Msanii Ray C azidiwa na Madawa ya Kulevya; asaidiwa na Polisi

Msanii Ray C azidiwa na Madawa ya Kulevya; asaidiwa na Polisi

Rehab panamuhusu alikua anamshauri chid sasa yeye ndio yamemkuta
 
Katika jambo la kushangaza ni kumsaidia Ray c wakati ashajichagulia maisha yake .... vema aongeze dozi hii ya sasa ndogo
 
Watanzania wenzangu tumejionea jinsi msanii MKUU wa muziki Ray C akihaha kuomba msaada wa watanzania wenzake kutokana Na madawa ya kulevya yalivyomdhuru.Msanii huyo Jana Jeshi la polisi lililazimika kumwokoa maeneo ya Kinondoni Manyanya.Msanii huyo wakati wa me akiwa anawika hapa nchini hakuwahi hata Siku moja kujitoa Kwa watanzania wenzake wenye shida mbalimbali au watoto yatima kuwatembelea Na kuwapa misaada.Lakini Leo yamemkuta anaomba asaidiwe.Nawasihi watanzania tunapokuwa tumepata tujaribu kuwasaidia wenzetu wenye shida tusijifanye sisi in malaika hatutapata shida on a Ray C tuliyekuwa tunasikia Leo Yuko
China, Leo yuko America.
 
REHEMA CHALAMILA (RAY C)

kama wewe ni mtu wakufatilia sanaa especially bongo flava music utakua unafahamu jinsi tunavyozidi kupoteza nyota wa muziki kwa madawa ya kulevya.
Ni takribani mwaka na zaidi tangia mwanadada Ray C atoke kusaidiwa na Rais mstaafu JK kutoka kutumia madawa ya kulevya lakini hivi sasa tumeona video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii sana ikimuonesha binti huyu akiwa karudi kule kule.



CHID BENZ

Kwa chid benz nako cinema ni hile hile japo adui yako ndio atakae kusaidia. Chid benz alikua na beef na kalapina baada yakupigana club maisha miaka ya nyuma baada ya chid benz kuvamia show ya kalapina, lakini leo hii huyu huyu kalapina ndio amepambana kumsaidia chid benz kama ndugu wa damu. Hongera kalapina kwa hilo nisipo kupongeza ntakua mchoyo wa fadhila.

YOUNG DEE
huyu msanii mie huwa namuona kama mtu mwenye kipaji cha pekee kutokana na kazi zake. Katika umri mdogo lakini ameweza kufanya collaboration na wasanii wenye majina na wakongwe lakini dogo kawatoa kimasomaso.
Mwenendo wake wa sasa kwa kweli sijaupenda na naomba kwa watu wake wa karibu pamoja na dulla wa planet bongo tumsaidie huyu dogo kabla mambo hayajawa tight hili tuonekane kama tulikua tunasubiri aharibikiwe hili tutafutilizie kick humo humo. Kama tunaweza kumsaidia sasa jaman hima hima let us stand against madawa ya kulevya to save our generation.

 
Kama hawaoni starehe nyingine zaidi ya madawa ya kulevya mi napata shida sana kuhisi hili
 
Hivi huyu dogo ni kweli kaanza huu upuuzi? kuishi sinza kweli unahitaji uwe na masters.
 
Unafki wengine bana..
Huna majukumu!??
 
unaposema wanamtandao unamaanisha watumiaji na wauzaji unga au ?
 
...si vema kumhukumu, haswa sisi tunaoamini ktk Kristo huwa tunasamehe na kuombea. Angeweza kuokoka anaweza kupona kabisa.
Wewe uliwahi kusikia TEJA anabebeka?,acha hizo bhaanaa,huyo Rehema Chalamila amechezea pesa zetu za kodi kumtibu,Mkwere badala ya kusaidia Mayatima akawa anagharamia hilo jiteja linalonuka Laana.
 
Back
Top Bottom