Ni hapo ninapo kuwa na mashaka ya elimu zenu! Yaani kuona kama mnachukulia mtu mwenye PhD atakuwa na uelewa wa kila kitu!
Nikupe mfano wa Dr. fulani yeye amebobea kwenye buibui (spiders) - yaani tofauti, aina, zenye sumu, makazi yao n. k. Lakini hana interest na mambo ya sheria! Lakini akija kwenye fani yake ya buibui ni kiboko. Sasa nyinyi mtaanza kumuona huyo hafai, na wa PhD wote hawafai kwa sababu mmetafautiana kiitikadi!
Mnaposema maCCM ovyo na wao wanaposema CHADEMA nyumbu, hiyo inaeleweka na kipimo kiko sawa na ni kile kile. Lakini unapo ongelea PhD ambazo hazifanani na ni speciality ya kitu kidogo katika taaluma kubwa hapo nawashangaa! Naona kama uelewa wa hicho kitu kinachoitwa PhD hakijulikani kwa wengi!
Nikitumia mifano yako - Tundu Lissu siyo kwamba anawazidi wote wenye PhD! Kwa mfano wangu - Huyu mwenye PhD ya buibui hazidiwi na Lissu kwenye fani yake. Dr. Bashiru hazidiwi na Lissu kwenye elimu ya siasa na vile vile Bashiru hamzidi Lissu kwenye sheria.
Tukija kwa Mnyika - Fani ya uchumi ni kubwa na unaweza ukakuta hao unaowasema wenye PhD ya uchumu, ni katika kipengele kimoja kidogo (e. g biashara ndogo ndogo) wakati Mnyika ana general understanding ya uchumi tu - hivyo ni vitu tofauti!
Mwisho niseme kuwa msichanganye mambo ya taaluma na siasa! Kumbuka ili uwe mwanasiasa, lazima ujue kusoma na kuandika - na kutumia lugha ya Kiswahili/kiingereza.