Msekwa: Membe siyo mtu maalumu, afuate tu taratibu

Msekwa huyu huyu ambaye enzi zake Bunge lilikuwa kamati ya chama? Halafu mgombea urais alishindanishwa na kivuli!
Ameshapitwa na wakati huyu lakini haamini, halali!
Kivuli cha Membe kinawakosesha wengi usingizi.

Afadhali ya Bashiru ambaye jana (02/03/20) aliongea kwa umakini kidogo kuhusu hatma ya Membe (alijaribu kufanya damage control) kuliko tulivyowazoea. Na hapo ndipo ilipo tofauti kati ya kizazi cha Msekwa na kizazi kipya cha 'makada' wa CCM.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

"kuingia msituni kwa ufadhili wa mabeberu"

kukitokea hili... hao kina Msekwa sijui watakimbilia wapi yarabi?
mwenzao Gaddafi alikimbilia shimoni kama nyoka bado aliibuliwa na kuvutwa ndevu kinyama.

wacha tuendelee ku enjoy hii movie, steringi mkuu akiwa ni yule yule "mwamba wa pande za kusi"!!
 
Jambo la membe ni sawa na kusema

Huyu ni fisadi lakini hutaji huo ufisadi.

Huyu ni jambazi lakni hutaji alichofanya

Huyu ni mlevi lakini hutaji anacholewa

Huyu ni mtovu wa nidhamu,hutaji matendo ya huo utovu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Unatoa povu sana kama ulinufaika na membe sasa atapunguza matumizi kwako maana kupatab uraisi nje ya CCm ni ghalama kubwa au aanze biashara tukutane TRA achangie uchumi wa nchi, hata nyumbani kwako kuna utaratibu, kama mukeo mwisho kuingia usiku nyumbani ni saa mbili inabidi afate kanunu zako, ila wewe hata saa nane usiku unarudi, kwa hiyo destuli za CCM kama zilimshinda mapema angejiengua tu ili asipate kufukuzwa.
 
Msekwa, alipopelekewa shauri la mgogoro wa Musiba Vs Makamba, Kinana, alisema aachwe apumzike na kwamba wa kuyasemea hayo ni waliopo madarakani!
Sasa bado anapewa 'airtime' ya nini tena?
 
Hala
 

Metoa mawazo yake kama wengine ambavyo wangeweza kutoa.

Huyu mzee amezeeka, na ha anajitahidi kulinda penshini yake. Watu husema uzee ni busara, "lakini si kila mzee anabusara"
 
Mbona huyu Mzee ana hangaika sana kwani Membe kamwuuliza Utaratibu wa kufuata? Membe anaujua utaratibu sialikuwa ccm

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninachoshangaa ni kuwa Membe amefukuzwa na si mwana CCM tena sasa mbona wana CCM ndiyo wanaweweseka saaaana kuliko huyo aliyefukuzwa, tumechoka na huu upumbavu wenu, kama vipi mpigeni risasi mbona kwa Lissu mliweza?

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Msituni? Ataanzaje au ataingilia wapi msituni kwa mfano. Hii nchi sio DRC mbayo serikali imeshindwa kuthibiti ardhi yake! Hapa kila square inch ya nchi imehibitiwa tena tangu enzi za Mwalimu!
 
Sasa afuate taratibu gani maana hawamtaki. Kwani Seif na Oscar walifuata taratibu gani?
 
Eti linajifanya kuwa so special,Mara niguse ninuke,ameshaguswa wala harufu hatusikii

Sent using Jamii Forums mobile app
So far Membe ameonyesha kuwa ni icon iliyokuwa na upekee. Hajazungumza sana ila waliomfukuza ndo wanazungumza zaidi. Wanaccm wakikaaa kimya atapotea haraka zaidi kuliko wanavyozungumzia sana hili swala lake. Ameshafukuzwa, aachwe yeye ndo povu limtoke na si kinyume.
 

Oscar Kambona hakufukuzwa CCM, alikimbia nchi akiwa Waziri, Mwanachama na kada wa kitaifa wa CCM.

Sijui amefika umri gani lakini ni dhahiri Mzee Msekwa ameshaanza kupoteza kumbukumbu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…