Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 18,653
- 31,010
Kuwapatanisha CCM na wapinzani?Nina uhakika tena wa 100% kabisa kuwa hii juhudi yako ambayo sioni haya wala aibu kuiita ni ya 'Kinafiki' ya 'Kuwapatanisha' akina Emanuel Mbasha na Adam Mchomvu tena ukiwa 'Mubashara' kabisa katika Kipindi cha XXL cha Clouds FM leo ungeitumia katika 'Kumpatananisha' Bosi wako Mkuu (Rais Magufuli) na Wapinzani huenda Siasa na Demokrasia ya Tanzania ingekuwa ya Kuigwa.
Halafu sikuona haja sana Mtu kama Wewe 'Kuhangaika' na hao huku ukitakiwa 'Kumsaidia' mambo Makubwa na Muhimu Bosi wako (Rais).
Msemaji mkuu hana hiyo karama wala mvuto wa kisiasa kufanya hivyo.
Mtu aliyemeza casseti ya shukrani na kuabudu kwa aliyemteua, hana kuwiwa na wajibu wa upatanisho huo.Maana kuwepo kwake Kunatoka a na aliye mteua.
Yeye ni kukandamiza mwanzo mpaka mwisho wapinzani.
Hizo kazi wanaweza watu wenye upeo mkubwa kama Jaji Warioba.