Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

Ndugu, hujui unachokisema. Tunaipenda sana nchi yetu, ndiyo sababu hatutakaa kimya kuona watu wachache wanataka kuifanya ifilisike kwa maamuzi yao yasiyotumia akili bali nguvu kwenye karne ya 21.
Wewe hujui kuwa viongozi wapenda sifa huwa ni hatari kwa mustakabali wa Taifa? Maana watafanya kila wawezalo kufunika uchafu wao chini ya zulia na mwisho wa siku ni kilio chetu sote!!!
 
Usipindishe mada! Tujibu kwa ufupi.

Tunadaiwa hatudaiwi?

Ndege imekamatwa haijakamatwa?

Mlifanya siri au mliweka bayana haya mambo?
Awamu ya tano imewafutia hoja kabisa wapinzani.

Ni aibu na nadhani tunachekwa hata na majirani zetu kubaki tunajadili swala la madeni.

kwa ulimwengu wa sasa ni aghalab sana kukuta nchi isiyo na madeni.

Sijawahi kusikia madeni yamewahi kuwa kosa popote.

Marekani yenyewe anadeni la trilioni za dola kwa china; na bado wanaendelea na maisha hutasikia wakipoteza muda kama sisi.

Njooni na hoja mbadala za changamoto tunazokumbana nazo kama Taifa ila sio hivi vioja vya madeni.

America owes China $1tn. That’s a problem for Beijing, and Trump knows it
 
Unataka kumaanisha kua nikweli zile ndege za mwanzo zilikua ni USED, kama baadhi ya wadau walivyokua wakieleza? hivyo process ya ukamataji wa zile uwe tofauti na hizi ??
 
Hebu tusidanganyanye na kugeuzana kua watoto hapa!

>LISSU ndiye aliyevunja mikataba na wawekezaji?
>LISSU ndiye aliyeingia mikataba mibovu na wawekezaji?
>Lissu ndiye aliyewaita wazungu kuja kuwezeka nchini?
>LISSU ndiye anayetoa maamuzi kwenye Mahakama za kimataifa?
>LISSU ni nani hasa mpaka awaamrishe wazungu wakamate mali zetu?
>Hahakama zote,Takukuru na polisi kwanini wasimkamate Lissu kama anahongwa na wazungu?
>Tangu aanze kuhongwa na wazungu Lissu utajiri wake ukoje hadi sasa?

Tunapokosa la kuzungumza juu ya huyu mtanzania mwenzetu ni bora kukabakia kupambana na hali zetu.
 
Watanzania ni wajinga sana. Hatuna wasomi nchini. Mnamshambulia Lissu kwa kutuhabarisha ukweli mliotuficha kwa miezi kadhaa. Je, alichosema Lissu ni Uongo? Halafu mnakuja na majibu mepesi eti hizo njama kala Lissu na wapinzani. Kama Lissu na wapinzani wenzake wana nguvu kiasi hicho basi hao ndio wapewe uongozi wa nchi. Ninyi mna majeshi, wanasheria, bunge na vyombo vyote vya dola na vya kidiplomasia halafu mnamsingizia Lissu kwa madudu yenu. Ovyo kabisa nyie. Kuna methali inasema:

Mficha maradhi kifo humuumbua. Mkubali mumeumbuka kwa haya madudu na maradhi mliyokuwa mnatuficha
 
stroke: Kama madeni siyo hoja sasa mlikuwa mnaficha nini? Mbona sasa mapovu yanawatoka na mnaanza kuwasingizia wengine kwamba ndio waliosababisha na kutengeneza mgogoro?
 
Busara na hekima ni nguzo kuuu, ukitaja aibu za wenzako basi nawe kuwa tayari kutajwa za kwako, ukiwaita watu wapumbavu hadharani nao watataja upumbavu wako hadharani, heshima inaanza kwa mkubwa kumuheshimu mdogo na ndipo mdogo anajifunza kumuheshimu mkubwa
 
Mkuu shida ya kuweka uchama mbele ndio hii yaani lisu hta akiongea facts anaonekana ni mhaini..... sasa najiuliza lisu anaushawishi gani ndani ya serikali kiasi kwamba ACACIA wamhonge?? Yaani wamuache mwakyembe na kabudi wamuhonge lisu?? Does it make sense???

Hata haya mazungumzo na barrick ni kma wanataka kumkomoa lisu utaskia wachangiaje humu wanasema "lisu ataumbuka....cjui lisu atasemaje" yaani hawawazi barrick kuumbuka au mafisadi ya makinikia kuumbuka ila wao wanatafuta kumkomoa lisu!!!

Nachojua sio leo wala kesho ila kuna siku tu somehow somewhere tutamkumbuka lisu kwa haya yote anayosema sahvi na kuonekana chizi

Inanikumbusha siku mnyika kamuita kikwete dhaifu alitukanwa sana humu JF ila muda kma ulivyo mwalimu mzuri leo hii nani anaweza rudia matusi waliyompa mnyika 2012????

TIME WILL TELL
 
Kwani makanikia/magwangala ya wazungu wakati huo yalikuwa yamezuliwa???

Mchina wa jF.
Na washawasha!
Wakati wa ndege za kwanza? Sikumbuki vyema ila itakuwa bado yalikuwa hayajashikwa.

Yalivyokamatwa Yale ndio sokosoko lilianza, vichwa vikakaa, Lisu amongst them bila shaka, wakacalculate namna ya kuiumiza nchi ili alaumiwe presdaa.
 
Ajabu ya nini lipa deni acha maneno mengi kama umepewa talaka
Deni litalipwa, hasara roho, zitakazopotea kutokana na sabotages za Lisu na wenzake.

Tambua huyu Jamaa aliomba wafadhili walisusie taifa ili maskini wapate shida zaidi, ila wadhamini wakampuuza. Sasa amefanikisha alternative ingine ya kuumiza taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…