Msemaji wa JWTZ kuteuliwa kwenye NEC ya CCM, hii imekaaje?

Msemaji wa JWTZ kuteuliwa kwenye NEC ya CCM, hii imekaaje?

sialisemaga! japokua nchi ina mihimili mitatu ila yeye wakwake umezama chini zaidi, yeye ndio mtoa fedha..atakalo linakua! tuvumilie tu tumalizie kusoma namba zakirumi
 
Siku unayoteuliwa unaacha jeshi huwi mwanajeshi na unashika madaraka siku hiyo hiyo kama ambavyo lowasa alivyofanya.Siku alipoteuliwa na CHADEMA kuwa mgombea siku hiyo hiyo aliacha CCM na kuwa mgombea uraisi
kama siku zote mngekuwa mnajibu hoja kwa busara na kwa kueleweka kama ulivyojibu vizuri bila kutukana.

Jukwaa lingekuwa bora sana, na hata yanayompata ndugu Max yasinge kuwepo.

Ni bora tukajifunza siasa safi siasa rafiki na siyo siasa za chuki na kutukanana kutunga mambo ya uzushi kwa wengine.

Hapa naongelea pande zote mbili tujifunze siasa za kistaarabu siasa za hoja na siyo siasa za kutukanana na kuvunjiana heshima.
 
Mi si mwanasheria lakini nafahamu Tanzania ina wanasheria na taasisi nyingi za sheria, kwanin hawa viongozi wanapotoka nje ya katiba ambayo ni sheria mama (kwa ufahamu wangu) na wao wanaishia kulalamika tu kwenye vyombo vya habari na mitandaoni na mahakama zipo. Wajue ukimya wao wa kisheria ndo unazidi kutupeleka kwenye udikteta uliokidhiri. Tunapokwenda msemaji wa chama atawachapa vikobo majudge na bado watapigiwa makofi. Wake up guys [HASHTAG]#wanasheria[/HASHTAG]
 
Mkuu alisema anapenda kuwapa wanajeshi nafasi zaidi kwa sababu jeshini wanafunzwa nidham hivyo anavyowateua anajua watadumisha nidham maofisini pia alisema anapenda kuwateua wajeda kwa sababu ukimteua askari kwanza atarudisha shukran ya saluti lakin ukimteua raia wa kawaida hatokupa shukran yoyote sana sana atawadha akiingia ofisini apige madili ya fasta fasta anunue kiwanja ajenge mijumba tu.
 
Mtukufu wetu yuko juu ya kila kitu na hata akiamua kusema watz wote ni vilaza tutampigia makofi na kushangilia
Lkn hakuanza yeye; JK alimteua Kanali Ndomba kuwa RC Arusha na baada ya miaka michache akamrudisha JWTZ kuwa Mnadhimu Mkuu kabla ya kustaafu mwaka jana. Inajulikana wazi hiyo nafasi ni ya Kisiasa na Col. Ndomba alikuwa bado ndani ya ajira ya JWTZ!

VV
 
Tumia akili, jeshi limefungwa kisheria lkn lowassa hajafungwa kisheria. Huu ndio tunaoita kwa kingereza GRAFT CORRUPTION. Taasisi inahongwa ili itoe upendeleo.
Limefungwa kisheria pale unapotaka kuvaa kofia mbili kwa wakati mmoja ila ukipata nafasi ya kisiasa unaacha jeshi mara moja na kwenda kwenye siasa
 
Siku unayoteuliwa unaacha jeshi huwi mwanajeshi na unashika madaraka siku hiyo hiyo kama ambavyo lowasa alivyofanya.Siku alipoteuliwa na CHADEMA kuwa mgombea siku hiyo hiyo aliacha CCM na kuwa mgombea uraisi
Kwa hiyo ameteuliwa akiwa si mwanachama wa CCM?
 
nina harufu ya damu kutapakaa 2020 kwani kijani hawatakubali kushindwa, na zaidi itabidi njugu zisambazwe kwa raia wasio na hatia ili tu wabaki madarakani, tuandae makaburi, kwanza watapoteza pesa nyingi sana kuliko walizopoteza 2015, na watakuwa wako juu ya sheria, kama walinzi wetu nao wanaingizwa kwenye siasa, mark my words
Magufuli anashinda kwa kishindo Hata nzi hafi 2020 uchaguzi ushaisha mbona tunasubiri kuapishwa kwa magufuli tu?
 
