Msanii Mbalamwezi kutoka kundi la 'The Mafik' afariki dunia ikidaiwa ni kutokana na majeraha ya kupigwa

Msanii Mbalamwezi kutoka kundi la 'The Mafik' afariki dunia ikidaiwa ni kutokana na majeraha ya kupigwa

Kundi kubwa la mziki hawana special security wa kutembea nao?
Na ukishakua msanii mkubwa kutembea tembea ovyo sio sawa , bora ukae nyumbani ulale. ,tembea kwa lengo maalum labda either unaenda kusain deal au kufanya airtime kwenye redio, na zaidi ukiwa unaelekea huko hakikisha una ulinzi na usiende na miguu....kama huna gari, basi ita hata UBER.
Mkuu ukabwa wa msanii una sifa zipi? Samahani lakini tunaomboleza ila tukibadilishana mawili matatu kwenye msiba wa MBALAMWEZI
 
duh alazwe pan
Saturday , 15th Dec , 2018

Msanii wa kundi la The Mafik anayejulikana kwa jina la Mbalamwezi, amekamatwa na jeshi la Polisi mkoa wa Kinondoni kwa tuhuma za wizi.

Tukio hilo limetokea hapo jana baada ya msanii huyo kumuibia dereva wa gari ya moja ya kampuni zinazotoa huduma za usafiri binafsi jijini Dar es salaam (Taxify), aliyejulikana kwa jina la Calvin.

Akisimulia tukio hilo Calvin amesema Mbalamwezi aliitisha usafiri akitumia simu ya mwenzake, lakini alipokuwa njiani alionekana kuwapigia simu watu kuomba hela kwani hakuwa na pesa ya kumlipa dereva, na ndipo alipochukua uamuzi wa kumuibia dereva baada ya kumfanya apoteze fahamu.

Meneja wa kundi la The Mafik aliyejitambulisha kwa jina la Kapasta amesema ni kweli kuna hilo tukio, lakini ndio yuko njiani akielekea kituo cha Polisi Oysterbay ambako msanii huyo amewekwa rumande ili ajue kinachoendelea.

East Africa Television ilifanya jitihada za kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Jumanne Muliro, lakini alijibu hawezi kuzungumza kwa wakati huo kwani alikuwa kwenye ziara ya Waziri Mkuu.

[Duh...! R I P
 
Kwahiyo ndio ilikua maskani,ukiona vijana wanaishi hivyo twn kuna mawili aidha wanavuta pamoja plus uwizi wa vifaa vya magari na ndio wengi sana wenye kula bata wkend masaki
Kwa pale walipokuwa wanakaa sijaskia issue hiyo
Kama wangekuwa karibu na watu wa ngwasuma ningeshapata code#
Sema lazima kuwe na sababu........ Itajulikana tu

Ova
 
Ingekuwa mimi ndio wewe ningekuwa na utamaduni wa kusoma thread kwa makini. angalia hiyo habari ilitolewa lini na huyo kafa lini!!!
halafu mkipata supp mnakilimbilia ku apply kumbe hujasoma swali vizuri unajibu unachojua sio ulichoulizwa!!!
Uliyoyaandika yanakuhusu wew kabisa.

Kwani hapo Mimi nimeshangaa nini
 
Saturday , 15th Dec , 2018

Msanii wa kundi la The Mafik anayejulikana kwa jina la Mbalamwezi, amekamatwa na jeshi la Polisi mkoa wa Kinondoni kwa tuhuma za wizi.

Tukio hilo limetokea hapo jana baada ya msanii huyo kumuibia dereva wa gari ya moja ya kampuni zinazotoa huduma za usafiri binafsi jijini Dar es salaam (Taxify), aliyejulikana kwa jina la Calvin.

Akisimulia tukio hilo Calvin amesema Mbalamwezi aliitisha usafiri akitumia simu ya mwenzake, lakini alipokuwa njiani alionekana kuwapigia simu watu kuomba hela kwani hakuwa na pesa ya kumlipa dereva, na ndipo alipochukua uamuzi wa kumuibia dereva baada ya kumfanya apoteze fahamu.

Meneja wa kundi la The Mafik aliyejitambulisha kwa jina la Kapasta amesema ni kweli kuna hilo tukio, lakini ndio yuko njiani akielekea kituo cha Polisi Oysterbay ambako msanii huyo amewekwa rumande ili ajue kinachoendelea.

East Africa Television ilifanya jitihada za kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Jumanne Muliro, lakini alijibu hawezi kuzungumza kwa wakati huo kwani alikuwa kwenye ziara ya Waziri Mkuu.

aisee... kumbe inawezekana chanzo ni wizi.
 
Bongo5 mjomba wake kaelezea kidogo ila chanzo bado mtihani... utata
 
Jamaa walichukua nafasi ya wakali kwanza. Napenda ile ile ngoma yao ya "niwaze" ft Ruby kuna vionjo fulani hataree sana!!
Alikuwa mgonjwa au ni ajali? Pole kwa ndugu jamaa, marafiki na mashabiki wake. Binafsi ndio nimemjua kupitia habari hizi ingawa kundi lake nimelisikia mara kadhaa.
 
Nimemsikia Mjomba wa marehemu anasema marehemu alikutwa amevuliwa nguo zote na madaktari wanasema alikanyagwa na gari maana utumbo ulikuwa nje wote na alisha haribika hivyo atazikwa kesho.
 
Hapana Mkuu hiyo taarifa ni ya Mwaka Jana,inaonyesha ni mtu wa Matukio ,Maana kuna utata wa kifo wengine wanasema kapigwa wengine wanasema kagongwa na gari....Ndio nimejaribu kuunganisha dot matukio yake ya nyuma.
Gsri ndiyo inagua nguo...za yule aliyegongwa?
 
Jamaa inaonekana yalimkuta makubwa kabla ya kufariki[emoji24][emoji24][emoji24]
 
awa wazee wa magunia ya mkaa inaelekea wako wengi sana hapa mjini.
 
Back
Top Bottom