Msemaji wa JWTZ kuteuliwa kwenye NEC ya CCM, hii imekaaje?

kama kaacha,mbona haitwi "mstaafu" au atumie jina lisilo na asili ya jeshI,atumie majina yake tu?

halafu hii ya kurundika wanajeshi,je ikitokea ccm imeshindwa kwenye uchaguzi,hawa wanajeshi wataelewa? au wanachonganishwa na wananchi?
Ha ha ha du! Ila kweli mkuu umenena hawa jamaa hawatoelewa kitu[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]
 

Mbona ume quote kitu ambacho wewe mwenyewe hujakielewa?
 
Siku unayoteuliwa unaacha jeshi huwi mwanajeshi na unashika madaraka siku hiyo hiyo kama ambavyo lowasa alivyofanya.Siku alipoteuliwa na CHADEMA kuwa mgombea siku hiyo hiyo aliacha CCM na kuwa mgombea uraisi
Unamaana huyo mteule alikuwa na Kadi ya Chama?
 
Kwa hiyo uteuzi wake uliegemea kwenye lugha ya mawasiliano sio? Ingekuwa lugha ya mawasiliano ndiyo kigezo cha uteuzi hivi leo ungemteua mtu anayozungumza broken english?
 
Naona kwa ufahamu wangu Mkuu yuko juu ya katiba.Hata vyama Sasa ruhsa kufanya mikutano yake mikuu ikulu alimradi ajenda zao zitambuliwe kwanza.
 
Siku unayoteuliwa unaacha jeshi huwi mwanajeshi na unashika madaraka siku hiyo hiyo kama ambavyo lowasa alivyofanya.Siku alipoteuliwa na CHADEMA kuwa mgombea siku hiyo hiyo aliacha CCM na kuwa mgombea uraisi
Lowasa anakukera sana kila kitu mpaka utolee mfano kwake, kweni ni mtu wa muhimu sanaaaaaaaaaa kwako YEHODAYA
 
Swali ni kuhusu uteuzi bro, kwa sababu mtu hawezi kuteuliwa tena kwenye nafasi kama ya msemaji kama sio mwanachama wa muda mrefu
Kuna sehemu ya katiba inayomkataza askari kuwa mwanachama wa chama cha siasa ?
 
Umesema wakati tukiwa mfumo wa chama kimoja, sasa hivi tuna mfumo wa vyama vingi.
 
Hili jambo linaumiza sana kama watetezi wa RAIA wanajiunga na siasa nini hatima ya nchi yangu? Kwanini tunabaka demokrasia nia yao nikuona tukichafua amani iliyodumu kwa MUDA mrefu kwa maslahi yao binafsi au,? Nimesikitishwa sana
 
Taratibu tunarudi enzi za Ujamaa ......... Jenerali Ulimwengu nafikiri yeye aliona mapema zaidi!!
 
Siku unayoteuliwa unaacha jeshi huwi mwanajeshi na unashika madaraka siku hiyo hiyo kama ambavyo lowasa alivyofanya.Siku alipoteuliwa na CHADEMA kuwa mgombea siku hiyo hiyo aliacha CCM na kuwa mgombea uraisi
Sio lazima ujibu ujinga,katiba ya CCM inataka uwe mwanachama miaka miwili ili upate wadhifa huo
Sasa mtu aliyelewa madaraka katiba kwake ni karatasi ya chooni tuu
 
Hivi watu kama nyie mnaishi dunia ya wapi?
Afu utakuta una elim ya chuo kikuu!!
 
Awamu hii tumeamua kwa dhati kuikanyaga-kanyaga katiba....
"Mtawala yuko juu ya sheria za nchi"
Nani anajali!....
 

Upo sawasawa lakini nafikiri wewe na mleta mada mnachanganya katiba ya CCM na katiba ya Tanzania.

Katiba ya CCM inamruhusu mtu yoyote kuwa mwanachama bila kujali anakotoka.

Na Katiba ya Tanzania kupitia ibara ya 5 kifungu (1) inawaruhusu raia wa Tanzania kupiga kura.

Ila mleta mada angefafanua kuhusu vifungu alivyoweka hapo juu vinavyokataza wanajeshi kujiunga na vyama vya siasa huku wakiwa na haki ya kupiga kura- yaani wawe wametimiza umri wa kupiga kura.
 
Mi Naona katiba imekosewa,irekebishwe😉
Shangaa pamoja nami,mwenyekiti
wa ulinzi na usalama wa mkoa/wilaya
ni mkuu wa mkoa/wilaya ambaye ni kada wa chama

Kicheo huyu yupo juu ya RPC
au kiongozi wa polisi aliyepo anayeongoza kwenye eneo lake
kwa maneno mengine anamtuma kazi
kiongozi wapolisi aliyepo chini ya eneo lake.
Sasa kwa nini katiba iwazuie wanajeshi au polisi
kuwa wanasiasa, au mimi ndo sielewi?

Kama tunataka kutenda haki,kiongozi
au m/kiti wa ulinzi na usalama wa mkoa/wilaya
awe kiongozi wa polisi wa mkoa/wilaya husika
hapo tunaweza kusema,vyombo vya ulinzi na usalama
vipo mbali na siasa,vingenevyo katiba irekebishwe
ili kuondoa utata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…