Binti kasema vizuri tu.
Video ilikuwa private watu wakaimwaga.
Binti hajatunga uongo kukataa kwamba si yeye. Kakubali ni yeye. Hapa kaepuka kuongeza kosa la uongo. Kwa hili namoa heko. Kawa muwazi tu.
Mi binafsi nishamsamehe hata kama sijaona hiyo video na sioni cha kusamehe.
Binti mkristo. Kaomba msamaha mpaka kanisani kwake.
Hata kwenye sala ya bwana (nafuatilia sana maandiko matakatifu katika muktadha husika, kinyume na wengi wanavyoweza kufikiri) wakristo wameambiwa wasamehe kama na wao watakavyosamehewa, hivyo kutomsamehe mtu aliyeomba radhi ni kitu kibaya.
Halafu hawa mabinti wengine roho zao nyepesi mkiwashikia bango sana hamchelewi kusikia wamekunywa vidonge na kujitoa uhai.
Iwe fundisho kwa wengine.
Ila upande wa pili unasema binti katuma video mwenyewe ili kupata kick na msela ana mpaka voice notes.
Hapo lazima unuse ushuzi na kuona hawa watoto hawana akili nzuri vichwani.