Msela na Mbabe TAMISEMI walivyoichonganisha awamu ya tano na wananchi na wafanyakazi

NewPage

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2021
Posts
1,321
Reaction score
2,106
Mama Samia Suluhu Hassan ameshtuka mapema. Ninamsifu sana. Ukweli kabisa Msela Jafo hakuwa na impact kabisa katika awamu ya tano. Aliyafanya yale ambayo alifikiri yanampatanisha Rais wa Awamu ya Tano na Serikali na wananchi. Ona Msela huyu alivyoharibu kabisa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mwaka 2019.

Hili haliwezi sahaulika kamwe. Jaffo alikuwa akijiendea tu na anacheka cheka tu na wala hakuwa na uwezo wa kushauriana na Mbabe wa TAMISEMI Katibu Mkuu Engineer Nyamhanga. Huyu alikuwa anawasiliana direct na classmate mwenzio JPM - so hakuwa anatikiswa wala na Waziri wake. Nyamhanga ndiyo chanzo cha Wakurugenzi Wasimamia Uchaguzi 2020 kuiba kura na kununua Uchaguzi. Huyu alikuwa wakati wowote anaongea na JPM kwa simu na Mahera. Kwa sasa sijui kama ana ubavu huo.

Kibaya Zaidi hata sasa wafanyakazi wengi uhamisho ambao hupaswa kuidhinishwa naye umekwama pale. Watendaji wake wa chini wanaoshughulika na uhamisho wanakula rushwa kama mchwa - Nyamhanga mwenyewe kalundika barua kibao badala ya kuzisaini na kuwapa majibu waombaji ameshikilia tu. Yaani sijui binadamu tunajisikiaje kuchelewesha mambo ya watu. Niliomba uhamisho kutoka Dar-es-Salaam kwenda Mwanza kama Mwalimu nikamhudumie mzee wangu aliyekuwa anaumwa leo ni miaka mitatu hamna majibu wakati sehemu hizo zote walishanipitishia na mpaka mzazi wangu kipenzi akafariki dunia. Ukienda TAMISEMI eti unaambiwa Katibu Mkuu hajasaini barua zenu. Wenzao UTUMISHI ni hamna longolongo, unaomba uhamisho haujakubaliwa unajibiwa, hawa TAMISEMI kuna nini?

Samia pls hamia kwa Katibu Mkuu huyu uchuro aliyekuwa anafanya kazi kwa favour ya kuwa classmate na Jiwe. Hafai huyu msaidie faster, ili hata wananchi waone haki ikianza kushamiri kupitia TAMISEMI. Yaani ilikuwa ni bora mtu kwenda kwa Waziri Mkuu au kwa Rais mwenyewe kuliko kwenda TAMISEMI.

Tafadhali Mama Ummy Mwalimu hebu kaanza na hizo barua za idhini ya uhamisho za miaka kibao kazitoe au hakikisha basi waombaji wanajibiwa faster.

Updates:
Jana Tarehe 04 Aprili, 2021 wengi wamefurahi kuona Nyamhanga naye kaondoshwa TAMISEMI. Haijulikani atapangiwa wapi lakini ukweli ubabe wake na karma ya kuongoza mbinu za kuiba kura Mwaka 202o na kutibua Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 itaendelea kumfuata na hana la kujivunia. Na tena sijui anajisikiaje kuondoka pale wakati lundo la barua za uhamisho zikiwa mezani kwake.
 
Jiwe watu wake aliwadekeza sana. Unamfahamu Engineer Nyamhanga lakini?
Mzee unaishi sayari gani wewee, jiwe alitumbua adi marafiki zake na urafiki ukaisha, mtoto wa dada ake aliye teuliwa kule kawe, akala kichwa . Nilikuwa simpendi jiwe lakini baadhi ya uwe da wazimu wake ulikuwa na manufaa kwa nchi hii!!!
 
