Msemaji wa JWTZ kuteuliwa kwenye NEC ya CCM, hii imekaaje?

Msemaji wa JWTZ kuteuliwa kwenye NEC ya CCM, hii imekaaje?

Kuna watu hawajui kwanini baada ya mfumo wa vyama vingi baadhi ya taasisi kama jeshi ziliondolewa kujihusisha na mambo ya siasa sasa wanaweza kujiona salama sababu wanatumia vyombo kama majeshi kuwalinda ila itakapotokea wanajeshi wakageukia upande wa pili ndio watajua kama waliofanya hivyo mtazamo wao ulikuwa wa mbali kiasi ganik
 
Hiyo quotation hapo chini sijui nilimnukuu nani vileee .
hatari sana
 
Kaanza kuwa mwanachama siku hiyo hiyo aliyoteuliwa. Kabla hakuwa mwanachama wa chama chochote

Yeye kateuliwa kaacha jeshi kachukua kadi kaanza kazi. Ni sawa na lowasa alihama CCM siku hiyo hiyo akachukua kadi ya Chadema na akawa mgombea urais
Kwani Lowassa alikuwa mwanajeshi wkt anahamia Chadema.....?issue apa ni mwanajeshi kuteuliwa kuwa kiongozi wa chama cha siasa.
 
Shida kubwa ya Watanzania tuna tabia ya kusahau.marehemu Mosses Nauye, marehemu Captain Komba, Canali Abdahaman Kinana wote hawa walitumikia Jeshi still walitumikia chama so hakuna kitu kipya.Jamani can we use our energy to participate in the productive sectors and so widen the tax base of our Nation than continue with this kind of issues
 
kuna mhimili mmoja mizizi yake imekwenda chini zaidi ya mihimili mingine wacha waisome namba eeeh
 
Ni kada wa muda ndyo maana kabla ya usemaji wa jeshi alikuwa mkuu wa wilaya ya mlele
 
Huyo Lubinga si ndo alisema Ukatili hauepukiki si ndio??? Kipindi kile Kifaru cha jeshi kusemekana kimeibiwa???
 
Trend ya Magufuli na wanajeshi inaashiria maandalizi fulani. Huwezi kujua kwa hakika ni nini ila sio mambo mema.

Vijana wa ccm wanaoshabikia haya huku wakiwa na ndoto za kufanya siasa ndani ya demokrasia wajitafakari sana.
Huyu hana tofauti na Yahya Jammeh. Ni suala la muda tu
 
Police ni CCM
MAHAMAKA NI CCM
MGAMBO CCM
WAKUU WA WILAYA NA MIKOA NI CCM
 
Unakimbia mwendo wakati huna break, what do you expect
 
Kumekuwa na mitazamo mingi, thread nyingi zikisifisia na zingine zikihoji uhalali wa CCM kumteua Kanali wa Jeshi kuwa Mtumishi wa chama, Namimi nimeona nitoe maoni yangu kuhusu jambo hili ikienda sambamba na utoaji wa ufafanuzi wa baadhi ya mambo…..

HISTORIA YA JESHI LA JWTZ

Baada ya Uhuru, 1961, Tanganyika ilirithi jeshi la kikoloni la Uingereza lilojulikana kama Kings African Rifles ingawa Tanganyika ilibadili jina la Jeshi hilo na kuwa Tangayika Rifles (TR). Pamoja na kubadilika jina Tanganyika Rifles ilikuwa na muundo sawa na Kings African Rifles (KAR). Maafisa wenye mamlaka bado walikuwa Waingereza, pamoja na Waafrika watano waliopandishwa cheo wakati wa uhuru na kupokea mafunzo katika vyuo vya kijeshi vya Kiingereza. Afisa mkuu alikuwa Brigedia Jenerali Patrick Sholto Douglas.

UASI WA TANGANYIKA RIFLES (TR)

Tarehe 20 Januari 1964, wakati wa usiku, kikosi cha kwanza cha TR kwenye kambi la Colito Barracks mjini Dar es Salaam kiliasi na kujipatia silaha kutoka kwenye ghala la jeshi. Maafisa Waingereza walikamatwa na kufungwa lakini mkuu Douglas aliweza kujificha. Waasi walivamia kituo cha redio, uwanja wa ndege, ikulu na ofisi ya posta na simu. Maafisa Waingereza na Waafrika wasioshiriki na waasi walisafirishwa nchini Kenya. Rais Nyerere alienda mafichoni katika kanisa moja la kikatoliki ng'ambo ya bandari(kigamboni) akamwachia waziri Oskar Kambona kazi ya kuwasiliana na wanajeshi.

Madai ya wanajeshi yalikuwa kuachishwa kwa maafisa Waingereza na kupandishwa kwa mishahara. Siku za kwanza ya mgomo wa jeshi ilifuatwa na vipindi vya fujo mjini vilivyobadilika na vipindi vya kimya, mashambulizi dhidi ya maduka ya Wahindi na kukamatwa kwa Wazungu wachache. Hata mbalozi wa Uingereza alikamatwa kwa kipindi kifupi.

Tarehe 24 Januari serikali ya Tanzania iliomba rasmi Uingereza kuingia kati na kuzimisha uasi. Asubuhi ya 25 Januari kikosi kidogo cha wanajeshi wa Kiingereza waliondoka kwenye meli iliyokwepo karibu na Dar es Salaam kwa njia ya helikopta. Walivamia kambi la Colito barracks na jenerali Douglas alidai kwa kipazia sauti wanajeshi wajisalimishe. Mwanzoni walikataa lakini baada ya mashambulio mafupi walio wengi walijisalimisha wengine wakakimbia. Viongozi walikamatwa, na pia askari wa Dodoma na Nachingwea waliowahi kujiunga na uasi walijisalimisha bila upinzani kwa askari Waingereza wachache.

