Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

Rais kwa Tanzania ni mtu mkubwa sana. Kama kweli mnasema L angekuwa adui ya JPM kama JPM. LIsu ataponaje. Kuweni na akili na acheni kuweka maneno kwa Rais. Hivi kweli mtz unashangilia. mtz anayeshangilia majanga yetu. Ndo tulipofika kweli. Watz mahali pote hawatakiani mema wivu na malengo mabaya. Sasa wananchi tunsahau kama nchi ni yetu. Sasa tumekaa nia yetu nchi ishindwe kutawalika na sie tubaki nyuma tunaumia. Kutumiwa na mabepari ni dalili mbaya sana .endeleeni na siasa. Lakini kama mnataka maendeleo Watz lazima kupitia kaa La moto.
Hakuna anaye shangilia Majanga Je hayo majanga yamefikaje, Sikia hili 'Any decision you make in life you are responsible for it'
 
Ukiwa mkweli kwenye taifa linaloabudu uongo hayo ndiyo mzara yake lazima mkweli atachukiwa,radhma lisu achukiwe kwa kuwa ni mkweli,lkn kwakuwa pia watanzania walio wengi uongo ndo sehem ya maisha yao,yanayofanywa na hao wanaodanganyaga watanzania kuwa msema kweli mpenzi wa mungu kumbe ni kinyume chake nchi hii inakoelekea ni pabaya sana,wacha tuabudu uongo iko siku tutaambiwa tutembee uchi na kwa upumbavu wa watanzania watatembea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu uzalendo wanahuubiri hawa jamaa mtanzania mimi siuhitaji.Ninarudia tena sina hajanao.Yakitukuta sisi utasikia "sitoi chakula cha msaada,bora mfe njaa" wakirikoroga wao utasikia "mniombee".

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ili kuanza kuonyesha umuhimu wa kufanya maamuzi makini kwa ajili ya Taifa letu, hebu tuanze na hili deni la Bombardier, watanzania tukomae hizo bilioni 87 zinazodaiwa huko Canada, mzigo huo tusibebeshwe walipa kodi wa Tanzania, Bali deni hilo alilipe yeye mwenyewe aliyetusaababishia ambaye si mwingine bali baba Jesca!

Hapo ndipo akili zitamrudi na kujua kuwa suala LA kuongoza nchi siyo sawa na kuongoza familia yako ambayo unaweza kutembeza ubabe na kuwacharaza viboko wanao......

Kwenye kuongoza nchi ni lazima Rais aitii na kuilinda Katiba ya nchi ambayo aliapa kuitii na kuiheshimu kabla hajakabidhiwa madaraka, anapotokea Rais ambaye hataki kuitii na kuilinda Katiba ya nchi yetu, kama ambavyo aliwahi kutamka Baba wa Taifa letu Mwalimu Nyerere kuwa Rais wa aina hiyo HATUFAI.....

Mwalimu Nyerere aliendelea kwenda mbali zaidi kwenye hotuba hiyo kwa kueleza kuwa Rais wa aina hiyo analazimika kutuachia Urais wetu na yeye akafanye shughuli zake nyingine kama vile kufuga ng'ombe wake........
mkataba huo na kesi hiyo ni 2009 JPM alikuwa rais?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lisu kiboko ya utawala wa awamu ya 5 anachofanya ni kuwavua nguo hadharani kisha anawapa kazi kina polepole na vijakazi wengine kazi ya kuwastiri mabosi zao.
 
Hivi Bombardier iliyozuiliwa ni nani kwani?? Je ni ya ATCL kama shirika la ndege au ni ya Tanzania kwa maana ya kwamba inamilikiwa na serikali?? Nikijibiwa hapo ndiyo naweza kuchangia. Maana yamkini hata wazungu nao wamekurupuka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ccm walikuwa wanasubiri Siku ya mnada ndio watanzania wajue kwamba ndege inauzwa,lissu mzalendo na muungwana kaamua kutustua kwamba ndege yetu inauzwa halafu kuna misukule inamlaumu,sasa angekaa kimya wakati Mali ya Tanzania inataka kupigwa mnada
Swali ni je ni kweli alihusika kwenye kuwaunganisha hiyo kampuni ya ujenzi inayoidai serikali na kampuni ya watengeneza ndege?Sina uhakika wa jibu Hilo.
 
