili mbili
 
mm wasanii wa bongo wengi nimeshakutana nao na story za hapa na pale...ila msanii mkubwa wa nje niliyepiga nae story ni chris tucker ni comedian huyu wa usa huko Hollywood..alikuja tz, arusha miaka hiyo 2008 ilikuwa ngorongoro huko ...sema dah akiongea uambulii kitu ile lafudhi ya ndani..
Ilea lafudhi ni changamoto sana asee, ila wakiandika tunagrab kama kiswahili mzeee dahb🤣🤣🤣
 
Miss Tanzania 2020, Rose Manfere hadi siamin kama amekuwa miss. Anasoma na mdogo angu pale Ardhi na ni best friends kinaz na wanakaa room moja basi huwa tunatanianaga kwa voice note whatsapp ila ndo hivo ndio mrembo wa taifa.
Ila honestly sijawahi kutana naye bado.
 
Ni P the Mc, tena alinikuta nasikiliza ngoma yake "mama mjane" dah ilikuwa fresh aisee, jamaa alikuwa happy sana nikamuonesha kwenye pc yangu Kuna ngoma zake karibu zote na wasanii wenzake WA tamaduni.

Sent from my 502SO using JamiiForums mobile app
Huyo mwamba nakubali sana flow zake za kimnato kama akina lunya, salmin swagg na con boy
 
Prof J, alikuja nyumban Songea alikua anazungumza na kaka mkubwa, mie nilikuwepo kwa pembeni. Na nilimsalimia, ikiwa bado hajawa mbunge.

Jux, huyu nilikutan nae Morogoro, GM HOTEL, kuna jambo lilitukutanisha

Foby, huyu ndo namjua in and out, nimecheza nae San, na mchumba ake alikua anaitwa rose, akiwa anasoma Ruhuwiko sec school (shule ya jeshi) ,
Hii shule iko wapi? 🤔🤔
 
Nlikutana na Cyril Kamikaze kituo cha polisi Rujewa Mbarali nlipoenda kuchukua loss report. Alikuwa amepeleka malalamiko ya kuzurumiwa tsh 25M na mtu aliekuwa anampa hela amlimie mpunga jamaa akatembea na mavuno. Alikuwa analima kwa simu.
Afu Cyril Kamikaze na Mabeste nashindwaga sana kuwatofautisha 🙄🙄
 
One day nilikuwa Vancouver baada ya kualikwa na mtasha mmoja week kadhaa. Katika outings kwenye cafe moja nikamuona Drake ila sikuwa na uhakika ila mwenyeji wangu akaniambia ni yeye basi nikawa starstruck ila nikawa naona aibu ikabidi niombe tu bodyguards wake jamaa nikaongea nae nikamwambia natokea bongo.

Akanisainia kitabu ambacho nilikuwa nimenunua cha Bones to Ashes.
 
Back
Top Bottom