Wakazi wengine wa Daressalaam walikuwa na hofu ya kwamba Uingereza ulikuwa umerudi ili kurudisha ukoloni lakini baada ya kusita masaa machache Nyerere alieleza kwa njia ya redio ya kwamba kuingilia kwa Uingereza ulifuata ombi la serikali yake. Askari Waingereza waliondoka kwenye Aprili 1964 na nafasi yao ilichukuliwa na kikosi kutoka Nigeria iliyofika kwa niaba ya Umoja wa Afrika kufuatana na ombi la serikali ya Tanganyika


UUNDWAJI WA JESHI JIPYA

Jeshi jipya lilijengwa kwa kuajiri hasa wanachama wa Umoja Wa Vijana wa TANU. Jeshi hili jipya liliwekwa chini ya usimamizi ya chama cha TANU (baadaye CCM) kwa kufuata mtindo wa nchi kama Urusi na China. Kamanda wa kwanza alikuwa Mrisho Sarakikya aliyewahi kusimama upande wa serikali wakati wa uasi akapandishwa cheo kutoka luteni hadi kanali, baadaye kuwa jenerali. Na hapo ndipo Jeshi likabadilishwa jina toka Tanganyika Rifles (TR) na kuwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),September, 1964.

MSIMAMO WA KATIBA JUU YA WANAJESHI NA VYAMA VYA SIASA

Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) ibara ya 147(3) imeweka marufuku kwa mwanajeshi yeyote kujiunga na chama chohote cha siasa na imempa haki ya kupiga kura, hii inafuatia mabadiliko ya katiba yaliyofanywa mwaka 1992 chini ya sheria ya 1992 Na.4 ib. 36.



COL. NGEMELA ESLOM LUBINGA NI NANI??

Kwasasa Col Ngemela Eslom Lubinga ni Katibu mteule wa NEC Siasa na Uhusiano wa kimataifa( CCM). Col Ngemela alishawahi kuteuliwa na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kuwa mkuu wa wilaya ya Mlele mara baada ya kustaafu utumishi wake katika Jeshi la JWTZ. Ngemela aliachwa kwenye orodha ya Madc waliotangazwa February 19, 2015, Baadae akarudi jeshini kwa mkataba wa mwaka mmoja ulioisha November, 2016.


VITU VYA KUZINGATIA

· Ngemela alijiunga na jeshi la JWTZ kabla ya 1992

· Ngemela alistaafu jeshi kabla ya 2015

· Ngemela alshawahi kuhudumu kama mkuu wa wilaya ya Mlele mara baada ya kustaafu kuwa mtumishi wa Jeshi.
 
Katiba ina maana tu endapo itaheshimiwa, itahifadhiwa, itatetewa na kutekelezwa! Vinginevyo ni ubatili!
 
Siku unayoteuliwa unaacha jeshi huwi mwanajeshi na unashika madaraka siku hiyo hiyo kama ambavyo lowasa alivyofanya.Siku alipoteuliwa na CHADEMA kuwa mgombea siku hiyo hiyo aliacha CCM na kuwa mgombea uraisi

Ulimsikia Nnape wakati akimtangaza,alisema alikuwa mwanajeshi kisha akawa mkuu wa wilaya(siasa) baadae akarudishwa tena jeshini na sasa karudishwa tena nec(siasa),sasa ewe mjuzi sana nipe uhalali wa hii movement kwa mujibu wa Nnape jeshi-siasa-jeshi-siasa..

Pia kama ukiteuliwa(nafasi za kisiasa) unaachia ngazi katika jeshi ilikuaje akarudi tena jeshini(nukuu maelezo ya NNape akimtangaza,hivyo vifungu tajwa hapo juu vya katiba pia jinukuu mwenyewe kwenye quote )?
 
Kaanza kuwa mwanachama siku hiyo hiyo aliyoteuliwa. Kabla hakuwa mwanachama wa chama chochote

Yeye kateuliwa kaacha jeshi kachukua kadi kaanza kazi. Ni sawa na lowasa alihama CCM siku hiyo hiyo akachukua kadi ya Chadema na akawa mgombea urais
Unaleta ushabiki wakati hata haujui chochote,unajua kabla ya hapo ashashika wazifa gani wa kisiasa?
 
Kama kastaafu HAINA shida
Kama kateuliwa akiwa bado mtumishi wa JW ni upuuzi ulio pitiliza
Mnao fahamu haya,Je Kanali Lubinga kastaafu JW?
 
Haya mazinga hombwe lazima uwe mtu wa aina fulani kuyaelewa na kuyakubali. Kastaafu, akawa DC (hii nafasi kama huna kadi hupewi), karudi tena jeshini (nafasi ya juu)-akiwa mwanachama hata kama ni mwanachama mfu lakini ni mwanachama sasa kateuliwa tena huko CCM watasema sasa ni mwanachama hai. Kuna mmoja alisema hii nchi ni ya serikali by extension serikali ni ya CCM hivyo hii nchi ni ya CCM wanaweza kutenda watakavyo.
 
Mwl Nyerere aliwahi kunukuliwa akisema hivi , " HATA KAMA TUTACHAGUA ASIYEAMINI MUNGU , TUTATAFUTA NAMNA YA KUMUAPISHA , NA NI LAZIMA AAPE , KWAMBA ATAILINDA NA KUITETEA KATIBA YA TANZANIA "

MYTAKE - Kusigina katiba ya nchi ni kosa lisilosameheka milele .
 
Back
Top Bottom