Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

Weka siasa pembeni. Mtu yyte anayesaliti nchi yake na kushabikia makampuni ya nje,huyo ni msaliti na adhabu yake inafahamika.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ivi tuseme kama utaratibu ungelikua unafuatwa vzr katika mikataba hata mtu angeshabikia makampuni ya nje ingeleta shida gani kwa taifa au labda niulize maswali kidogo
1 aliyetangaza tenda ni nani?
2 aliyesaini mikataba na haya makampuni ni nani?
3 je alisaini kwa makubaliano yapi?
4 je aliyevunja mikataba na haya makampuni ni nan
5 je kipindi anasaini mikataba alikua kashikiwa bunduki
6 je kwenye maswali yangu hapo juu kuna sehemu lisu alihusika?

Nikipata majibu ya hapo juu nami nahic ndo naweza kupata wa kumraum
7 nani anapaswa kuraumiwa?

sent from makinikia
 
Awe na ufahamu na aache unafiki. Ndege imeshikiliwa kwakuwa kwa sababu tunadaiwa na kampuni ya ujenzi ya Canada $ 38.7 milioni kwa kusitisha mkataba kinyume cha sheria. Hayo yalifanywa na Magufuli akiwa Waziri wa Ujenzi 2009.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sidhan kama chama ndo kimesababisha hii hasara..ko kama waziri alisababisha hii hasara na waziri ni mwajiliwa wa serikali haina budi serikali kulipa hilo deni..ndo mana mmeambiwa hili swala litamalizwa kidiplomasia nadhan mengine tuendelee kujenga nchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nani anamwajibisha aloletaa majanga haya ili ajifunze asirudie tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nani anamwajibisha aloletaa majanga haya ili ajifunze asirudie tena

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu nadhan majanga yashafanyika mengi sana katika serikali zilizopita ko hili ni mojawapo kwa hiyo sababu mweshimiwa rais amesema lazma yarekebishwe ko hakuna budi hata hili kuwa moja wapo ya marekebisho na kukubal makosa ya serikali zilizopita na kuangalia tunalifanyia nini taifa kwa kupitia serikali hii kwa manufaa ya kizazi kijacho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesoma kwa masikitiko makubwa michango na lawama zinazoelekezwa na baadhi ya wachangiaji kwenye mitndao ya kijamii kwa mwanasiasa T. Lissu. Nadiriki kuwaita wapumbavu kwani wanajifichajificha bila kueleza uhalisia.

Najiuliza hivi lissu ndo nani had Iakwamishe ndege yetu?
Ni kwa nini makosa yanayofanywa na mtu flani mzigo abebeshwe lissu?

Ni dhahiri tumekuwa na kizazi cha kinafiki sana sana. Hakitaki kusema ukweli. Wanaona mh Rais akikosea hapaswi kukosolewa. Hawajui katika kukosoa na kusema ukweli ndio kuijenga Tanzania njema ya kesho. Hili lote ni tatizo lililosababishwa na mfumo mbovu wa elimu unaoleta watu/wataalamu uchwara wasio na ujasiri wa kuhoji na kushauri.

Hii yote ni kwa sababu hawajui ukweli na uelewa wao ni Mdogo. Mtu hawezi akawa anakosea then eti msomi anajitoa ufahamu na kumbebesha mtu mwingine lawama. It is a shame!!

Ukimsikiliza lisu yupo very clear.anatoa na way forward. Ccm and co,jueni mnachokipanda Leo ndicho mtakachovuna Leo. Vuteni kumbukumbu zenu nyuma kidogo muone aliyokuwa akiwashauri lissu,mkapuuza na matokeo take. Tizameni katiba mpya na mchakato mzima. Mliliingiza taifa hasara kubwa sana. Zile hela zingetumika kujenga hospital ngapi?miradi mingapi ya maji?

Mikataba haivunjwi tu hovyohovyo!!hata kama ni wewe kama investor lazima uhakikish emkataba unaoingia upo salamakwako kimaslahi. Sasa kama nyie mikataba mnasaini kwa kuwafuata hhotelini na wanaosaini ndo wale wapiga meza unategemea mini!! It is very clear. Mkitaka muwe salama jengeni timu imara ya kutengeneza mikataba. Na mnapotaka kuvunja mjataba wowote hiyo timu ishirikishwe .

Msiwe wabaguzi. Mnaacha kuchukua vichwa viwasaidie kisa wapinzani. Mnaishia kuchukua washangiliaji. What do you expect. Mtapigwa sana

NIWAULIZE KINA MPENDAZOE NA LUMUMBA WENZAKE;

1. MLIJUA KAMA NDEGE YETU ILIKAMATWA?
2. KAMA NDIO MBONA HAMKUTUSHIRIKISHA WATANZANIA WENZENU?
3.MBONA SASA MBAMSHAMBULIA ALIYETUHABARISHA?
4. ALIYEPELEKEA HASARA HIZI MNANJUA?
5. MNAAMINI KATIKA NJIA ILIYOTUMIKA KUVUNJA MKATABA?


BAADA YA HAYO HAPO JUU,WAJUE WANASIASA WALIPELEKEA NDEGE KUZUIWA:
1. MH MAGUFULI-MWANASIASA ALIYEVUNJA MKATABA ULIOPELEKEA HUKUMU ILIYOTUTAFUNA
2. MAHAKAMA-SI MWANASIASA
3. KAMPUNI-SI MWANASIASA

ng'amua mwenyewe

UKIJA KAMA UPEPO UNAPEPEA,UKIJA KAMA PEPO TUNAKEMEA

PEPO SHINDWAAAAAA
 
Watu wanalazimishwa kununua Efd kwa laki 8 kwa mtaji wa million moja...