Wanajitahidi sana kutumia nguvu kubwa kuaminisha umma kuwa bwana fulani ni mtu safi,mtendaji mzuri asie na kasoro na hivyo kutaka kuaminisha watu kuwa bwana fulani anafaa hata kuongezewa muda japo mwenyewe kazuga hana mpango huo.

Sasa tatizo ni pale bwana Lissu anapofunguka kwani hata akipata muda wa nusu saa tu kuongea basi inakwa shida kwani sumu anayotema ndani ya mudao huo mfupi inaharibu kila kitu cha Mh.na kumtoa kabisa kwenye reli na kusababisha watu kumuona hafai au kumtilia mashaka.


Yaani bwana mkubwa kila siku,kila dakika na kila sekendu anaitumia kutengeneza jina alafu anakuja kijana mmoja mharibu(bwana Lissu) anatumia nusu saa tu au lisaa limoja na dakika kadhaa tu na kuharibu kila kitu!

Yaani ni sawa na mkulima anatumia muda wake mwingi kuhudumia mahindi yake shambani na yanafikia hatua fulani alafu mara "nzige" wanaingia na ndani ya dakika kadhaa tu work done ya mkulima inakuwa ni sawa na zero.

Kijana kwa mwendo huu wa kuharibu shamba la watu,ujue ni lazima wakuchukie tu na angalie sana wasijie wakakushghulika kama nzige wanavyoshughulikiwa.
Lissu ni mwanasiasa mpumbavu tu. Badala ya kwenda jimboni kwake kumbana na umasikini uliokithiri wa ndg zake wanyaturu,yeye anapoteza muda kuibua uzushi kila kuchwapo. Ngoja 2020 aone kama atapata tena kofia ya ubunge.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili deni lipo toka 2009 nasikia, hizi ndege mbili za mwanzoni hazikukamatwa. Ila cha ajabu imekamatwa hii ya tatu.

Is this not an inside job of the traitors?
 
Mzazi hapendi kuambiwa mtoto wake ni mwizi hadi hapo atapokumbana na kipigo cha watu wenye hasira kali ndipo atakapojua kuwa mtoto wake alikuwa mwizi. Mkulu hapendi kuambiwa kuwa anachukua uamuzi kwa kurupuka hadi hapo maamuzi yake yatakapopelekwa kwenye mahakama za ki-mataifa na kushindwa ndipo anajua kuwa alikulupuka.

Tatizo la Lissu ni kumhurumia mkulu asifike huko, wangine wa kumwambia ambao ni washauri wake wa karibu kama mwanasheria mkuu wanaogopa kutumbuliwa
 
Hebu niambieni kwani lisu kafanya nini, haswa. Maana siku ya pili sasa kila mahali Lisu, tatizo nini ????? Kafanya nini ??? Kosa lake nini.

Mwenye hoja hebu aziweke wazi hapa siyo viroja. Wekeni hoja mezani.
Hana uzalendo kwa kuungana na wanaoihujumu Tanzania
 
Rais kwa Tanzania ni mtu mkubwa sana. Kama kweli mnasema L angekuwa adui ya JPM kama JPM. LIsu ataponaje. Kuweni na akili na acheni kuweka maneno kwa Rais. Hivi kweli mtz unashangilia. mtz anayeshangilia majanga yetu. Ndo tulipofika kweli. Watz mahali pote hawatakiani mema wivu na malengo mabaya. Sasa wananchi tunsahau kama nchi ni yetu. Sasa tumekaa nia yetu nchi ishindwe kutawalika na sie tubaki nyuma tunaumia. Kutumiwa na mabepari ni dalili mbaya sana .endeleeni na siasa. Lakini kama mnataka maendeleo Watz lazima kupitia kaa La moto.
Kama kuyazungumzia majanga yetu ni kushangilia basi wewe si mhenga wa Maemo wa , "ashakum si matusi"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom