TANZIA Msanii wa Bongo Flava, Haitham Kim afariki dunia

TANZIA Msanii wa Bongo Flava, Haitham Kim afariki dunia


Mwimbaji wa Bongofleva na mwanachama wa JamiiForums, Haitham Kim amefariki dunia hospitali ya Temeke alipokuwa anapatiwa matibabu. Meneja wake amethibitisha.

Hivi karibuni Wasanii na Wadau wengine walianzisha kampeni ya kusaidia kuchangisha pesa kwa ajili ya matibabu yake.

Bryson ambaye ni Mume wa Marehemu alisema hali ya Haitham ilibadilika ghafla siku saba zilizopita akisumbuliwa na upumuaji ambapo ilianza kama homa ya kawaida lakini baadaye akawa anakosa pumzi hadi kupelekea kuwekewa mashine na kuchomwa sindano za kila siku zilizogharimu shilingi laki 7 kwa siku.
Mwenyezi Mungu amweke panapostahili
 
Matibabu ni zaidi ya Starehe mkuu, usiseme hivyo kabisa. Kumbuka kwenye Starehe unatumia wakati huo huo unaingiza. Unapopata maradhi huingizi kitu bali unatoa tu.
Hata wewe ukiumwa kufikia mwezi 1 tu maisha yako yanabadilika.

Tumemuona hapa Prof Jay, kama sio huruma ya Mama Samia ilikuwa anarudisha jezi mapema sana, alikosa pesa za matibabu ya uhakika na watu walichanga lkn mpka pale Rais alipotoa tangazo la kumgharamikia.

Ugonjwa sio starehe ndugu yangu. Usitukane watu wala kukashifu kisa amefariki na hakuwa na hela za matibabu, hadi anapatwa na umauti unajua alitumia kiasi gani kwa matibabu achilia mbali huduma zingine muhimu?

Tuache Dharau, sisi ni Binadamu tu. Pumzi yako isikufanye kuwaona waliotangulia mbele za haki kama wazembe.
Shida wasanii wanajisahau sana hapa Duniani,mtu km diva anasema Kwa mwezi matumizi yake y kawaida ni 10 Ina maana anaingiza Si chini ya million per day,anaishi nyumba analipa Dola 2500,halafu Wanaita watu masikini wanaishi stooo etc wakipata shida Sasa hv wanageuka omba omba,Ruge aliumwa hakuna mtanzania alimdhihaki hta Professa na wastars NAE hawakudhihakiwa hivi vidada viba nyodo Sanaa Ndo maana watu wanawadhihaki
 
Back
Top Bottom