Lkn hakuanza yeye; JK alimteua Kanali Ndomba kuwa RC Arusha na baada ya miaka michache akamrudisha JWTZ kuwa Mnadhimu Mkuu kabla ya kustaafu mwaka jana. Inajulikana wazi hiyo nafasi ni ya Kisiasa na Col. Ndomba alikuwa bado ndani ya ajira ya JWTZ!

VV
Ccm wanatumia ubabe sana, haramu haihalaliswi na haramu
 
HAYA NI MAAJABU YA KARNE....
mjeshi anaruhusiwa kuwa na kadi ya chama??
 
Lkn hakuanza yeye; JK alimteua Kanali Ndomba kuwa RC Arusha na baada ya miaka michache akamrudisha JWTZ kuwa Mnadhimu Mkuu kabla ya kustaafu mwaka jana. Inajulikana wazi hiyo nafasi ni ya Kisiasa na Col. Ndomba alikuwa bado ndani ya ajira ya JWTZ!

VV
Hata sasa hivi wapo kibao ni wakuu wa wilaya kule Kigoma na Bado ni waajiriwa wa jeshi tatizo RAIA wengi magumashi uzalendo hakuna sasa hizo nafasi bora amewapa wazalendo wa nchi hii kuliko hawa RAIA( kifaa kinachomika baharini kwenye meli kujiokoa)
 
Mtukufu wetu yuko juu ya kila kitu na hata akiamua kusema watz wote ni vilaza tutampigia makofi na kushangilia
Muheshimiwa anataka kuingiza nidhamu ya kijeshi kwenye chama, ni transformation anafanya!!
 
Limefungwa kisheria pale unapotaka kuvaa kofia mbili kwa wakati mmoja ila ukipata nafasi ya kisiasa unaacha jeshi mara moja na kwenda kwenye siasa
Ndio maana tunauliza toka lini alianza kuwa mwanachama wa ccm? Kwa kazi gani aliyoifanyia ccm hadi ikamuona kuwa sasa anafaa?
Kwa kifupi ni hivi alikua ccm kitambo jambo ambalo ni kinyume cha sheria, na kuna kitu ameifanyia ccm ndio maana anapewa zawadi. Hasahasa wizi wa kura na kuwatisha wanajeshi waipigie kura ccm. Lkn yanamwisho
 
Nimegundua si kosa lako, tatizo lako unataka kuonyesha wana JF kuwa unajua lakini hujui chochote. Acha tukukumbushe-wakati tukiwa na chama kimoja asilmia kubwa ya wafanya kazi wote na wafanyabiashara walikuwa wanachama wa ccm, majeshi yote walikuwa wanachama wa ccm na siasa ilifundishwa hadi majeshini, na ndo maana tokea nyakati hizo wanajeshi waliteuliwa katika nyadhifa mbalimbali mfano-Mh. Jakaya Kikwete, Mh.Kinana na wengine wengi-si ajabu hicho kinachofanyika
umeshasema ilikuwa enzi za chama kimoja..........................
 
Kwani katiba ya Chadema inasemaje, mwanachama mpya lazima amalize miaka 2, bila kupewa wadhiwa wowote, lakini lowasa aliingia asubuhi jioni mgombea urais mbona hili hamkuhoji
hoja c uanachama mpya hoja ni aunajeshi wake mbn nyie watu ni wazito kuelewa!
 
Siku unayoteuliwa unaacha jeshi huwi mwanajeshi na unashika madaraka siku hiyo hiyo kama ambavyo lowasa alivyofanya.Siku alipoteuliwa na CHADEMA kuwa mgombea siku hiyo hiyo aliacha CCM na kuwa mgombea uraisi
Acha kutudanganya...!kumbuka huyu kateuliwa ina maana aliye mteua anajua fika kuwa huyu Ni mwanajeshi na mteuliwa hakujua kama atateuliwa ili astaafu jeshi alafu ateuliwa kuwa kiongozi wa chama cha siasa....!sasa unapotuambia lzm astaafu ndio awe kiongozi wa chama cha siasa unamaanisha nini.....?
 
Hoja si uteuzi wake tu,alianza lini kuwa mwanachama wa Chama cha mapinduzi huku akiwa mwanajeshi?

Kaanza kuwa mwanachama siku hiyo hiyo aliyoteuliwa. Kabla hakuwa mwanachama wa chama chochote

Yeye kateuliwa kaacha jeshi kachukua kadi kaanza kazi. Ni sawa na lowasa alihama CCM siku hiyo hiyo akachukua kadi ya Chadema na akawa mgombea urais
 
Back
Top Bottom