Huyo mtoto wa dadake aliteuliwa na nani? Je kwa sasa yupo wapi na wakati anateuliwa competency yake na yako unailinganishaje? Further to that unaweza kweli mlinganisha aliyekuwa Katibu Mkuu Fedha Mkenda na Doto James wa sasa? Usitetee nepotism kama sio mnufaika ndugu!
 
Acha utoto, lini Mkenda alikuwa Katibu Mkuu wa wizara ya fedha ?
 
Jafo ni mchapakazi hakuwa anakurupuka katika maamuzi yake. Amesimamia ujenzi wa madarasa nchi mzima, vituo vya afya, zahanati na hospital za wilaya stand na vituo vya mabasi,miradi ya maji,n.k katika mazingira magumu ya fedha za halmashauri kuwa chini ya hazina/serikali kuu. Kama sio ubunifu wake wa kutumia Force account kufanikisha miradi hii, halmashauri nyingine zingeshindwa kukamilisha miradi kutokana na urasimu wa kupata fedha toka hazina. Ni pontetional to higher office Madame SSH anajua hill na alichofanya ni nyundo. Huwezi mfananisha Jafo na mawaziri uchuro kama Mwigulu, atang'ara tu hata wizara anayoenda
 
Hujui kitu? Jafo alikuwa anasafiri safari tu na maneno meeeeeeeeengiiiiiii kama Mzaramo!
 
Mama Samia Suluhu Hassan ameshtuka mapema. Ninamsifu sana. Ukweli kabisa Msela Jafo hakuwa na impact kabisa katika awamu ya tano. Aliyafanya yale ambayo alifikiri yanampatanisha Rais wa Awamu ya Tano na Serikali na wananchi. Ona Msela huyu alivyoharibu kabisa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mwaka 2019.

Hili haliwezi sahaulika kamwe. Jaffo alikuwa akijiendea tu na anacheka cheka tu na wala hakuwa na uwezo wa kushauriana na Mbabe wa TAMISEMI Katibu Mkuu Engineer Nyamhanga. Huyu alikuwa anawasiliana direct na classmate mwenzio JPM - so hakuwa anatikiswa wala na Waziri wake. Nyamhanga ndiyo chanzo cha Wakurugenzi Wasimamia Uchaguzi 2020 kuiba kura na kununua Uchaguzi. Huyu alikuwa wakati wowote anaongea na JPM kwa simu na Mahera. Kwa sasa sijui kama ana ubavu huo.

Kibaya Zaidi hata sasa wafanyakazi wengi uhamisho ambao hupaswa kuidhinishwa naye umekwama pale. Watendaji wake wa chini wanaoshughulika na uhamisho wanakula rushwa kama mchwa - Nyamhanga mwenyewe kalundika barua kibao badala ya kuzisaini na kuwapa majibu waombaji ameshikilia tu. Yaani sijui binadamu tunajisikiaje kuchelewesha mambo ya watu. Niliomba uhamisho kutoka Dar-es-Salaam kwenda Mwanza kama Mwalimu nikamhudumie mzee wangu aliyekuwa anaumwa leo ni miaka mitatu hamna majibu wakati sehemu hizo zote walishanipitishia na mpaka mzazi wangu kipenzi akafariki dunia. Ukienda TAMISEMI eti unaambiwa Katibu Mkuu hajasaini barua zenu. Wenzao UTUMISHI ni hamna longolongo, unaomba uhamisho haujakubaliwa unajibiwa, hawa TAMISEMI kuna nini?

Samia pls hamia kwa Katibu Mkuu huyu uchuro aliyekuwa anafanya kazi kwa favour ya kuwa classmate na Jiwe. Hafai huyu msaidie faster, ili hata wananchi waone haki ikianza kushamiri kupitia TAMISEMI. Yaani ilikuwa ni bora mtu kwenda kwa Waziri Mkuu au kwa Rais mwenyewe kuliko kwenda TAMISEMI.

Tafadhali Mama Ummy Mwalimu hebu kaanza na hizo barua za idhini ya uhamisho za miaka kibao kazitoe au hakikisha basi waombaji wanajibiwa faster.
Huyu jumanne wanakula kichwa wala usijali
 
Back
Top Bottom