Kwa ajiri ya kuwalipia watu deni nonsense issue kwa kweli ni upuuzi mkubwa......

Mi nadhani kwa hili bunge na mahakama wafanye kama kwa Zuma alipojenga kile kijiji kwa kodi za wa SA na huyu wetu arudishe pesa yetu.....
 
Ccm walikuwa wanasubiri Siku ya mnada ndio watanzania wajue kwamba ndege inauzwa,lissu mzalendo na muungwana kaamua kutustua kwamba ndege yetu inauzwa halafu kuna misukule inamlaumu,sasa angekaa kimya wakati Mali ya Tanzania inataka kupigwa mnada
 
Bàaadhi ya Watanzania wapumbavu kweli kweli kwani hiyo bilion inatoka mfukoni kwa nani??
dogo tangu ulipotimuliwa na shemeji yako kwake ukajitegemee ukapotea umerudi umebadilika unajibu kwa jazba. Ulizoea bando za bure kutoka kwa sister na miguu umekunja kwenye sofa. Sasa hivi umemvamia kaka yako uswaz bando za kubahatisha ukiingia jamvin jazba
 
Ili kuanza kuonyesha umuhimu wa kufanya maamuzi makini kwa ajili ya Taifa letu, hebu tuanze na hili deni la Bombardier, watanzania tukomae hizo bilioni 87 zinazodaiwa huko Canada, mzigo huo tusibebeshwe walipa kodi wa Tanzania, Bali deni hilo alilipe yeye mwenyewe aliyetusaababishia ambaye si mwingine bali baba Jesca!

Hapo ndipo akili zitamrudi na kujua kuwa suala LA kuongoza nchi siyo sawa na kuongoza familia yako ambayo unaweza kutembeza ubabe na kuwacharaza viboko wanao......

Kwenye kuongoza nchi ni lazima Rais aitii na kuilinda Katiba ya nchi ambayo aliapa kuitii na kuiheshimu kabla hajakabidhiwa madaraka, anapotokea Rais ambaye hataki kuitii na kuilinda Katiba ya nchi yetu, kama ambavyo aliwahi kutamka Baba wa Taifa letu Mwalimu Nyerere kuwa Rais wa aina hiyo HATUFAI.....

Mwalimu Nyerere aliendelea kwenda mbali zaidi kwenye hotuba hiyo kwa kueleza kuwa Rais wa aina hiyo analazimika kutuachia Urais wetu na yeye akafanye shughuli zake nyingine kama vile kufuga ng'ombe wake........
 
Hizo fedha zotakazolipa deni ni kodi za watanzania.
Usifikiri zitatoka kwenye mshahara wa JPM ,vijana wa chadema inabidi mjifuunze hata kidogo haya mambo ya kodi na jinsi fedha za serikali zinavyopatikana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazalendo wa kweli kwasasa wamebaki jina tu[emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji124] [emoji125] [emoji125] [emoji377] [emoji377] [emoji377] tupo wachache

nafight with my weather[emoji23][emoji23]
 
Sivuti bangi kutoka nje ya Tanzania lakini najua hiz 80b tunalipa sisi wenyewe wananchi na sio wenye nchi[emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji124] [emoji125] [emoji125] [emoji377] [emoji377] [emoji377]

nafight with my weather[emoji23][emoji23]
 
Ccm walikuwa wanasubiri Siku ya mnada ndio watanzania wajue kwamba ndege inauzwa,lissu mzalendo na muungwana kaamua kutustua kwamba ndege yetu inauzwa halafu kuna misukule inamlaumu,sasa angekaa kimya wakati Mali ya Tanzania inataka kupigwa mnada
That is very true.

Adui no 1 wa maendeleo ya watanzania sasa tushambaini kuwa kumbe ni Chama chetu cha CCM!

Hivi mkataba ulisainiwa na Waziri wa Ujenzi wa wakati huo ambaye ndiye Rais wetu wa sasa na yeye mwenyewe kwa hulka yake ya kutumia ubabe na utemi badala ya kufuata taratibu za kisheria akauvunja mkataba ule, halafu leo hii hiyo misukule ya Sisiem eti inamlaumu Tundu Lissu kuwa ndiye aliyesabsbisha kadhia hiyo!

Badala ya kumshukuru Tundu Lissu na kumuona shujaa nyiye mnamlaumu na kumwita eti kanunuliwa na hao mnaowaita wezi wa rasilimali zetu!

Hivi nyinyi maccm hizo akili zenu huwa mnaporwa na kulazimishwa mkaziweke rehani pale mtaa wa Lumumba?

Kwa kuwa haiingii akilini namna mnavyoweza kutokwa na mapovu kwa ajili ya kumtetea huyo mtu wenu ambaye ndiye dhahiri hilo lori lake analoliendesha linaelekea kutumbukia shimoni!

Wakati jambo hilo liko straight forward kabisa kuwa ni lazima yeye mwenyewe Mkulu wetu ajisearch toka mifukoni mwake alillpe hilo deni aliloisababisha yeye mwenyewe!

Tujikumbushe ule msemo unaosema kuwa kila mtu ataubeba mzigo wake yeye mwenyewe.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…